Kuanzia leo
Oktoba 8 mpaka 14 vijana bila kujali itikadi tunapaswa kuungana kote nchini
kuadhimisha wiki ya taifa ya vijana. Hata hivyo, toka wiki hii ilipoanzishwa na
Serikali mwaka 2003 imekuwa ikiadhimishwa bila mwitikio wa kiasi cha kutosha
katika ngazi mbalimbali isipokuwa katika maeneo ambayo wiki hii imekuwa ikiadhimishwa
kitaifa kwa kufanya maonyesho ya namna mbalimbali. Hivyo, nia ya taarifa hii ni
kuhimiza vijana, serikali na wadau mbalimbali ili maadhimisho ya mwaka huu yawe
na hamasa na maana zaidi kwa maisha ya vijana wa Tanzania na Taifa kwa ujumla.
Aidha,
maadhimisho ya kila mwaka ya wiki ya vijana yamekuwa yakichanganywa pamoja na
kilele cha mbio za Mwenge na Maadhimisho ya siku ya Mwalimu Nyerere kitaifa.
Matokeo yake wiki ya vijana imekuwa ikifunikwa na shamrashamra za mbio za
Mwenge na hatimaye kupoteza malengo ya msingi ya kushughulikia masuala
yanayowagusa vijana moja kwa moja.
Pia zaidi ya
maadhimisho yanafanyika kitaifa Shinyanga ni vyema mkazo ukawekwa katika
kufanya maadhimisho katika ngazi mbalimbali hususani wilayani. Hivyo maafisa
maendeleo wa vijana wa wilaya walau mwaka huu wajitokeze kutembelea vikundi vya
vijana, kuratibu matukio ya asasi za vijana na kuhamasisha mijadala ya vijana
kuhusu mustakabali wao na taifa kwa ujumla.
Natoa mwito
kwa vijana nchini kushiriki kikamilifu katika maadhimisho ya wiki ya taifa ya
vijana ya mwaka huu iliyoanza Oktoba 8
ambayo kilele chake kitafikia Oktoba 14. Kila kijana wa Tanzania afanye walau
kitu kimoja katika wiki hii kama sehemu ya maadhimisho ya wiki ya jamii-kama ni
kusaidia wasiojiweza, kufanya usafi wa mazingira, kufanya majadiliano kuhusu
mustakabali wa vijana na taifa, kuonana na viongozi kuzungumza nao kuhusu
maendeleo katika maeneo yao kuhusu masuala ya elimu, ajira, afya, ukuzaji wa
vipaji vya vijana, michezo, ushiriki wa vijana katika uongozi na mengineyo.
Wiki hii ni
muhimu kwa sababu kwa upande mmoja, vijana ndio
kundi linaloathirika zaidi na mabadiliko ya kisiasa, kiuchumi na kijamii
yanayojiri nchini kwetu na duniani kwa ujumla. Kwa upande mwingine vijana ndio
chachu ya mabadiliko katika taifa lolote duniani kutokana na nguvu, ubunifu, na
uwingi wetu.
NB: Maelezo haya kwa sehemu kubwa yalikuwa sehemu ya
Taarifa kwa Umma niliyoitoa tarehe 5 Oktoba, nayasambaza leo kuwakumbusha kwa
ajili ya hatua kila mmoja kwa nafsi na nafasi yake.
Maslahi ya umma kwanza.
1 comment:
je Hii ni kweli, watoto wa vigogo waliopita UVCCM ngazi ya taifa ni DICKSON MEMBE, FREDY LOWASA, RIDHIWANI KIKWETE, ASHURA HUSSEN MWINYI, BENY SAMWEL SITA, DEBORA MWANDOSYA, IREN PINDA, FELSTER NDUGAI, CHRISTOFER NDEJEMBI, SHARIFER BILALY, HAWA KIGODA, JUDITH MUKAMA NA JALOME MSEKWA.Kama ni kweli basi Nchi hii imekwisha. Inatia hasira, wacha watoto wa maskin tupambane kupitia mlango mwingine "CHADEMA" ili kute tea maskin wenzetu, wazaz na wadogo Zetu! Vita Hii Inaanza Sasa!
Post a Comment