Sunday, February 23, 2014

Pata nakala ya rasimu ya kanuni za Bunge Maalum la Katiba hapa, na shiriki mkutano wa mtandaoni leo tuijadili kutoa maoni na mapendekezo

Ratiba na utaratibu wa Bunge Maalum la Katiba haujatuwezesha kurejea kupata maoni ya mliotutuma au walau kuwekwa utaratibu wa Mwenyekiti wa Muda kuitisha mkutano wa kusikiliza umma/wadau (public/stakeholders hearing) hapa Dodoma.

Nilitoa pendekezo hili kwa Mwenyekiti wa Muda wa Bunge na kwa wadau; rejea: http://mnyika.blogspot.com/2014/02/kwanini-ni-muhimu-tushirikishe-wananchi.html na http://www.ippmedia.com/frontend/?l=64919

Hata hivyo, mjadala wa bungeni unaanza kesho na hatimaye kanuni kupitishwa kwa kile ambacho vyanzo vyangu vimenidokeza kuwa msimamo wa wenye madaraka ni kwamba “mamlaka ya kujitungia kanuni ni ya bunge maalum lenyewe, kutunga kanuni ni suala la ndani la wajumbe wenyewe”.

Kutokana na ukuu na upekee wa kanuni hizi katika uendeshaji wa Bunge Maalum, ni wazi kasoro katika kanuni zitaacha mianya ya maoni ya wananchi yaliyomo kwenye rasimu ya katiba kuchakachuliwa badala ya kuboreshwa. 

Aidha, yapo mambo katika rasimu ya kanuni yanayohusu haki, kinga na maslahi ya wajumbe wa Bunge Maalum ambayo katika mizania ya utawala bora ni vyema katika kuyatunga maoni na mapendekezo ya wadau wengine wa nje ya Bunge la Maalum yakatolewa.

Tarehe 20 Februari 2014 vyombo vya habari vilimnukuu Mwenyekiti wa Muda wa Bunge Pandu Kificho kwamba ameunda kamati ya muda ya kanuni ya kumshauri na kuahirisha vikao kutoa nafasi kwa kamati hiyo kufanya kazi na pia wajumbe kujisomea nakala ya rasimu za kanuni walizopewa.

Aidha, alitangaza kwamba mjadala wa rasimu ya kanuni hizo utaanza leo jumapili 23 Februari, 2014 na jumatatu tarehe 24 Februari 2014 na hatimaye kanuni kupitishwa. Katika mazingira hayo, njia ya haraka ya kuweza kuwasiliana na kupata maoni na mapendekezo ya wananchi na wadau ni kupitia Teknolojia ya Habari na Mawasiliano (TEHAMA) mathalani kupitia mitandao ya internet na simu za mkononi.

Hivyo, chukua hapa au popote kwingine nakala ya rasimu ya kanuni za Bunge maalum; soma, jadili na wenzako na fikisha maoni na mapendekezo kupitia TEHAMA kwa mjumbe anayekuwakilisha katika Bunge Maalum la katiba.

Kwa upande wa wananchi wa Jimbo la Ubungo na wengine mtakaopenda kushiriki pamoja nasi; nawakaribisha kwenye mkutano wa mtandaoni siku ya leo jumapili tarehe 23 Februari 2014. 

Mkutano huo wa mbunge na wananchi utaanza saa 6 kamili mchana mpaka saa 8 mchana kupitia mtandao wa http:mnyika.blogspot.com. Mkutano utaendelea saa 2 usiku mpaka saa 4 usiku kwa mliokuwa wakazi wa Ubungo mlio nje ya nchi na pia kwa watakaokosa nafasi ya kushiriki mkutano wa mchana. 

Jinsi ya kushiriki mkutano huo, pitia nakala ya rasimu iliyotolewa na uliza maswali au toa maoni na mapendekezo mara baada ya ujumbe huu. Nitapitia maoni na mapendekezo yenu nami nitachangia maoni na mapendekezo yangu wakati mkutano ukiendelea kupitia ukurasa huu. 

Natanguliza shukrani nikitarajia kupata maoni na mapendekezo yenu ya kuboresha rasimu ya kanuni tuweze kupata nyenzo sahihi ya kuboresha au kufanya mabadiliko katika rasimu ya katiba tupate katiba bora.

Wenu katika uwakilishi wa wananchi,

John Mnyika (Mb)

23 Februari 2014
Bungeni, Dodoma

Rasimu kanuni bunge maalum-nyingine

12 comments:

Anonymous said...

Mh, Mnyika. Kwanza nikushuru kwa kutupa fursa hii ya kupata nakala ya rasimu ya kanuni. Nashangaa zilifanywa kuwa siri, haziko kwenye tovuti ya Bunge, wala ya Baraza la wawakilishi, wala ya Wizara ya katiba wala ya yeyote nyingine.

Nikizisoma nitachangia zaidi. Naomba uongeze muda wa mkutano mpaka kesho au kesho kutwa.

Lakini naunga mkono mapendekezo ambayo uliyaeleza jana kwenye gazeti la Nipashe; ni kweli Mwenyekiti wa Bunge maalum amepewa mamlaka makubwa sana. Vifungu vya 20,44, 80 na vyote vinavyosema maaamuzi ya mwenyekiti ni ya mwisho ni vya kidikteta. Akiwa mwenyekiti mtumumiwa wa ufisadi kama Chenge au yeyote anayepokea maagizo toka kwenye chama chake mustakabali wa katiba mpya utakuwa mashakani.

John Mnyika said...

Nashukuru, nasubiri mchango wako kwa kuwa sasa natangaza mkutano wa mtandaoni umefungiliwa rasmi.

Kikao cha kwanza cha leo kitaanza muda huu mpaka sasa nane mchana. Tutasitisha kikao mpaka awamu ya usiku ambapo tutaanza saa 1 mpaka 3 usiku.

Kama kuna maswali au maoni kuhusu rasimu ya Kanuni za Bunge Maalum na vikao vinavyoendelea hivi sasa niko tayari kuweza kujibu au kupokea.

JJ

Juma Mussa said...

Mimi nipo Mtwara, je naruhusiwa kushiriki mjadala huu? Kwanini sasa Bunge Maalum halionekani LIVE? Mnafanya nini muda huu?

Anonymous said...

Tunashukuru sana mh Mnyika kutushirikisha kwenye hili... Nasoma then ntarudi kwa maswali/maoni/ushauri, tuko pamoja sana

John Mnyika said...

Hata wa Mtwara una haki ya kujadili. Maoni yako unaweza kuyaandika hapa na pia ukamtumia mbunge au mjumbe. Bunge haliko Live kwa kuwa kikao kikao kimeahirisha mpaka ijumaa. Lakini jumatano kutakuwa na semina ya wajumbe kuelezwa kuhusu hizi kanuni lakini pia kuwasilishwa marekebisho yaliyofanywa na kamati ya muda ya kanuni iliyoundwa na Mwenyekiti wa Muda Kificho. Kamati hiyo kwa sasa inaendelea na vikao vyake leo na kesho. Mkitoa maoni maana yake ni kwamba wajumbe wa kamati hiyo wanapokuwa mapumzikoni kwa watakaopata wasaa wa kutembelea watapata maoni yenu. Lakini wasipopata, mimi nitayachukua na kuyatuma wakati nikapowasilisha mapendekezo ya mabadiliko baada ya maboresho yatayokuwa yamewasilishwa na Kamati. Kwa majibu hayo, natangaza kuahirisha mkutano huu wa mtandanoni mpaka saa 1 usiku tutakapokutana tena. Lakini kwa wote watakaotembelea kabla ya muda huu jisikieni huru kuacha maswali au maoni na mkutano utakapoanza tena tutayazingatia kwenye majadiliano. Aidha, kwa wale ambao watakuwa hawana mchango lakini wanapenda kuacha kumbukumbu kwamba walihudhuria mkutano kwa kutembelea mtandao huu waingie tu sehemu ya "comments" na kuacha ujumbe.

Ahsante kwa juhudi zako

Unknown said...

ivi ni kweli ile posho ya kila siku imeongezwa tayar hadi laki 5 au bado

John Mnyika said...

Evelius, madai kwamba posho imepandishwa na kuwa laki tano hayana ukweli. Ni uzushi wa kuendeleza mjadala wa posho hatimaye kuihamisha nchi kwenye mijadala muhimu ya sasa juu ya rasimu ya kanuni za Bunge na rasimu ya katiba. Hii ni mara ya tatu mara baada ya kuzinduliwa kwa rasimu ya katiba kwa kuibuliwa kwa mijadala inayohusu malipo ya wabunge inayohusisha kutolewa kwa taarifa zisizokuwa za kweli. Mjadala huu wa posho unakuzwa na athari zake ni kupoteza uhalali wa kimaadili wa wabunge katika kutumia mamlaka ya Bunge Maalum katika kutunga sharia kwa kuwa na taswira hasi mbele ya umma kwamba ni wenye ubinafsi na kujipendelea. Hata kama ingekuwa ni kweli, haiwezekani madai ya watu wachache ya nyongeza ya posho yakatumika kuhukumu wabunge wote wakati ambapo kazi ya kupandisha au kupunguza viwango hivyo vya posho si ya bunge bali ni ya Rais. Hivyo, ili Bunge libaki linaendelea na mjadala wake wa msingi kuhusu rasimu ya kanuni na rasimu, kama kuna shinikizo lolote juu ya posho basi lielekezwe kwa Rais kumshinikiza asiongeze na awianishe malipo ya watumishi wa umma kwa kuboresha maslahi ya watumishi wengine mfano walimu, waaguzi, polisi nk. Nashauri msiingie katika mtego wa kumezwa na mjadala wa posho, na kukosa kuhoji masuala ya msingi juu ya msimamo na njama za chama kimoja wa kuchakachua rasimu ya katiba kinyume na maoni ya wananchi. Udhaifu katika kanuni hizi ni mwanzo wa kuwepo mianya ya kuchachua rasimu kwa kutumia mamlaka makubwa aliyopewa mwenyekiti na utaratibu mbovu wa kujadili rasimu katika kamati za Bunge Maalum zinazokusudiwa kuundwa ambazo zitawafanya wajumbe kujadili vifungu vichache tu, badala ya kila mjumbe kujadili na kuboresha katiba kifungu kwa kifungu kuanzia katika hatua ya kamati.