Kwa
mwezi huu wa Septemba, katika siku za katikati ya wiki nitaendelea na kazi za
kuwawakilisha wananchi kwa lengo la kuisimamia
serikali jimboni na kitaifa katika utekelezaji wa miradi ya maendeleo.
Kwa siku za mapumziko ya mwisho wa wiki, nitakuwa nafanya matukio na mikutano
ya kichama jimboni kwa malengo;
Mosi,
kutekeleza programu ya demokrasia na ujenzi wa chama ngazi ya chini katika kata
na mitaa mbalimbali.
Pili,
kuhamasisha viongozi na wanachama kufuatilia kazi za maendeleo jimboni na
kujiandaa kutoa maoni ya mabadiliko ya Katiba Mpya.
Jana
Septemba 1, 2012 nilianza kata ya Msigani-Makondeni, Mbezi Hii, Malambamawili,
Msingwa, Bwaloni na Masaki ambapo nilizindua misingi, matawi,ofisi na nimepokea
wanachama. Aidha nimesomewa risala za masuala ya kufuatilia, nimeulizwa maswali
na nimehutubia kama njia moja wapo ya kujibu baadhi ya hoja zenye kuhitaji
majibu na ufafanuzi.
Leo
Septemba 2, 2012 nitakuwa kata ya Mbezi-Luis; Kilimahewa, Msumi, Msakuzi,
Makabe na Mshikamano.
Njoo
ushiriki, tulijenge jimbo letu. Kwa pamoja tunaweza.
Maslahi
ya Umma Kwanza.
John Mnyika (MB)
Jimboni Ubungo
02 Septemba, 2012
No comments:
Post a Comment