Na
Veronica Romwald, Dar es Salaam
MBUNGE
wa Ubungo, John Mnyika (Chadema), amewaomba wapiga kura wake kumuombea kila
siku kutokana na madai kuwa amekuwa akiwindwa na watu wanaotishia uhai wake.
Mnyika
alitoa kauli hiyo juzi jioni katika eneo la Mbezi mjini Dar es Salaam, wakati
akihutubia mkutano wa hadhara.
“Nimekuwa
nikizungumza mambo mengi ninapokuwa bungeni Dodoma, hasa ninapowatetea wananchi
na wapiga kura wangu, lakini kuna watu hawafurahishwi kabisa…sasa wamefikia
hatua ya kunitishia maisha yangu.
“Wengi
mnakumbuka kwamba, Mwenyekiti wa Chama cha Madaktari Tanzania (MAT), Dk. Steven
Ulimboka, alitekwa na kupigwa na watu wasiojulikana na kisha kung’olewa meno,
baada ya tukio lile aliyekuwa akifuatia nilikuwa mimi, sasa sijui na mimi
wanataka kunifanyia hivyo au la,” alisema Mnyika.
Alisema
taarifa za yeye kutishiwa maisha zilianza kuvuja baada ya kumalizika kwa vikao
vya Bunge la Bajeti.
Alisema
kashfa ya Kampuni ya kufua umeme ya IPTL ilianza miaka ya tisini, baada ya
maridhiano kati ya Serikali ya Tanzania na Serikali ya Malaysia ili kuleta
mitambo ya kufua umeme nchini na kwamba, Rais Jakaya Kikwete anafahamu kiini
cha mzozo.
Alisema
IPTL imekuwa ikiitia hasara kubwa Serikali kwa kipindi kirefu, jambo ambalo
halina budi sasa kuchukuliwa hatua.
“Wenzetu
walikuwa na mtaji mdogo walipokuja kiasi ambacho hata Mtanzania anayefanya
biashara ndogo ndogo aliweza kuumiliki, lakini uliongezeka kutokana na sisi
kupandishiwa gharama za umeme kwa mujibu wa ushahidi wa Mahakama,” alisema.
Chanzo: Gazeti la Mtanzania (http://mtanzania.co.tz/?p=432)
No comments:
Post a Comment