Tuesday, January 31, 2012

Hatimaye mkataba wa vijana wa Afrika waletwa bungeni kuridhiwa

Kwa Vijana wenzangu kwa nafasi na wote wenye nafsi za ujana, leo ule mkataba wetu wa Afrika (African Youth Charter) hatimaye unaingia bungeni kuridhiwa. Ni matokeo ya harakati zetu za miaka mingi kabla na hata baada ya Rais Kikwete kuusaini Gambia mwaka 2006 lakini ukaishia makabatini. Baada ya kunituma bungeni kuwatumikia mkataba huu ni kati ya mambo niliyohoji mara kwa mara kutaka uletwe bungeni kuridhiwa ili utekelezaji wake uweze kuanza.

Nawashukuru wote tuliounganisha nguvu kwenye harakati za vijana kwa nyakati mbalimbali kuanzia NYF, TYVA, YUNA, TSNP, UDSM, BAVICHA, asasi zingine na mwisho lakini kwa umuhimu mkubwa vijana wote tuliokesha pamoja kulinda kura Loyola.

Kwa kurejea nyuma katika historia, nawaletea moja ya ujumbe nilioandika kwenu na kwa vijana wa Afrika mwaka 2008: http://mnyika.blogspot.com/2008/10/vijana-tufikiri-na-kuungana-kukomboa.html Kila kizazi lazima kiitambue dira na dhima yake; ama kisaliti au kitimize. Tuendelee kuwajibika; kwa pamoja tunaweza.

John Mnyika
Bungeni, Dodoma-01/02/2012

4 comments:

Anonymous said...

ni jambo la kheri kwa manufaa ya taifa la sasa na vizazi vijavyo, hongereni nyoote mlioshiriki na mnaoendelea kutuwakilisha kwa kuzingatia maslahi yetu na tz kwa ujumla...vijana taifa la leo linalojengwa leo na si kesho!

N.A, Mgonja

Pigangoma A. D said...

Ni mwanzo mzuri kwa maendeleo ya vijana kwani hata sera ya Taifa ya Maendeleo ya Vijana Tanzania imeshindikana kutekelezeka hali inayopelekea kufikia kilele cha miaka mitano mwaka huu bila hata changamoto na matamko yake kutekelezwa na wanaojiita chama tawala.

Hongereni wabunge wetu wa CHADEMA kwa kuonesha njia na kuwafundisha kazi hao vilaza wa CCM!

Pigangoma A. D said...

Mh. J. J. Mnyika!

Nimetafuta nakala ya mkataba wa vijana Afrika kwenye website lakini nimekosa. Naomba kwa kuwa najua unayo nakala hiyo please nisaidie!

Nitumie kwa: aldapig@gmail.com

Anonymous said...

go Jembe go mnyika tuko nyuma yako kamanda wetu,pigana kwa hoja wasipokusikiliza nguvu ya umma itaamua