Wednesday, November 2, 2011

Kumbukumbu ya Loyola-Maslahi ya Umma KWANZA

Kwangu tarehe 2 Novemba itaendelea siku ya kuwakumbuka kwa mchango wenu wa hali na mali 2010 wakati wa kutafuta, kupiga na hatimaye kulinda kura vituoni na hatimaye kukesha Loyola.

Kwa mara ya kwanza nilitokwa machozi hadharani sio kwa furaha ya ushindi bali kwa kuguswa na imani mliyoonyesha kwangu.

Niliwaeleza sina cha kuwalipa isipokuwa kuwatumikia kwa akili, mwili, moyo na roho yangu yote.

Novemba 5 nitakuwa na mkutano kata ya Ubungo kuwaeleza kazi tulizofanya 2011 na kupata tathmini, mawazo na maoni yenu kuhusu mwelekeo kwa 2012 na kuendelea. Maslahi ya Umma Kwanza

1 comment:

Eucalyptos said...

Mbunge wangu Mnyika,
Ninakushukuru kwa kujali kwako na kufanya kazi kwako kwa maslahi ya umma.

Sipo jimboni na natumai pia wapo wengi ambao hawapo; ninaomba utuarifu yatokanayo kwani hatukuweza kuhudhuria na hatupo.

Kila la kheri na Mungu akujalie pamoja nasi ili tuyafikie malengo yetu ya maendeleo.

Keep it up Mnyika!