Thursday, October 21, 2010

Tawi la Nyerere(CHADEMA) katika matawi ya NATO na Kosovo ya CCM na CUF




Kama ishara kuu ya kumuenzi Mwl.J.K.NYERERE siku ya Oktoba 14, 2010 nilizindua tawi la CHADEMA maeneo ya Manzese Bakhressa kwa jina la Mwl. Nyerere. Tawi hilo likiwa eneo sambamba na matawi ya vyama vingine vya siasa nchini yaliyopewa majina kama NATO na KOSOVO.

Nikifungua bendera ya CHADEMA na ipepee kwa wananchi wote ikisimamia ujumbe uliobebwa katika bendera hii ya CHADEMA. Ujumbe mzito na muhimu kwa Taifa zima la Tanzania

Hili ndilo Tawi la Mwl.J.K.NYERERE eneo la Manzese Bakhressa



Wananchi wengi sana walisitisha shughuli zao na kujumuika nasi katika tukio muhimu sana la kidemokrasia kufungua Tawi la Mwl.NYERERE eneo la Manzese Bakhressa


Peopleeeeeeeeeeeesssssssss.......Poweeeeeeeeeeeeeeeeeerrrrrrrrrrrrrr!!!!!!!!!!!!!

Moja ya vipaumbele vyangu ni MAJI!nawaendea wapiga kura huko wachotapo maji


Wakina mama huwa wakati mwingine wanakosa fursa ya kushiriki katika mikutano ya hadhara wakisaka maji. Nina wafata huko huko waliko wanakochota maji nikiwaelewesha namna nitakavyosimamia utatuzi wa kero ya maji

Diwani wangu Mushi wa Goba akilakiwa na wanaGOBA!Chagua madiwani wa CHADEMA!CHAGUA MNYIKA

Naipenda CHADEMAAAAAA....!!!

Wednesday, October 20, 2010

Tunaongeza mashina na mabalozi wa CHADEMA kila kona!!


Nikipandisha bendera katika moja ya mashina mapya ya CHADEMA kata ya Mabibo

Kabla ya kukamilisha mchakato wa ufunguaji rasmi wa shina ni muhimu kuelezea na kufafanua misingi, itikadi na nguzo za CHADEMA.

Monday, October 18, 2010

Mkutano wa hadhara wa Sinza

Makamanda mbalimbali wakihutubia mkutano wa sinza


Nikiwa na Diwani wangu Renatus Pamba wa Kata ya Sinza


Kamanda Eric Ongara, Engine!akihutubia wananchi wa kata ya sinza

Kamanda Edward Kinabo akihutubia mkutano wa Sinza

Mkutano wangu uliweza kuhudhuriwa na vyombo mbalimbali vya habari kikiwemo BBC ambao licha ya kurekodi na kurusha mkutano pia walifanya mahojiano nami baada ya kumalizika kwa mkutano

Polisi walikuwepo pia kulinda amani licha kwa muonekano wao(mavazi, silaha nk) uliondoa amani kwa kuleta hofu kwa wananchi ambao walikuwa wakifatilia mkutano kwa utulivu




wananchi walinilaki baada tu ya kumaliza kuhutubia!Nashukuru sana kwa moyo na hamasa kubwa mliyoionyesha wana wa sinza.

Usimikaji wa mabalozi wa CHADEMA Kata ya Sinza




Sinza yazizima!-Chaguo lao MNYIKA na Diwani Pamba II




Sinza yazizima!-Chaguo lao MNYIKA na Diwani Pamba

Sinza yazizima!-Chaguo lao MNYIKA na Diwani Pamba





Saturday, October 16, 2010

Pale mwanaCCM alipompigia saluti MNYIKA!


Ewe mwananchi fanya uamuzi sahihi-AMUA!!

Ewe mwananchi, makala zimeandikwa, katuni zimechorwa, picha zimepigwa, nyimbo zimeimbwa, hotuba zimetolewa. Hakika ni wakati wako sasa kufanya uamuzi sahihi.

"Uchaguzi Mkuu wa mwaka 2010 ni baina ya UADILIFU na UFISADI, baina ya UMAKINI na USANII, baina ya HAKI na DHULUMA, baina ya Dr.Slaa na Kikwete, na kwa jimbo la Ubungo chaguo ni moja tu MNYIKA!!"

Wednesday, October 13, 2010

Mnyika kufungua Maadhimisho ya siku ya Nyerere Ubungo

Mgombea Ubunge Jimbo la Ubungo,John Mnyika ambaye pia ni Kaimu Katibu mkuu wa CHADEMA ataongoza wanachama na wapenzi wa chama hicho ktk maadhimisho ya siku ya Nyerere tar14Oktoba.Maadhimisho hayo yatafanyika ktk eneo la Manzese darajani.

Pamoja na hotuba zitakazotolewa Mnyika atazindua rasmi Tawi la Mwl Nyerere ktk mtaa wa Mwongozo.Uzinduzi huo utafuatiwa na ufunguzi wa matawi mengine ktk maeneo mbalimbali na kumalizia na Mkutano wa hadhara ktk mtaa wa Sisi kwa Sisi.

CHADEMA inamuenzi Mwalimu kwa vitendo kwa kupambana na ufisadi ,kutetea rasilimali za taifa na kuhakikisha fursa kwa wote ikiwemo kutoa huduma kama elimu bure.

Mnyika anaendelea na kampeni ambapo tar12 amehutubia kata ya msigani,tar13 amehutubia Kwembe na tar 15 anatarajia kuwa Kimara.

Tuzidi kuwa Pamoja!!

Tuesday, October 12, 2010

Hawa wananichangia na kuniunga mkono-Unasubiri nini wewe?

Wakina mama hawa na watoto wao walinigusa sana kwa moyo wao wa kizalendo kwa kuweza kunichangia kampeni zangu katika zoezi la uchangishaji nilifanyalo katika mikutano ya hadhara. Wewe unangoja nini?shiriki katika mchakato wa kuhakikisha ushindi kivitendo.

Changia sasa chochote ulichonacho!waweza tuma kupitia MPESA (0754 694553) ama ZAP (0784-222222)

Waweza pia kuchangia kwa kutuma salio la muda wa maongezi katika simu "vocha" kwa ambao mpo mbali na huduma hizi.

Wahi sasa kununua Vifaa vya NAMUUNGA MKONO MNYIKA-Ushiriki kivitendo kampeni zangu

Wheel covers zipo za ukubwa wote; Tsh. 30,000/- tu!

Stickers ni Tsh. 1,000/- tu! weka katika gari, mlangoni nk

Shiriki sasa kwa vitendo, Niunge Mkono na ufanye kampeni nami;
Pata vifaa hivi pamoja na vingine vingi kama;
Fulana (Tsh. 10,000/-), Skafu Tsh. 5,000/-


Wasiliana na: 0783-222217, 0713-503023, 0714-137371


Wahi sasa!

Hujuma!!! Uvunjwaji wa Sheria





Hii ni sehemu tu ya picha ambazo zimechanwa katika maeneo ya Jimbo la Ubungo. Uchanwaji wa picha huu ni kosa kisheria. Lakini pia hurudisha nyuma sana zoezi zima la upashaji habari ukizingatia uhuru wa kupata taarifa ni moja wapo ya nguzo imara katika demokrasia. Mwelimishe mwenzako kutokuhujumu mchakato wa kidemokrasia kwa kuchana picha kwani inakosesha fursa wananchi wengine wengi kupata taarifa za wagombea.