Monday, March 25, 2013

Picha za Uzinduzi wa Daraja la Suka-Golani!

















Tujikumbushe harakati na jitihada mbalimbali ambazo zilifanywa mpaka kufikia hatua ya sasa kuhakikisha upatikanaji wa huduma bora ya miundombinu ya barabara ya Suka-Golani hapa:

1 May, 2012  Daraja Golani-Suca na Barabara Mburahati-Mabibo

Mkandarasi aliyepewa zabuni ya ujenzi wa daraja la Golani-Suka anapaswa kuanza mapema ujenzi wa daraja hilo muhimu linalounganisha kata za Kimara na Saranga ili kupunguza kero kwa wananchi hasa wakati wa mvua.

Mwezi huu wa Aprili nimefuatilia kuhusu hatma ya daraja hilo na hatimaye mkataba wa ujenzi wa daraja husika umesainiwa kati ya Manispaa ya Kinondoni na Mkandarasi Kika Co. Ltd kwa gharama za shilingi milioni 447.

Hata hivyo, ujenzi wa daraja husika haujaanza suala ambalo linahitaji Manispaa ya Kinondoni kumsimamia kwa karibu mkandarasi husika ili ujenzi uanze kwa haraka kwa kuwa mchakato wa zabuni ulianza kuanzia mwanzoni mwa mwaka 2012.

Izingatiwe kwamba kutokuwepo kwa daraja katika eneo hilo mwaka miaka mingi kumefanya mawasiliano katikati maeneo hayo kuwa magumu nyakati za mvua na kusababisha madhara ya kibinadamu na mali wananchi wanapovuka mto katika eneo hilo wakati wa mafuriko.

Baada ya kuwawakilisha wananchi kutaka ujenzi wa daraja hilo lilingizwa kwenye bajeti ya Manispaa ya Kinondoni kwa mwaka wa fedha 2011/2012 hata hivyo miezi ikiwa imebaki takribani miwili kabla ya mwisho wa bajeti husika ujenzi wa daraja hilo ulikuwa haujaanza bado.

Hatua kama hiyo inahitajika pia kwa barabara ya Mburahati mpaka Mabibo NIT ambayo inapaswa kuanza kujengwa kwa kiwango cha lami ikiwa imetengewa kiasi cha shilingi milioni 504 kwa ajili ya kuchangia katika kupunguza msongamano wa magari katika barabara ya Morogoro . 

Tathmini ya utekelezaji wa bajeti inaonyesha kwamba kasi ya utekelezaji wa miradi ya maendeleo ni ndogo pengo ambalo linapaswa kuzibwa kwa kusimamia kwa karibu miradi inayopaswa kuanza katika muhula uliobaki wa mwaka wa fedha 2011/2012.

Rejea: http://mnyika.blogspot.com/2012/05/daraja-golani-suca-na-barabara.html 


January 27, 2012 Kuhusu Msongamano wa Magari DSM na Ziara Kwembe: http://mnyika.blogspot.com/2012/01/kuhusu-msongamano-wa-magari-dsm-na.html

2 comments:

DENIS MASOLA said...

MHESHIMIWA MNYIKA MBUNGE WA JIMBO LA UBUNGO NAKUTAKIA AFYA NJEMA NA MAISHA MAREFU MUNGU AKUBALIKI SANA, KWANZA NAKUPA PONGEZI KUBWA SANA KWA KUISIMAMIA SERIKALI VIZURI NA KUDAI MASLAI YA WANAUBUNGO NA UJASILI ULIONAO NINAFURAHI SANA KWA HILO KAKA,MHESHIMIWA NAOMBA UNISAIDIE KITU KIMOJA MIMI NI MFANYAKAZI, LAKINI NAVYOIPENDA CHADEMA NATAMANI NIJE NAMI KUWA MWANAHARAKATI WA CHADEMA, NAKIPENDA SANA HIKI CHAMA,ELIMU YANGU NI DIPLOMA IN COMPUTING AND INFORMATION TECHNOLOGY(IT) BY DENIS MASOLA.

Anonymous said...

HIVI BWANA MNYIKA KWENYE ELIMU YAKO YA SEKONDARI HUJAJIFUNZA LOLOTE KUHUSU GLOBAL WARMING AND ANTHROPOGENIC ENVIMENTAL DEGRADATION JE UTAKAPOIKOMBOA TANZANIA KWA KILE UNACHODAI NI UKOLONI WA CCM UTAFANYAJE MAENEO YA MAKAME KAMA SAME NA DODOMA MVUA ZINYESHE MARA KWA MARA ILI KILA KIJIJI KIPATE MAJI SAFI NA SALAMA UTACHUKUA HATUA ZIPI MIKOA YA DODOMA SHINYANGA NA SINGIDA IWE NA MISITU MIZITO ILI KUVUTA MAWINGU YA MVUA ILI MVUA ZA AWALI ZIRUDI,NI VIPI UTAZUIA GLOBAL WARMING ILI THELUJI YA MLIMA KILIMANJARO IREJEE,UNAJUA UKIELEZEA VIZURI UTAJENGA CV YA KUPEWA NCHI MIKAKATI UNAJIDAI UNAWEZA WA MAPROFESA NI IPI SIKU HIZI UONGO SIO DHAMBI UKIWA UMEZUNGUKWA NA MAZUZU HEBU ELEZA MUNGEWEZAJE KUTUPATIA KATIBA MPYA SIKU MIA MOJA KINACHOTAKIWA NI KUONYESHA YALE MAENEO AMBAYO MUNA WABUNGE KUONDOA KERO ZA WAPIGA KURA ILI MAJIMBO MENGINE YAONE WIVU NASHANGAA WANAFANYA CCM MUNADAI NI JIMBO LAKO THIHIRISHA NI CHADEMA WALIOFANYA KUWA MKWELI TU KAMA MREMA ,CHEYO NA MBATIA MSEMA KWELI MPENZI WA MUNGU SINA UHAKIKA MUNGU NINAYEMWAMINI ANASIKILIZA WAONGO ,WAMBEA,WADAKU ,WAZUSHI,MAKAHABA,WASIO NA SHUKRANI KAMA MUNAHITAJI BARAKA ZAKE BADILIKENI SIWAONI MUKISHIRIKI KWENYE MAZISHI MBALIMBALI KAMA VILE NYINYI MTAPAA ASIYEKUJALI KWENYE SHIDA SINA UHAKIKA AKIPATA NEEMA ATAKUKUMBUKA SI RAHISI UWAPO MASIKINI UWE SHETANI ,ILA UKIWA TAJIRI NDIO UWE WA MUNGU MAADILI YENU KWENYE VITEDO NI SIFURI KABISA MUNAAHIDI KUONYESHA MAADILI MAZURI MUKIPATA NCHI MAZUZU WANAWEZA KUKOSEA MUKAPEWA ILA RASILIMALIWATU NI SIFURI KABISA