Nipo bungeni lakini nimepokea taarifa za mafuriko katika maeneo mbalimbali jimboni kama Kibamba, Malambamawili, Makoka nk Nimeshatoa maelekezo kwa Katibu Msaidizi wa Ofisi ya Mbunge Ubungo kufatilia kwa ukaribu na kuzitaarifu mamlaka husika kwa hatua za haraka.
Kwa maeneo mengine yenye mafuriko tafadhali mpeni taarifa kupitia: 0715-379542 au 0784-379542
2 comments:
Mheshimiwa Mnyika pole na majukumu ya hapa na pale pamoja na Mchakato ya katiba mpya.Mungu yupo pamoja nanyi itapatikana iliyo bora.Ila watu wa ubungo tuna tatizo la maji mwezi wa pili sasa hatupati maji na hatuambiwi sababu.Mimi natoka Ubungo Msewe tulikuwa tunapata maji walau mara mbili kwa wiki sasa hatupati kabisa.maji ni muhimu sana kwa maisha ya mwanadamu.
Tusaidieni Mbunge wetu bado tunakuamini sana tu
Mbunge yuko bize kutuaharibia nchi ashawasahau nyie mfe tu na kiu
Post a Comment