Naibu Katibu Mkuu Bara alifanya mkutano na waandishi wa habari kutokea Ngome ya UKAWA Kawe Jijini Dar jana 03.10.2015, zifuatazo ni dondoo za aliyoyazungumza
Mnyika: Hatujaridhika na majibu ya Jaji Lubuva kuhusu udhaifu wa BVR na uchakachuaji wa kura
Mnyika:
UKAWA Tunataka tume ya Uchaguzi itupe nakala tete (soft copy) ya nakala
ya Daftari la wapiga kura. Kinachoendelea ni ucheleweshaji!
Mnyika:
Tume iseme kwanini hawatoi daftari la wapiga kura?Na ni lini daftari
litatolewa?UKAWA haipo tayari kusubiri Siku 8 kabla ya Uchaguzi
Mnyika: Ili kuepusha vurugu kwenye Uchaguzi daftari hili litolewe kuanzia Leo!
Mnyika:
Tume ya Uchaguzi waeleze kwanini wameamua kuchelewa kukutana na vyama
vya siasa juu ya suala la kupewa soft copy ya Daftari!
Mnyika:
Tume imejibu ipo tayari kutoa fursa ya Vyama vya siasa kukagua mfumo wa
kujumlisha kura ila hawasemi ni lini? Hizi ni delay tactics
Mnyika: kuna haja ya kuwa na mashaka, mfumo wa kompyuta unaweza kuchezewa, lazima mfumo huu uhakikiwe
Mnyika: Tume imesema wana mfumo miwili ya kujumlisha kura. Lazima mfumo yote ihakikiwe na watalaamu wetu vyama vya siasa!
Mnyika: UKAWA tunasisitiza tena, ukishapiga kura, kaa mita 200 subiria matokeo, ili kuzuia mianya yote ya wizi!
Mnyika:
Wananchi waendelee kupuuza kauli ya Mwenyekiti wa Tume, wasiondoke
baada ya kupiga kura, wabakie mita 200 nje ya kituo kusubiria!
Mnyika:
Matokeo kutangazwa na wanahabari sio hisani, ni suala la kisheria.
Kutangaza matokeo itamkwe ni haki ya msingi ya kila mtu.
Mnyika:
Kila Mwananchi afanye ujumlishaji wa kura "parallel voter tabulation"
ili wananchi wajue hakuna uchakachuaji na wizi wa kura!
Mnyika:
Kazi pekee ya Tume iwe ni Kumtangaza Mshindi, lakini haki ya kutangaza
matokeo iwe ni kwa kila mdau wakiwemo waangalizi wa Uchaguzi
Mnyika:
Naungana mkono na wanahabari kuwa wasikubali watu wenye press card
pekee kutangaza matokeo! Hii itapanua wigo wa Habari kusambaa
Mnyika: wanahabari Nawaomba msambae kwenye vituo mbalimbali ili muweze kutangaza matokeo!
Mnyika: Ukiangalia mazingira hivi sasa, bado hakuna mazingira mazuri ya maandalizi ya huu Uchaguzi!
Mnyika:
Sera ambazo UKAWA inaendelea kuzitangaza kupitia @edwardlowassatz sisi
wengine tunaendelea kudai mazingira ya Uchaguzi yaboreshwe!
Mnyika:
Rais wa nchi ameiingilia Tume tangu Uchaguzi uanze, alikataa Katiba
Mpya ya wananchi, alikataa maazimio ya TCD juu ya tume huru
Mnyika: Rais alienda kinyume na ahadi zake kuhusu marekebisho ya Tume ya Uchaguzi.
Mnyika: Rais anapoenda kwenye Tamasha la Amani kesho, aombewe ili aweke mazingira mazuri ya Uchaguzi
Mnyika: Wananchi wamuombee Jaji Lubuva ili awe na ujasiri wa kutangaza matokeo ya Rais Mpya wa Tanzania
Mnyika: Kesho Rais akiongea naomba aeleze mkakati wake amejiandaaje kukabidhi Madaraka kwa Amani kufuatia Mabadiliko ya tarehe 25.10.2015
Mnyika:
Jaji Lubuva alisema atakutana na vyama vya siasa ila hakutaja tarehe!
Kuhusu daftari hakujibu hoja yetu ya kupewa "Daftari"
Mnyika: kama Tume ina dhamira, itoe Daftari la wapiga kura na sio orodha ya wapiga kura, waitoe hata leo!
Mnyika:
Tume imesema watatoa haki kwa waliopoteza kadi za kupiga kura,
wanadanganya! Wanaotakiwa kupiga kura ni walipo kwenye Daftari!
Mnyika:
Tume wanachelewesha Daftari ili mawakala wetu vituoni wasiwe na daftari
linalofanana na daftari la wasimamizi wa Uchaguzi
Mnyika: Tunayasema haya kwa sababu tuna uhakika wa kushinda, na Tunataka mazingira mabaya ya Uchaguzi yarekebishwe mapema
Mnyika:
Daftari la wapiga kura likiwa 'bovu' tayari goli la mkono
limeshafungwa! Mfumo wa kujumlisha kura ukiwa 'mbovu' ni goli la mkono!
Mnyika: Kabla ya tarehe 25 Oktoba tunasisitiza wasiondoke, wakae umbali unaoruhusiwa kisheria, walinde kura zao!
Mnyika:
Wananchi wa Dar es Salaam, nawahimiza wao waende kwenye kituo cha
majumuisho ya kura cha Taifa kwa niaba ya WaTZ wengine!
Mnyika: Wananchi walinde kura zao kwa amani!
No comments:
Post a Comment