Thursday, July 31, 2014

Kuhusu uongozi mpya wa wilaya ya CHADEMA Ubungo

Katibu wa CHADEMA Wilaya ya Ubungo, Goodluck Justine (wa kanza kushoto) akiongea na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam
UONGOZI mpya wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo wilaya ya kichama Ubungo unatarajiwa kujulikana Agosti 3, 2014 baada ya uchaguzi wa ngazi za chini katika wilaya hiyo kukamilika. 

Mbali na viongozi wa wilaya hiyo kujulikana siku hiyo, pia chama hicho kimeeleza kuwa, kimejiandaa vema kuwadhibiti mamluki wasijipenyeze katika uongozi huo. 

Hayo yalibainishwa na Katibu wa CHADEMA Wilaya ya Ubungo, Goodluck Justine, wakati akielezea mafanikio yaliyopatikana katika uchaguzi wa ngazi za msingi, matawi na kata. 

Nafasi zitakazowaniwa ni ya mwenyekiti, katibu, katibu mwenezi na mhazini na kwamba, kwa ngazi ya mabaraza ni vijana, wazee na wanawake. 

Justine alisema, ni fursa kwa kila mwanachama muadilifu wa CHADEMA Wilaya ya CHADEMA Ubungo kuwania nafasi anayoona ataimudu.

Aliwataka wagombea wote wa nafasi mbalimbali za uongozi katika jimbo hilo kuchukua fomu, kuanzia jana katika ofisi za jimbo ili kuwania nafasi hizo kwa ngazi ya kichama na mabaraza na siku ya kurudhisha fomu za wagombea ni Agosti Mosi, mwaka huu saa kumi alasiri.

Chanzo: www.wavuti.com (http://www.wavuti.com/2014/07/kuhusu-uongozi-mpya-wa-wilaya-ya.html)

No comments: