Monday, November 30, 2009

Ripoti ya Kundi la Wataalamu wa UN: Wembe huu leo utamkata Waziri Membe

Waziri wa Mambo ya Nje na Mahusiano wa Kimataifa, Benard Membe amekurupuka na kuibeza ripoti ya Kundi la Wataalamu wa Umoja wa Mataifa(UN) ambayo imeitaja Tanzania na baadhi ya watanzania kuhusika moja kwa moja na biashara haramu ya silaha na madini huko DRC ambayo inawezesha vikundi vya waasi kuendeleza vita yenye kupoteza maisha ya raia. Ama hakika waziri Membe amelilia wembe, na leo utaanza kumkata.
Kwa nafasi yangu ya Mkurugenzi wa Mambo ya Nje na Mahusiano wa Kimataifa nitafanya mkutano na waandishi wa habari na kuichambua ripoti husika. Serikali ijiandae 'mabomu' ya leo yatarushwa Wizara za: Mambo ya Nje na Mahusiano ya Kimataifa; Ulinzi; Utawala Bora; Usalama wa Raia; Nishati na Madini; Viwanda na Biashara; Wizara ya Miundombinu; Wizara ya Maliasili na Utalii na Wizara ya Fedha.
Natarajia mkutano utafanyika saa 5 asubuhi katika ofisi za Makao Makuu ya CHADEMA. Kwa maelezo zaidi wasiliana nami kupitia 0754694553. Vita ni vita Mura!
JJ

No comments: