Ndugu zangu wananchi,
Miongoni mwa ahadi zangu kwenu wakati nikiomba ridhaa ya uwakilishi katika chombo cha maamuzi ilikuwa ni kuhakikisha nachochea katika kukuza uwajibikiji na utawala wa kidemokrasia wakilishi.
Nitakuwa na mkutano wa hadhara wa kukusanya maoni yenu na kusikiliza ninyi wananchi ambao mmenipatia ridhaa niwawakilishe bungeni kabla ya kwenda kuanza vikao vya kibunge.
Nitazimiza ahadi na utashi wangu wa kuwa na mikutano ya kukusanya maoni ya wananchi kabla ya kwenda katika vikao vya bunge. Na zaidi kutoa tunu na thamani halisi ya uongozi wa uwakilishi kwa ninyi kunituma kuwa sauti yenu katika kufanya maamuzi!
Mkutano utakuwa J2 06/02/2011 Mahala:Manzese Bakhresa Muda:Kuanzia saa 10 mpaka 12 jioni.
Ikumbukwe Dodoma kazi zinaanza kuanzia tarehe 7, mkutano tarehe 8.
Tuhimizane kujitokeze kwa wingi. Tushirikiane.Inawezekana. Tufanye sasa!
Maslahi ya Umma Kwanza!!
Baruapepe kwa Ofisi ya Mbunge: mbungeubungo@yahoo.com
3 comments:
kaka wewe nikiongozi mtu wangu mungu akubariki na akusaidie ufike mbali tuko pamoja mkubwa
Mimi ni mwana-Ubungo, ingawa kwa sasa niko ughaibuni. NI vizuri sana unavyofanya, kukutana na wanaUbungo kabla ya kwenda Bungeni, maana tunataka mbunge awe kweli anawasilisha maoni na matakwa ya wananchi.
Ninapofuatilia mazungumzo na mijadala Bungeni, wakati mwingine napata picha kuwa baadhi ya wa-Bunge huwa wanawakilisha mambo yanayowajia kichwani. Huu ni ukweli, tukizingatia kilio cha muda mrefu cha wa-Tanzania wengi kuwa wabunge wao wakishachaguliwa, hawaonekani jimboni kwao.
Kwa hivi, nawaomba wana-Ubungo wenzangu mjitokeze kwa wingi kwenye mkutano huu. Tuko pamoja.
Kaka wewe ni mfano wa kuigwa kwa rika letu la ujana.Ufanyayo hayana hata chembe ya uchama bali utaifa.Nina imani MWENYEZI MUNGU atakusimamia na utatimiza yale yote mema unayofikiria kuwafanyia wana ubungo.Nakutakia kila la kheri.
Post a Comment