Leo nimeendelea na kazi za kibunge jimboni katika kata ya Kwembe nimefanya ziara na kukutana na wananchi, wameniuliza maswali kuhusu maji, barabara ya kwenda Mpiji Magohe, Luguruni Satellite town, mgogoro wa ardhi katika eneo la Msakuzi na uharibifu wa daraja katika mto Mdidimua/Kibwegere (Mji Mpya). Nimewajibu hatua ambazo nimechukua kwa kila jambo.
Pia nimekabidhi Jengo la Kituo cha Afya na Mama na Mtoto Kata ya Kwembe Jimboni Ubungo, tulichojenga kwa fedha za Mfuko wa Kuchochea Maendeleo ya Jimbo (CDCF). Habari zaidi zitafuata; Maslahi ya Umma KWANZA.
1 comment:
Mh:
Sisi wakazi wa Mtaa wa Bwaloni, kata ya Msigani tunakuhitaji. Maji na barabara yamekuwa matatizo makubwa ambayo hadi hivi leo hatujapatiwa majibu yanayoridhisha kutoka kwa wahusika hasa viongozi wa Serikali ya Mtaa (Mbezi) Temboni!
Post a Comment