Ndugu IGP MwemaLeo vijana wako msafara wa magari takribani ishirini wamefanya patrol Tarime na kukamata zaidi ya vijana hamsini kwa sababu za kisiasa. Na wengine wamekamata mpaka pikipiki na mali zao nyingine. Vijana wako, wanaolipwa mishahara kwa kodi zetu watanzania, wanakubali kutumika kisiasa kwa kuwa tu wanapata chakula toka kwa tajiri anayeitwa Zakaria ambaye pia anagombea udiwani kwa CCM Tarime. Naandikia ujumbe huu wa wazi uchukue hatua za haraka. Nami siku chache zijazo naelekea huko huko Tarime. Mtukamate wote mujaze mahabusu na magereza yote huko. Uchaguzi utakapokishwa, dhana nzima ya polisi jamii ambayo umekuwa ukihubiri itakuwa umepotea.
Wako katika ujenzi wa Taifa
John Mnyika
Mkurugenzi wa Vijana-Taifa
0754694553
No comments:
Post a Comment