Saturday, November 12, 2011

Matumizi ya nguvu katika mgomo Chuo Kikuu DSM jana, 11.11.11

Poleni wanafunzi na jumuiya ya Chuo Kikuu cha DSM (UDSM), ni aibu kwamba mpaka mgomo na mabomu ndio serikali ichukue hatua kwa madai ya mikopo kucheleweshwa na kupewa kwa masharti yenye kuumiza watoto wa watanzania wa kawaida.Kila binadamu anayo haki ya kusoma!Ni moja ya haki ya msingi ktk haki za kibinadamu. Nasikitika siko pamoja nanyi jimboni Ubungo ktk wakati huu mgumu, nitachukua hatua za kibunge huku Dodoma-Bungeni.Kwa Pamoja Tunaweza!!








Shukrani Chanzo za Picha: Mtandao wa JamiiForums

Nimehuzunika sana baada ya kuona picha hizi na habari katika vyombo mbalimbali vya habari. Nipo pamoja nanyi!

10 comments:

Anonymous said...

na askari wetu ni tatizo kwani hawashirikishi akili zao wao wanafanya kazi kama roobot shem on them.

Anonymous said...

huu ni uvamizi wa jeshi la polisi kwa wanafunzi..aliwafata na kuwapiga katika eneo la chuo..ni uonevu wa kupindukia huu.hatuwezi kuukubali hata kidogo

Anonymous said...

Hivi kweli ni chama gani hiki ambacho hata hakijikoshi kwa wapiga kura wake hata kwa kutoa majibu yenye matumaini? Kama hilo halitoshi, serikali gani hii inayosema elimu ni kipaumbele wakati haiwagharimii watoto wa masikini? Hivi Kawambwa watoto wako wamesoma hivi? Au kwa kuwa unaishi kwa pesa za wazazi wetu? Hivi kweli serikali haina pesa za kuwapa wadogo zetu hata hela ya kujikimu? Mbona nyie mnaishi maisha ya kifahari? Ni lipi mmewatendea watanzania? Kawambwa, hivi una roho ngumu kiasi gani, huumii kuona tunavodhalilika na kuteseka hivi? Kama haijatosha, mnaleta askari wasio wazalendo watuue chuoni kwetu, kweeeeeli nyie ni binadamu? Ni nchi gani hii inayojiita eti ya kidemokrasia wakati haiwapi wananchi suluhu ya matatizo yao? Hivi kawambwa, hilo gari unalotembelea na kusema serikali haina hela huoni hata roho inakusuta? Hivi wewe hata unaamini kama mungu yupo? Hakika nakuambia kama umeshindwa kuwapa fadhila watoto hawa wa masikini, umekwisha hukumiwa na huna haki mbele ya mungu. Malipo ya anasa mnazoishi kwa pesa za wazazi wetu yapo hapa hapa duniani, hukumu ni mbinguni.Mbona wizara ya ujenzi mliipa mpaka hela zisizo na kazi, leo bodi eti inakosa hizo bilioni kadhaa tu kuwapa walau hela ya kula watoto hawa masikini? Kibaya zaidi, wale masikini wa kutupwa ndio ati bodi yako inasema hawana vigezo wana uwezo wa kulipa, na matajiri kama nyie ndio ati hawana uwezo. Hivi kawambwa, milioni 4 ya kusoma mwaka mmoja, sisi ambao wazazi wetu wanategemea kuponda kokoto watazitoa wapi? Hivi huwa mnapofikiria huwa mnafanya makusudiii? au mna upungufu? Yani kweli mnafurahi kuona watu wanakufa njaa chuoni kisa hela mnakula nyie? mtakua wakatili hivi mpaka lini? Hivi mnadhani serikali na nchi hii ni ya kwenu? Hakika nakwambia, lawama na laana zetu na za wazazi wetu na watanzania wote ziwe juu yako na chama chako chote. Mmetupa fundisho la maisha bora kwa kila mtanzania, hata aibu hamuoni. Mkichoka kutupiga risasi na mabomu katika ardhi yetu, tulipueni kabisa tufe ili tusidai kabisa, tufe kwa ajili ya kutetea maslahi ya watanzania wasio na sauti.

Anonymous said...

Jamani wabunge tusaidieni serikali itupe wote mikopo. Mbona mnatusikia mnakaa kimya. Ndio fadhila mnayotulipa? Kuweni wazalendo tuoneeni huruma masikini sisi. Au na nyie mkiona askari hawa wakatili wanavyotuua mnafurahi? Hakika nawaambia bunge la awamu hii likiisha hamjatafuta suluhu ya sisi tuliokosa mikopo tutawalaani sana kwani mtakua mmeshirikiana na serikali kutunyima haki na kula anasa kwa pesa za walipakodi. Tusaidieni jamani tunakufa na njaa, hatujalipa ada pia hatuna hela, muogopeni mungu jamani anayewapeleka dodoma salama.

Anonymous said...

Rais kikwete, umeleta askari wako watupige chuoni, miliwapiga wazee wa A mashariki mkawadhalilisha, mmewapiga wamachinga wasio na kipato wakitafuta walau watakulaje, kama hiyo haitoshi mmetupiga wasomi tusiseme madai yetu ya msingi. Laana hii itawafata nyuma siku zote na mwisho wenu hauko utafika. Mmeamua kuila nchi, kuwakandamiza masikini na kuwarudisha wakoloni kwa kivuli cha uwekezaji, leo rasilimali za nchi yetu na kodi za wazazi wetu mnagawana na familia zenu na kupanga nani apate kiasi gani na sisi masikini eti hamna hata hela za KUTUKOPESHA ili tusome. Kama kweli uko serious na taifa letu, tafadhali tupe mikopo watoto wa wakulima tusome. TENA JUA KUWA, TANZANIA SIO NCHI YA AMANI, UNADHANI KAMA WATU HAWAPATI HAKI ZAO, WANA NJAA, WANAKOSA ELIMU NIYO AMANI? Kama CCM ndivyo ina define amani basi imepitwa na wakati. Msijifariji kusema tanzania ina amani, yatawatokea puani, si mnafanya makusudi, kwa kuwa nyie na watoto wenu mna maisha ya kifahari ya pesa za kodi zetu! Poa yote 9.

Anonymous said...

MUKANDARA kaonyesha ana uwezo mdogo sana wa uongozi katika kipindi chake cha uongozi. kipindi cha Ruhanga hapakua na huu ujinga, wanafunzi kupigwa mabomu ....... yeye kama Professor anashindwa align na wanafunzi na kuweza kuyatatua haya mambo, na kama ni mambo ya bodi kwa nini yeye aingilie kwa kuita polisi, angeacha wanafunzi wagome mpaka Bodi watoe majibu -yeye hayamuhusu!
Shame on you MUKANDARA
p.d

Junior Rebel said...

KUPIGA WATU AU KUTISHIA WATU HAKUTAZUIA WATU KUDAI HAKI ZAO. TANZANIA SIO NCHI HURU TENA MAANA INAONEKANA UONGOZI WETU WA SASA UNATAWALA KIMABAVU. LAKINI I UNDERSTAND NA WATANZANIA WENGI SASA HIVI WANAELEWA KUWA "FREEDOM IS NOT FREE". I AM READY TO DIE TO BE FREE. ANGALIA YALIYOTOKEA TUNISIA, EGYPT, LIBYA NA NCHI NYINGINE MBALIMBALI DUNIANI. WATU WAKITAKA HAKI ZAO MTUTU HAUWEZI UKASHINDA.

Anonymous said...

balkaMmeona picha ya mabomu udsm kwenye gazeti la mmwananchi la trh 12? Hivi wale watu kumi waliokua mtaroni wamemkaba yule dada,ni askariiii au wabakaji?

Anonymous said...

pole Mhe.Mbunge, kazi yako ni kubwa sana njia mbadala ni kuwasaidia hawa ffu nachofahamu upeo wao ni mdogo, hawa hawa jioni wanakuja kukopa fedha kwa wazazi wa hawa wanafunzi siku zote hua nawaambia jamani ffu ni wajinga wamefungwa ufahamu,lakini pili kwao wanafunzi hatuna njia nyingine siku zote huwa nawaambia vifaranga hata mama yao akiwaacha hawafi wataparua hadi watakuwa, wazazi wao waliambiwa iogopeni serikali na kwa ujinga huo hata vijana wenzetu wengine wako bungeni kwa kupewa nafasi za bure sijui hata wamehonga nini wanafanya ujinga tu,vijana badilikeni hasa wale waliokipigia kura ccm,matunda yake ndo hayo poleni sana wananikumbusha mbali wadogo zangu, mara zote wale wanaoingia chuo baada ya uchaguzi hayo ndo matokeo yake,poleni sana tubadilike tuko vitani.da bertha.

Anonymous said...

mi sijui nisemeje kuhusu nchi yetu kwani ni sikitiko sana.viongozi wetu wa upinzani tusaidieni na Mungu wa Mbinguni atawalipa na kam sio hapa basi Mbinguni ambako ndiko kuliko na Makao ya Milele.