MHE. JOHN MNYIKA AMTAKA RAIS ATEUE WAZIRI WA NISHATI NA MADINI KUONGOZA MAJADILIANO KUHUSU MADINI
Mbunge wa Jimbo la Kibamba, ambae ni Waziri kivuli wa nishati na madini, Mhe. John Mnyika, akiongea katika Mkutano wa hadhara Jana Jumatano 2/8/2017 eneo la Goba mwisho katika Jimbo la Kibamba, Mhe. Mnyika amemtaka Rais Magufuli ateue Waziri wa nishati na madini ili aongoze majadiliano kuhusu madini.
"Ni muda mrefu umepita Rais ajateua Waziri wa nishati na madini, ambae ndiye anayestahili kuongoza majadiliano kuhusu madini, badala yake anamuachia Waziri wa Katiba na Sheria kuongoza majadiliano kuhusu masuala ya madini, Ameamuachia Waziri wa Katiba na Sheria kwa sababu alikuwa kwenye tume ya mabadiliko ya Katiba, nae amekataa kuendeleza mabadiliko ya Katiba mpya" amesema Mnyika.
Amesema Serikali makini isingeanza na makinikia huku madini yanaendelea kuchimbwa na kutoka, wakati kuna makampuni mengine yanaendelea na uchimbaji, na kampuni inayoingoza kwa uzalishaji ni kampuni ya Geita Gold mine (GGM) na inaendelea na uchimbaji hakuna ufuatiliaji wala majadiliano yeyote yanayoendelea, huku Taifa likielekezwa kwenye majadiliano kuhusu makinikia badala yafanyike majadiliano kuhusu madini kwa upana wake.
KATIBA MPYA
Mwaka 2010, akiwa Rais Kikwete, Mnyika ndiye aliyeibua mjadala kuhusu Katiba mpya ambapo ilipelekea hatua mpaka Rais Kikwete akaanzisha mchakato wa kipatikana Katiba mpya.
Mnyika ameahidi katika Bunge lijalo litakaloanza Septemba 5 mwaka huu kuanzisha tena mjadala mpya utakaopelekea kupatikana kwa Katiba mpya ambayo ndiyo suluhisho ya mambo mengi yanayoendelea.
KUHUSU MIRADI NA KERO JIMBONI
Katika mkutano huo wananchi walipata nafasi ya kuuliza maswali mbalimbali yanayohusu miradi na kero mbalimbali katika Jimbo, ambapo alisimama Mstahiki Meya wa Ubungo, Mhe. Boniface Jacob ambae alijibu maswali mbalimbali ya wananchi, pia kuwataka vijana na wakina mama kujitokeza kwa wingi kwani kuna mikopo ambayo inatolewa kwa ajili ya kufanya ujasiriamali na kujiendeleza katika mambo mbalimbali.
Na Sunday Urio
Katibu Msaidizi wa Mbunge, Jimbo la Kibamba