Wednesday, November 23, 2011

Waziri wa Ardhi, Nyumba na Makazi, Prof.Anna Tibaijuka katika Kata ya Sinza kukagua uuzwaji maeneo ya wazi


Waziri wa Ardhi, Nyumba na Makazi Prof. Anna Tibaijuka akiongea na mkazi wa Sinza Ndahani Yohana ambaye amenunua eneo la wazi kwa utapeli kwa shilingi milioni 500 wiki mbili zilizopita, ambapo ramani halisi inaonyesha eneo hilo ni la wazi.

Waziri wa Ardhi Nyumba na Makazi Prof. Anna Tibaijuka akihakiki na kuonyesha kupitia ramani maeneo ya wazi yaliyouzwa na kuvamiwa katika Kata ya Sinza eneo la Sinza E

Waziri wa Ardhi, Nyumba na Makazi Prof. Anna Tibaijuka wa pili kutoka kulia akiangalia ramani halisi inayoonyesha maeneo ya wazi wakati alipokagua maeneo ya wazi yaliyovamiwa na wananchi maeneo ya Sinza E wilaya ya Kinondoni, ambapo pia alikuwa akikagua mabango yaliyowekwa kwa ajili ya kuwataarifu wananchi na kuwaelimisha maeneo ambayo ramani inaonyesha yako wazi kwa ajili ya mipango ya maendeleo ya Serikali.

Diwani wa Kata ya Sinza, Renatus Pamba akimwonyesha Waziri wa Ardhi, Nyumba na Makazi, Prof. Anna Tibaijuka maeneo ya wazi yaliyovamiwa na wananchi katika maeneo ya Sinza E

Nashukuru sana blogu ya http://www.hakingowi.com/ kwa kurusha habari hii!

4 comments:

jacky said...

Duuu! Tugepata mawaziri kama hawa 10,nchi ingekuwa tambarare.

renny said...

Miji inakua kwa kasi sana, wakati watendaji wa wizara wamelala na wenye meno wanashindwa kufanya maamuzi, maeneo mengi kwa sasa yamevamiwa na mengine yamebadilishwa matumizi ambayo yanakinzana na matumizi yaliopo (incompatible change of use). Nionavyo mimi suala la ardhi linazidi kuwa la kisiasa zaidi na hili linatufanya tushindwe kuwa hata na jiji moja tu la mfano. Napenda kushauri, wizara ipeleke wataalamu katika kila ofisi za kata ili waweze kusimamia ujenzi holela, vinginevyo nyumba zitaendelea kuota kama uyoga. Kutoa elimu ya kutosha kwa wananchi katika masula yanayohusu ardhi ili kupunguza utapeli wa ardhi. Miaka hamsini ya uhuru hatuna hata mji mmoja uliopangika?

Kheri said...

Mi siielewi hii style ya huyu Mama, Hivi kwa kasi hii ya yeye kutaka awe field atakamilisha zoezi kweli. Nijuavyo kuna mikoa 20, wilaya zaidi ya 100 na ana miaka mitatu tu iliyobaki kutatua kero hii na nyingine zilizobaki. Namshauri atengeneze mfumo na ausimamie ufanye kazi kotekote. Lini atafika huku Kihesa iringa? au ndo Upanga, Palm Beach, Sinza, Tabata, Oysterbay..... na sijui lini atafika Mwananyamala. Anyway labda anawavutia kasi kama paka anavyomvizia panya kama hamtaki vile!

Anonymous said...

Concern zako ni nzuri sana kuwa Mama Profesa Anna Kajumulo Tibaijuka hawezi kutimiza ndoto za kuwa na mji au miji bora akiwa mwenyewe. Hata hivyo kuna SIRI moja kubwa iliyo wazi. Siri hiyo ni kuwa hii vita anapigana yeye mwenyewe. Siamini kama ana support kutoka Serikali yake wala watendaji wa Wizara na Manispaa zetu zote tatu. Na hii insabababishwa na baadhi ya viongozo waliopo na waliopita kuhusika sana katika kuuza au kujiuzia maeneo ya wazi. Wewe jaribu kufuatilia kwa mfano maeneo yote yanayoitwa ya Sisiem. Utakuta maeneo mengi yalikuwa ni maeneo ya wazi. Sisiemi walijigawia kabla ya kuingia kwa vyama vingi ili wawe na vyanzo vya mapato. Na hii linasemekana kuwa lilikuwa ni agizo toka ngazi za juu za Chama. Ukitaka kwenda mbele zaidi waulize watendaji ambao ni Manispaa zetu. Watakueleza kuwa wanashindwa kusimamia miji kwakuwa ukitaka kufanya hivyo utagusa maslahi ya wakubwa fulani na si ajabu kukuta ukipoteza kazi au kuhamishiwa mbali ambapo utasahaulika. Mama Tibaijuka analitambua hilo, ila anajaribu kuonyesha mfano angalu kwa sehemu ndogo ndani ya kipindi chake cha uongozi ili kuonyesha kuwa inawezekana kupambana na wavamizi wa maeneo ya wazi japo wana support ya wakubwa. Yeye kama Waziri hakuna mtu wa kumzuia isipokuwa Rais tu. Hawa watendaji wengine, juu yao kuna wakubwa wengi, hawawezi wala kuthubutu kufanya hivyo.Ila kama wakiona wanapata support toka ngzi za juu ambazo ni Rais na Baraza lake la Mawaziri naamini wanaweza kusimamia miji yetu. Watakachohitaji ni kuongezewa watendaji wachache kidogo kama vile building inspectors na land rangers. Kwa maoni yangu, tusibeze jitihada hizi za Mama Ana Tibaijuka, bali wananchi wampe support ikiwezekana kufanya maandamano ya kumuunga mkono ili Serikali ijue kuwa wananchi wanakerwa na uvamizi wa maeneo ya wazi na ujengaji holela.