Monday, February 17, 2014

Mrejesho wa leo Februari 17: Jitihada za kuboresha barabara jimboni Ubungo na mengineyo

1. Barabara ya Goba-Mbezi Louis nawaomba wananchi wenzangu mfuatilie matengenezo yaliyoanza na kutoa mrejesho; lami kidogo nayo itaanza. Tuungane kupendekeza nyongeza bajeti hii

2. Barabara ya Malambamawili-Msigani naombeni tathmini ya matengenezo yaliyofanyika; ujenzi wa lami utaanzia kipande cha Kinyerezi-Kifuru. Kwa hii sasa ni hatua.

3. Barabara ya Bonyokwa-Mavurunza Kimara mwisho; nimewasiliana na Manispaa ya Kinondoni kukumbusha utekelezaji wa ahadi ya matengenezo. Majibu kesho.

4. Barabara ya Matete-Jeshini-Golani haikutengewa fedha KMC, nimewatumia ujumbe TANROADS wakishughilikia Msewe wasogee

5. Barabara ya Mavurunza-Golani-Msewe-Matete hali ya barabara ni tete. Nimewasiliana na diwani Pascal Manota na kumtumia posho ya leo kuweka mafuta grader. Ikiwa unatumia barabara za Mavurunza-Golani-Matete wasiliana na Diwani 0713792966 utuunge mkono sasa; mamlaka zingine nazo tunazifuatilia

Tayari nimefika Dodoma, nimekabidhiwa makabrasha; kesho Bunge Maalum. Ingia http://www.katiba.go.tz soma nyaraka tujadiliane tupate katiba bora

Kwa namna ya kipekee pia, nawakatika kila la kheri wahariri walioteuliwa na gazeti la MWANANCHI (Ndugu Sanga na Ndugu Miruko). Naamini mtazingatia ADUUU na kulinda uhuru na uwajibikaji wa uhariri.

No comments: