Wednesday, July 27, 2016

ZIARA YA UKAGUZI WA SHULE ZILIZOKO NDANI YA KATA YA KWEMBE





OFISI YA MBUNGE JIMBO LA KIBAMBA PAMOJA NA DIWANI KATA YA KWEMBE IMEFANYA ZIARA YA UKAGUZI WA SHULE ZILIZOKO NDANI YA KATA YA KWEMBE ILI KUONA CHANGAMOTO MBALIMBALI ZINAZOKUMBA SHULE HIZO PAMOJA NA UKAGUZI WA MADAWATI YALIYOFIKISHWA KUNAKO SHULE HIZO.
Ofisi ya Mbunge jimbo LA kibamba imefanikiwa kufika ktk shule zilizoko Kata ya Kwembe huku ikiwakilishwa na mwakilishi toka ofisi ya Mbunge Ms. SUNDAY URIO pamoja na Diwani wa Kata hiyo Mhe. DWEZA KOLIMBA ili kujionea hali halisi na changamoto zinazozikabili shule hizo.
Katika ziara hiyo tumebaini changamoto zifuatazo:
*Uhaba wa madarasa ya kusomea watoto hao. Huku mhe. Diwani KOLIMBA akalijibia swala hili kwa kusema, ni kweli ameona changamoto hiyo ndani ya shule zilizoko ktk Kata na kwamba atashirikiana bega kwa bega na wananchi wa Kata yake pamoja na wadau mbalimbali wa elimu pasipo kumsahau mhe. Mbunge JOHN JOHN MNYIKA ktk kufanikisha swala zima la kuwezesha elimu bora ndani ya Kata ya Kwembe pamoja na jimbo zima LA kibamba.
*Uhaba wa madawati ya kukalia wanafunzi hao. Napo hapa mhe Diwani KOLIMBA alisema kwamba, japo kuna madawati yamewasilishwa ktk shule zilizoko ndani ya Kata yangu bado natambua uhaba huo ya kwamba hayatoshelezi...na kwasababu hiyo basi manispaa ya kinondoni chini ya Mstahiki Meya BONIFACE JACOB imefanikiwa kutengeneza madawati bora na imara zaidi ambayo yanazidi kuwasili ktk manispaa hiyo toka kwa wazabuni waliopewa tenda hiyo na muda si mrefu sana yataanza kuwasili ktk shule zetu zote zilizoko ndani ya manispaa ya kinondoni..
Na hakika tatizo LA madawati ktk shule zetu ndani ya manispaa ya kinondoni litakuwa limekwisha na kuwa historia. Hivyo msiwe na hofu wala mashaka linashughulikiwa ipasavyo.
Lakini pia tulipofika ktk shule ya MSAKUZI tulijionea mambo yafuatayo:
Ubovu wa choo cha shule ambacho kinanyufa nyingi ambacho kinahatarisha usalama wa wanafunzi wa shule hiyo kwa kujengwa chini ya kiwango hivyo kuweza kudondoka muda wowote. Pamoja na ubovu wa baadhi ya madarasa nayo kujengwa chini ya kiwango na kusababisha nyufa kubwa na madarasa hayo kuanza kumomonyoka. Huku Mwalimu mkuu na walimu wa shule hiyo kukosa ofisi na kufanyia kazi zao chini ya miti.
Nae Diwani Kolimba akamueleza Mwalimu mkuu wa shule hiyo kuwa kwanza atamfuatilia mkandarasi aliyejenga choo hicho pamoja na madarasa hayo ili kujua ni kwanini alijenga chini ya kiwango pia amelichukua na kulipeleka sehemu husika kwaajili ya utekelezaji.
Kuhusu walimu pamoja na mkuu wa shule hiyo kutokuwa na ofisi na kufanyia kazi zao chini ya miti, Diwani amesema swala hilo amelichukua na atalifanyia kazi kwa kushirikiana na wananchi wake, wadau wa elimu pamoja na mhe. Mbunge ili kuhakikisha Kata ya Kwembe inapata elimu bora kwa faida ya watoto wetu na kizazi kijacho ili kujenga taifa bora na imara.
Mwisho, mhe Diwani Kolimba aliwashukuru na kuwapongeza walimu hao kwa uvumilivu mkuu na upendo dhidi ya wanafunzi hao pamoja na changamoto zote zilizoko bado wameonesha kusonga mbele na kutimiza wajibu wao wa kuandaa kizazi kilichoelimika ambao wengi wao wameonesha kutaka kuwa viongozi wa kesho wa taifa..kama alivyo yeye Diwani wa Kata yao.

IMETOLEWA TAREHE 27/07/2016. NA OFISI YA MBUNGE JIMBO LA KIBAMBA.

No comments: