Thursday, January 5, 2012

Kuhusu kauli za Waziri Magufuli

Kwa wote mliotaka maoni yangu juu kuhusu kauli za Waziri Magufuli vyombo vya habari kuhusu mbunge wa Ubungo na Jimbo letu. Katika siku hizi tatu sina muda wa malumbano, niko katikati ya kazi ya kuwatumikia wananchi jimboni na kutekeleza wajibu mwingine wa kitaifa. Wananchi na wadau wengine mnaweza kumwambia ukweli mnaoufahamu kuhusu aliyoyasema mkipenda, kwa kuwa matendo yanazungumza zaidi ya maneno. Mjadala huu na mingine ni muhimu pia kubadilisha mifumo na kurejesha utamaduni wa uwajibikaji katika taifa letu. 

Mambo ambayo amesema kwamba siyashughulikii ukweli ni kwamba nilishachukua hatua kwa nyakati mbalimbali kwenye mwaka 2011 ndani ya bunge, kwenye halmashauri na pia nje ya bunge, na matokeo yameanza kuonekana. Baadhi ya hatua hizo nilimhoji yeye mwenyewe au mamlaka za Wizara yake kama sehemu ya kutimiza wajibu wa kibunge wa kuwakilisha wananchi, kutunga sheria na kuisimamia serikali. 

Kwa bahati mbaya amekuwa msahaulifu hata wa kauli zake mwenyewe kuhusu masuala niliyoyaibua, amelewa sifa kwa kiwango cha kusema maneno yasiyokuwa ya kweli, imani juu yake imempa upofu wa kupindisha mambo mbalimbali na kugeuzia watu wengine mambo ambayo yeye mwenyewe au wenzake katika serikali wamefanya uzembe wa kutochukua hatua kwa wakati. Kwa bahati nzuri, ukweli una sifa moja, huwa unadumu milele; nitamjibu hoja kwa hoja nikipata wasaa kwa sasa naendelea na utumishi, maslahi ya UMMA kwanza.

5 comments:

Anonymous said...

Kaka JJ,
Kwa roho safi na pasipo kukuficha; katika suala la nauli ya kivuko, wewe kuungana na vipofu wengine ulikula kasa. Acha kabisa kubaki upande wa upinzani kwa MAghufuli katika suala hili. Tayari walio wengi tunakuona umepelekeshwa katika kuunga mkono upuuzi wa wabunge wa Dar. Sasa kama hutaki ku-take advantage ya hii "benefit of doubt" basi ingia ulingoni na upambane na Maghufuli. Utakuwa unamkimbiza aliyekuibia nguo bafuni......Kila la heri

Anonymous said...

John Mnyika kamamtajifanya kufuatilia kauli za Magufuli na kuacha utendaji wenu wa kila siku wa kuwatumikia wananchi, ntakuingiza na wewe kwenye kundi la wanasiasa vipofu wanaosubiri fulani aseme nini ndio waanze kupiga domo.mimi nadhani waelewesheni wanachi wenu ukweli ulivyo.na kusema Magufuri amelewa sifa inamaanisha unakubali utendaji wake na ni mtendaje, ikumbukwe kua ni magufuli huyu huyu ambae rais alimwambia alegeze sheria kidogo sasa naona na nyie mnataka kumwambia acha kabisa kufanya kazi...tunapenda watu wawajibikiaji bila kuangalia itikadi za kisiasa...kila la kheri

Anonymous said...

Kweli mliocomment hapo juu nafikiri nanyie mmeleweshwa sifa na magufuli,kinachotakiwa kiangaliwe kwa ukaribu ni je mapato yote ya ferry ya kigamboni yanawasilishwa ndipo tuseme kinajiendesha kwa hasara.
Bila kuficha maneno hata kulipia vivuko ni kumkandamiza mlalahoi, kwani ni sawa na kulipia barabara hivi ni wananchi wa kigamboni tu wanaotakiwa kulipia barabara ya mkato (ferry) Kenya somewhere Mombasa kivuko kupanda ni bure ni magari tu yanayolipia kwa kuwa yanacover nafasi kubwa.

Anonymous said...

mimi ni mpenzi sana wa mafanikio yako Mnyika.lakini katika hili umeteleza tena omba radhi wananchi wako .kumbuka kuna barabara nyingi ubungo hazipitiki tangu mvua imenyesha na matatizo kibao.nakushauri kuanza upya si ujinga OMBA RADHI WANAUBUNGO

Anonymous said...

Mimi sio sababu ya mbunge kuomba radhi, kazi yake ni kuisimamia serikali na hapa amemsimia Magufuli. Labda ulitoa maoni haya kabla ya kusoma tamko lake, mimi nimesoma na kuona alichukua hatua kuhusu hizi barabara. Nimefurahi kwamba alipendekeza barabara zipandishwe hadhi na kuongezewa fedha. Sasa kazi kwa Magufuli kwa kuwa alidai hajapata mapendekezo, ni vizuri Waziri akatekeleza mapendekezo yote kwa maendeleo ya jimbo letu ili tuamini uchapakazi wake.