Sunday, October 4, 2015

Dondoo za mkutano wa pili na waandishi wa habari kuhusu Uchaguzi

Naibu Katibu Mkuu Bara alifanya mkutano na waandishi wa habari kutokea Ngome ya UKAWA Kawe Jijini Dar jana 03.10.2015, zifuatazo ni dondoo za aliyoyazungumza

Mnyika: Hatujaridhika na majibu ya Jaji Lubuva kuhusu udhaifu wa BVR na uchakachuaji wa kura

Mnyika: UKAWA Tunataka tume ya Uchaguzi itupe nakala tete (soft copy) ya nakala ya Daftari la wapiga kura. Kinachoendelea ni ucheleweshaji!

Mnyika: Tume iseme kwanini hawatoi daftari la wapiga kura?Na ni lini daftari litatolewa?UKAWA haipo tayari kusubiri Siku 8 kabla ya Uchaguzi

Mnyika: Ili kuepusha vurugu kwenye Uchaguzi daftari hili litolewe kuanzia Leo!

Mnyika: Tume ya Uchaguzi waeleze kwanini wameamua kuchelewa kukutana na vyama vya siasa juu ya suala la kupewa soft copy ya Daftari!

Mnyika: Tume imejibu ipo tayari kutoa fursa ya Vyama vya siasa kukagua mfumo wa kujumlisha kura ila hawasemi ni lini? Hizi ni delay tactics

Mnyika: kuna haja ya kuwa na mashaka, mfumo wa kompyuta unaweza kuchezewa, lazima mfumo huu uhakikiwe

Mnyika: Tume imesema wana mfumo miwili ya kujumlisha kura. Lazima mfumo yote ihakikiwe na watalaamu wetu vyama vya siasa!

Mnyika: UKAWA tunasisitiza tena, ukishapiga kura, kaa mita 200 subiria matokeo, ili kuzuia mianya yote ya wizi!

Mnyika: Wananchi waendelee kupuuza kauli ya Mwenyekiti wa Tume, wasiondoke baada ya kupiga kura, wabakie mita 200 nje ya kituo kusubiria!

Mnyika: Matokeo kutangazwa na wanahabari sio hisani, ni suala la kisheria. Kutangaza matokeo itamkwe ni haki ya msingi ya kila mtu.

Mnyika: Kila Mwananchi afanye ujumlishaji wa kura  "parallel voter tabulation" ili wananchi wajue hakuna uchakachuaji na wizi wa kura!

Mnyika: Kazi pekee ya Tume iwe ni Kumtangaza Mshindi, lakini haki ya kutangaza matokeo iwe ni kwa kila mdau wakiwemo waangalizi wa Uchaguzi

Mnyika: Naungana mkono na wanahabari kuwa wasikubali watu wenye press card pekee kutangaza matokeo! Hii itapanua wigo wa Habari kusambaa

Mnyika: wanahabari Nawaomba msambae kwenye vituo mbalimbali ili muweze kutangaza matokeo!

Mnyika: Ukiangalia mazingira hivi sasa, bado hakuna mazingira mazuri ya maandalizi ya huu Uchaguzi!

Mnyika: Sera ambazo UKAWA inaendelea  kuzitangaza kupitia @edwardlowassatz sisi wengine tunaendelea kudai mazingira ya Uchaguzi yaboreshwe!

Mnyika: Rais wa nchi ameiingilia Tume tangu Uchaguzi uanze, alikataa Katiba Mpya ya wananchi, alikataa maazimio ya TCD juu ya tume huru

Mnyika: Rais alienda kinyume na ahadi zake kuhusu marekebisho ya Tume ya Uchaguzi.

Mnyika: Rais anapoenda kwenye Tamasha la Amani kesho, aombewe ili aweke mazingira mazuri ya Uchaguzi

Mnyika: Wananchi wamuombee Jaji Lubuva ili awe na ujasiri wa kutangaza matokeo ya Rais Mpya wa Tanzania

Mnyika: Kesho Rais akiongea naomba aeleze mkakati wake amejiandaaje kukabidhi Madaraka kwa Amani kufuatia Mabadiliko ya tarehe 25.10.2015

Mnyika: Jaji Lubuva alisema atakutana na vyama vya siasa ila hakutaja tarehe! Kuhusu daftari hakujibu hoja yetu ya kupewa "Daftari"


Mnyika: kama Tume ina dhamira, itoe Daftari la wapiga kura na sio orodha ya wapiga kura, waitoe hata leo!

Mnyika: Tume imesema watatoa haki kwa waliopoteza kadi za kupiga kura, wanadanganya! Wanaotakiwa kupiga kura ni walipo kwenye Daftari!

Mnyika: Tume wanachelewesha Daftari ili mawakala wetu vituoni wasiwe na daftari linalofanana na daftari la wasimamizi wa Uchaguzi

Mnyika: Tunayasema haya kwa sababu tuna uhakika wa kushinda, na Tunataka mazingira mabaya ya Uchaguzi yarekebishwe mapema

Mnyika: Daftari la wapiga kura likiwa 'bovu' tayari goli la mkono limeshafungwa! Mfumo wa kujumlisha kura ukiwa 'mbovu' ni goli la mkono!

Mnyika: Kabla ya tarehe 25 Oktoba tunasisitiza wasiondoke, wakae umbali unaoruhusiwa kisheria, walinde kura zao!

Mnyika: Wananchi wa Dar es Salaam, nawahimiza wao waende kwenye kituo cha majumuisho ya kura cha Taifa kwa niaba ya WaTZ wengine!

Mnyika: Wananchi walinde kura zao kwa amani!