Wednesday, February 25, 2015

CHADEMA: YANAYOJIRI NJOMBE - BVR



1. Ikiwa zoezi la uandikishaji limeanza leo tarehe 23 Feb na likitarajiwa kuzinduliwa rasmi kesho tarehe 24 Feb na Waziri Mkuu Pinda, Naibu Katibu wa CHADEMA upande wa Tanganyika ameanza Operesheni R2R BVR ambapo asubuhi mpaka mchana alikuwa katika Mji wa Makambako akipitia mitaani pamoja na msafara wa viongozi wa chama hicho ngazi mbalimbali kuhamasisha wananchi kujiandikisha.

Aidha, Operesheni hiyo imehusisha kukagua utaratibu wa uboreshaji kwa kutumia BVR kwenye vituo mbalimbali ambapo imebainika kwamba udhaifu uliokuwepo wakati wa majaribio na mwingine mpya umebainika katika sehemu kubwa ya vituo vilivyotembelewa.

Baada ya kubaini udhaifu huo Mnyika na timu ya maafisa wa CHADEMA iliyoweka kambi katika mkoa wa Njombe ikihusisha wataalamu wa TEHAMA (ICT) wamekutana na Mkurugenzi wa NEC Mallaba na kueleza kuhusu udhaifu huo.

Mfano katika kituo cha Malombwe mpaka saa 6 mchana mashine zilikuwa hazifanyi kazi. Hali kama hiyo imejitokeza katika kituo kituo cha Liamkena ambapo uandikishaji ni taratibu kwa kiwango mpaka saa 4 waliandikishwa watu watano tu.

2. Aidha, pamekuwepo na tatizo la watu wenye mikono yenye vidole sugu kutokana na kufanya kazi ngumu mashine kugoma kuwatambua na hivyo kukataliwa kujiandikisha.

Hali kama hiyo imejitokeza mfano katika kituo cha Sigfrid, Malombwe na vituo mbalimbali. Kufuatia hali hiyo ambapo Operesheni R2R BVR iliamua kutembelea vituo zaidi na kubaini kwamba vipo ambapo mashine hazikuwa zikifanya kazi kabisa mathalani Lumumba.

Kwa ujumla katika vituo vingi ukiondoa matatizo ya mashine upo pia udhaifu wa waandikishaji na waendeshaji wa vifaa vya BVR (Kit Operators) ambao wanashindwa kutumia mashine hizo na walipohojiwa baadhi walikiri kwamba wamepewa mafunzo siku moja kabla ya kuanza uandikishaji huku wakiwa hawajawahi kutumia kompyuta wala kuwa na ujuzi wa ICT.

Wapo waandikishaji ambao walionyesha kutokuwa na ufahamu wa upigaji picha na hivyo kufanya zoezi kwenda taratibu na pia kupiga picha zinazoonekana vibaya.

Kasi ndogo ya uandikishaji huku siku zikiwa saba na kwa kituo inaashiria bayana kwamba wapo wananchi ambapo mwishowe watakosa fursa ya kujiandikisha.

Operesheni R2R BVR imebaini mpaka sasa kuwa pamoja na kutumia alama za vidole mfumo umeacha mianya mpiga kura kujiandikisha zaidi ya mara moja katika vituo tofauti tofauti kwa kuwa hakuna mawasiliano ya kimfumo kati ya kituo kimoja na kingine.

Mfumo unategemea kwamba taarifa zikitumwa kanzidata kuu (central databank) ya tume ndiyo itakayochambua wakati ambapo hakutakuwa na mawakala katika hatua hiyo kuthibitisha uondoaji wa wapiga kura waliojiandikisha zaidi ya mara moja kwa kuzingatia kwamba katika kipindi cha uhakiki wa daftari la awali napo hakuna mwingiliano baina ya daftari la eneo kwa eneo wakati wa ukaguzi.

Aidha, CHADEMA imeweka mawakala katika vituo vyote lakini wanapata vikwazo vya namna vya kudhibiti uchakachuaji katika hatua ya usafirishaji wa takwimu ambapo mifumo miwili inatumika kwa wakati mmoja; wa kutumia simu na ule wa kuhamisha kwa kutumia kifaa cha kuhifadhi taarifa (flash drive) bila uhakiki wa mawakala.

Operesheni R2R BVR katika mazingira hayo haitaishia tu kuwa na mawakala kwenye vituo bali kukagua mfumo mzima.

4. Naibu Katibu Mkuu Mnyika ametaka Waziri Mkuu Mizengo Pinda katika uzinduzi wa BVR Makambako tarehe 24 Feb aeleze namna Serikali ilivyoiwezesha tume kushughulikia udhaifu huo kwa kuzingatia kwamba mabilioni yametumika kwenye zabuni ambayo imeleta vifaa vibofu hali inahitaji uchunguzi kufanyika kubaini iwapo hali hiyo imetokana na ufisadi au imefanywa makusudi kuachia mianya ya uchakachuaji katika uchaguzi.

Mara baada ufuatiliaji huo jioni ya leo patafanyika Mkutano wa uzinduzi wa Operesheni R2R BVR jukwaani katika Jimbo la Njombe Kusini na kesho kutwa tarehe 25 Operesheni R2R inahamia wilaya ya Wang'ing'ombe kwenda kuhamasisha wananchi kujiandaa kujiandikisha.
Tumaini Makene
Mkuu wa Idara ya Habari na Mawasiliano -CHADEMA

1 comment:

Unknown said...

Nashauri kwenye ilani yenu muweke mambo haya:
(KWANZA)
Wafanyakazi wa serikali ni kama 500,000 but ukichanganya na wake zao na waume zao na watoto wao na wazazi wao jumla yaweza kufika 3,000,000 sasa hizi ni kura nyingi kama utazipata, sasa ili kupata kura za wafanyakaz unaweza kuweka katika ilani suala la

• motisha kwa wafanyakazi wa serikali
kivipi:
ni kwamba unaweza kuahidi ku-index GDP growth kwa mishahara ya wafanyakazi, kwamba pato la ndani (GDP) likiongezeka mishahara nayo inaongezeka automatically, hii itasaidia wafanyakaz watachapa kaz kwa bidii wakijua kuwa ongezeko lolote litawaletea tija, na serikali na vyombo vyake watajitahidi kupima sawasawa hili ongezeko ili lisiwe overstated or understated, kwa zaidi isiwe overstated na kwa namna hii tutakuwa na takwimu za uhalisia za kukua kwa GDP na effort za wafanyakazi zitaongezeka katika uzalishaji

pia tunaweza ku-index inflation rate katika mishahara ya watumishi wa serikali, hii ni motisha wakati wa inflation kuwasaidia kupambana na ongezeko la bei za vitu; hii itasaidia serikali pia katika kupima inflation kiuhalisia ili isipandishe mishahara ya wafanyakazi bila ukweli na itaifanya serikali kupambana na indicator zozote zinazofanya bei zipande, so utagundua hii ni motisha kwa wafanyakazi lakini pia inasaidia utendaji wa serikali.

(PILI)
Jambo lingine ni kuweza kupata kura za vijana walioko vyuoni sasa na ambao wanategemea kwenda chuo wakati wowote ujao na makundi ya watu wengine ambao wana vipaji Fulani katika michezo ila hawako kwenye mfumo wa shule:
Kundi hili nalo ni kubwa sana, linakadiriwa kuwa na watu 3,000,000, so kura hizi nazo ni nyingi;
Unazipataje hizi:
Ni kujenga fitness facility za kiwango cha kimataifa na kuweka kila kitu humo, gym, kuogelea, kukimbia, basketball, volleyball, tenes, badminton, kwenye gym kuwe na kunyanyua uzito, kurusha visahani, high jump, long jump….i just mention few, lakini namaanisha kila sport ambayo iko Olympic games itoke hapo, hapa US, vyuo ndio chimbuko la michezo hiyo, badala ya kusoma tu wanafunzi wanaendeleza vipaji vyao hadi kuwa professional, nakumbuka nikiwa secondary school nilicheza na jamaa mmoja hivi alianza kuwa kwenye timu ya shule ya football tangu akiwa form one na alikuwa anacheza kiungo cha ukwel, form four hakufanya vizuri na ule mpira uliishia pale coz sa ivi huyo jamaa ni dereva taxi hapa Manyanya Kinondoni, ni kipaji kimepotea, hapa US watu kama hao wanachukuliwa na kukopeshwa ada huku kipaji chake kikikuzwa mwisho wa siku anakuwa profession, katika hizi facilities za mazoezi za vyuo watu wengine wanaruhusiwa wanalipa kiwango kidogo cha pesa lakini wanabenefits kupatiwa mafunzo na wataalamu walioko kwenye hizi facilities na wanafika mbali pia kimchezo, na hapa ndio unapoona tofauti kati yetu sisi na hawa jamaa because anafundishwa vitu hivi tangu mtoto, nimeona watoto wa umri wa kwaka mmoja anafundishwa kuogelea, huyu huwezi kumshindanisha na mtanzania ambaye ameanza kujifunza na age ya 15-20; unaweza kufanya utafiti wako katika hili but mkiliweka vizuri katika ilani kuna uwezekano wa kupata kura nyingi sana za vijana na wapenda michezo na baadae hii itasaidia nchi katika michezo ya Olympic and other profession games,

Cha kufanya ni kwa kuanza kujenga hizi complex moja kila chuo e.g. UDSM, SUA au MZUMBE au vyote viwili, SAUT-mwanza, Mzumbe-mbeya, MUCOBs-moshi na SAUT-Mtwara

by kassim mwarabu,
United States of America,
mobile: +1 614 815 9503