Monday, November 26, 2012

Shime tujitokeze kutoa maoni yetu kupata Katiba Mpya!


Rejeeni mikutano ya hadhara na vikao mbalimbali ndani ya jimbo letu la Ubungo katika kata mbalimbali ambapo nilihamasisha elimu juu ya haja na hoja za mabadiliko ya katiba.

Sasa zamu ya jimbo letu imefika kutoa maoni.

Toa sasa na himiza wananchi wenzako wengine nao washiriki kutoa maoni.

Endapo utakosa fursa ya kutoa maoni yako katika mikutano na Tume ya Katiba. Hakikisha unatoa bado maoni yako kwa njia hizi: Facebook hapa: http://www.facebook.com/pages/Tume-ya-Mabadiliko-ya-Katiba-Tanzania/323414977745643?fref=ts  au Ingia hapa ujaze maoni yako: http://www.katiba.go.tz/index.php/toa-maoni-yako/wanaoishi-ndani-ya-nchi au baruapepe: katiba@katiba.go.tz

Pia kwa watanzania wenzetu waliopo nje ya nchi, huu pia ni wakati wenu wa kutoa maoni kwa kupitia: Facebook hapa: http://www.katiba.go.tz/index.php/toa-maoni-yako/wanaoishi-nje-ya-nchi au Ingia hapa ujaze maoni yako: http://www.katiba.go.tz/index.php/toa-maoni-yako/wanaoishi-ndani-ya-nchi au baruapepe: katiba@katiba.go.tz



RATIBA YA MIKUTANO YA MAONI YA KATIBA JIMBO LA UBUNGO.
NA.

KATA

TAREHE

MAHALI
MUDA WA MKUTANO
KUANZA
KUMALIZA
1
KIMARA

27/11/2012
BAHAMA TRA
3:00 ASB
6:00 MCH
UBUNGO
S/MSINGI MSEWE
8:00 MCH
11: JIONI
2
KIBAMBA

28/11/2012
S/MSINGI KILUVYA
3:00 ASB
6:00 MCH
MBEZI
S/MSINGI MBEZI
8:00 MCH
11:00 JIONI
3

GOBA

02/12/2012
ZAHANATI YA GOBA
3:00 ASB
6:00 JIONI
4
KWEMBE

03/12/2012
KIBAMBA HOSPITAL
3:00 ASB
6:00 MCH
SINZA
UWANJA WA TP
8:00 MCH
11: JIONI
5

SARANGA

04/12/2012
STENDI YA BONYOKWA

8:00 MCH

11: JIONI
6

MSIGANI

05/12/2012
UWANJA WA TANESCO

3:00 ASB

6:00 JIONI
7

MANZESE

07/12/2012
UWANJA WA BAKHRESA

8:00 MCH

11: JIONI
8

MABIBO

10/12/2012
S/MSINGI MPAKANI

3:00 ASB

6:00 JIONI
9

MBURAHATI

11/12/2012
S/MSINGI MBURAHATI U/KIFA

3:00 ASB

6:00 JIONI
10
MAKUBURI

13/12/2012
U/NJIA PANDA MABIBO HOSTEL

3:00 ASB

6:00 MCH
MAKURUMLA
GOMBERO
8:00 MCH
11: JIONI

MUHIMU: naomba wananchi wakati mkituma/toa maoni yenu, mnitumie pia nakala kwa simu: 0715-37 95 42 au baruapepe: mbungeubungo@yahoo.com kwa kuratibu na kurahisisha shughuli za ufatiliaji kwani kwa mujibu wa sharia ya mabadiliko ya katiba ilivyo sasa wabunge ni wajumbe wa Bunge la Katiba hivyo napaswa kupata nakala ya maoni ya wananchi pia juu ya katiba mpya niweze kuwakilisha kwa hatua hiyo ikifika.

Pia, napaswa kupata maoni yao kuhusu mchakato wa kupata katiba mpya ili niyazingatie wakati natekeleza wajibu wa kuwakilisha wananchi, kutunga sheria na kusimamia tume na serikali kwa ujumla wake ili nchi ipate katiba mpya na bora kwa maendeleo ya wananchi.



Maslahi ya Umma Kwanza!

John Mnyika
Mbunge Jimbo la Ubungo

1 comment:

pipi said...

Asante sana Bw. Mnyika, tunaopenda mabadiliko lazima yaanzie kwenye sheria mama ambayo ni katiba!

Tutoa maoni yetu ipasavyo! asante tena!