Tuesday, July 18, 2017

Uzinduzi wa albamu mbili za Baraka Mwaijande katika Kanisa la KKKT Usharika wa Temboni

Mkuu wa Jimbo, Mch.Mwangomola na Mchungaji wa Usharika wa Temboni, Mch.Lusekelo 

Baraka na Mkewe

Kwaya ya vijana
Nikiwa na Paul Clement


Jumapili Julai 16: Nilibahatika kualikwa kushiriki uzinduzi wa albamu mbili za kumsifu Mungu za kijana Baraka Mwaijande katika Kanisa la KKKT Usharika wa Temboni , Jimbo la Magharibi-Dayosisi ya Mashariki na Pwani [ndani ya Jimbo letu la Kibamba].

Nilifurahi na kufarijika sana kushuhudia  vijana wakitumia vipaji vyao kumsifu Mungu.

Baraka pia alinigusa kiupekee sana kwa ndoto yake ya kujenga kituo cha kuhudumia watoto yatima. Anafanya harambee kutekeleza azma hii. Tumuunge mkono. Kwa wenye kutamani kusikia kazi zake mbili za kumsifu Mungu au kumuunga mkono wawasiliane nae moja kwa moja: 0715-189 911

Paul Clement, alinigusa sana na wimbo wake “Amenifanyia Amani”! Hakika ana kipaji cha kipekee.

Nimefurahi pia kuwa na Baba Wachungaji, Mkuu wa Jimbo-Mch. Mwangomola, na Mkuu wa Usharika-Mch. Lusekelo na wachungaji wengine.


Naamini kila mmoja anaweza kuwa chachu ya kuiboresha jamii yetu kwa kutumia vipaji/talanta tulizopewa na MUNGU vyema.

John John Mnyika,
Mbunge wa Kibamba,
Julai 17, 2017

No comments: