Na Mwandishi Wetu,
Dodoma
Mbunge wa Ubungo
(Chadema)John Mnyika akihoji Kiti cha Spika juu ya serikali kushindwa kuleta
bungeni kauli ya serikali juu ya mkakati wa kukabiliana na uhaba wa mafuta
nchini Tanzania.
Uhaba wa mafuta
jana umewakimbiza kwenye kikao cha Bunge mjini Dodoma asubuhi, Waziri wa
Nishati na Madini, Profesa Sospeter Muhongo na naibu mawaziri wake George
Simbachawene na Steven Masele.
Waziri huyo na
naibu mawaziri wake hawakuwepo bungeni leo wakati Mbunge wa Ubungo (Chadema)
John Mnyika akiitaka serikali itoe sababu ya kutokuja bungeni leo kutoa tamko
la serikali jinsi inavyoshughulikia suala la uhaba wa mafuta nchini.
Spika wa Bunge Anne
Makinda alimlazimisha Waziri Mkuu Mizengo Pinda kusimama na kujibu hoja ya
Mnyika aliyemtaka Spika kulazimisha serikali ijibu hoja yake pamoja na mkakati
wa serikali wa kutatua uhaba wa mafuta nchini.Waziri Mkuu Mizengo Pinda
alilazimika kunyanyuka na kusema kwa ufupi kuwa serikali ilikuwa ikijiandaa na
kuja na hoja nzito ya kueleza umma mikakati kabambe ya kutatua uhaba wa mafuta
nchini.
No comments:
Post a Comment