Wananchi na wabunge wao wakiwa kaatika maandamano ya kuangalia nyumba zilizochorwa alama nyekundu kwa ajili ya kubomolewa katika maeneo ya kuanzia Kimara, Mbezi hadi Kibamba. Maanadamano haayo yaliishia Kibanda cha Mkaa baada ya hali kuwa mbaya kwa msongamano wa magari
Naibu Katibu Mkuu wa CHADEMA na Mbunge wa Kibamba John Mnyika akiwafafanulia wananchi katika mkutano huo juu ya mipango ya barabara na sera za nchi juu ya mipaka
Mbunge wa Ubungo, Said Kubenea akitoa neno kwenye tukio hilo
Mbunge wa Ubungo Said Kubenea na Mbunge wa Kibamba Mnyika wakiwa katika mkutano huo
Askari wa kikosi barabarani akimuomba Mnyika kupanda gari ili kuzuia wananchi wasiendelee kuleta msongamano barabarani
Wananchi wakimlalamikia trafiki baada ya kuamuru Mnyika kuondokaeneo hilo la Kibanda cha Mkaa ambapo maandamano hayo ya kawaida yaliishia hapo. (PICHA ZOTE NA ANDREW CHALE,MO BLOG)
Wabunge wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) John Mnyika wa Jimbo la Kibamba na Mbunge wa Jimbo la Ubungo, Saed Kubenea wamejitokeza kwenye mkutano wa wazi uliofanyika jiioni ya leo eneo la Mbezi Mwisho ambapo wamesema wapo tayari kukaa meza moja na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mh. Dkt. Magufuli ili kuangalia utaratibu mwingine wa kuwaondoa wananchi ambao wanataakiwa kuondoka kupisha maeneo ya pembezoni mwa barabara ya Morogoro, ambapo wamepewa mwezi mmoja pekee kwa hatua hiyo amewataka wananchi waliokumbwa na zoezi hilo kujitokeza Mahakama Kuu ya Ardhi.
Kauli hizo zimetolewa leo na wabunge hao akiwemo Mbunge wa Kibamba, Mh. John Mnyika ambaye ameeleza kuwa, hapingani na Serikali, bali anataka haki itendeke kwa wananchi hao kwani wamepewa notisi ya mwezi mmoja tu na hawajajua fidia zao pia namna zoezi hilo likavyoathiri familia nyingi kwani wengine hadi sasa hawajui wataenda wapi.
“Narudia tena. Sipingani na maendeleo ya upanuzi wa barabara yetu. Ila tunaomba haki itende. Nawaombeni Madiwani andikeni barua ya kuonana na Rais pamoja na mie Mbunge wenu nitakuwepo kwenye hicho kikao. Tunahitaji haki. Kikubwa kwa sasa wananchi wote kesho asubuhi kuanzia saa mbili kwa wale waliowekewa alama ya kubomolewa tujitokeze kwa wingi Mahakama ya Ardhi kusimamisha zoezi hili kisheria” amesema Mnyika.
Hata hivyo baada ya kusema kauli hiyo na kufunga mkutano huo wa wazi, Mnyika alieleza kuwa, anataka kwenda kujionea maeneo hayo yaliyotiwa alama ya nyekundu ya X, ndipo kundi zima la wananchi waliokuwa kwenye mkutano huo kuungana na Wabunge hao naa kusababisha maandamano kwani wananchi wengi walijitokeza na kuunga msafara huo huku wakiimba nyimbo mbalimbalii walitembea kutoka sehemu hiyo ya Mkutano mpaka eneo la Kibanda cha Mkaa ambapo maandamano hayo yalisimama licha ya wananchi kuwa na hamu ya kutembea umbali mrefu ili kufikisha ujumbe wao.
Wananchi hao walikiwa wakisikika wakiimba “Tumechoka, Kubomolewa’ tumechoka kubomolewa” huku wengine wakiimba “Tanzania yetu sote, kwa nini tubomolewe” hata hivyo wakati Mnyika amewatuliza wananchi waishie hapo ili yeye aondoke kuendelea na majukumu yake baada ya Askari Polisi kueleza kwamba wananchi hao wanahatarisha usalama wa mambo mengine, Mnyika aliingia kwenye gari huku wananchi wakiwa na shahuku ya kulisukuma gari ilo, hata hivyo trafki aliamuru kuondoka mahala hapo na ndipo ukawa mwisho wa wananchi hao na kutawanyika
Mnyika ambaye pis ni Naibu Katibu Mkuu wa CHADEMA na Mbunge wa Kibamba awali katika mkutano huo alipokea kero mbalimbali huku kero kubwa ikiwa suala hilo la wananchi hao kuwekewa alama hizo nyekundu za kutakiwa kubomolewa pamoja na suala la Maji kwenye mabomba yao licha ya kuwekewa huduma ya mabomba.
Habari kutoka Mo Dewji Blog