Sunday, July 22, 2012

PICHA ZA ZIARA ZA VIONGOZI WA CHADEMA, Ndago Mkoani Singida

Mbunge wa jimbo la Ubungo jijini Dar-es-salaam,John
Mnyika,akihutubia wakazi wa kijiji cha Ndago jimbo la Iramba magharibi.

Baadhi ya Viongozi wa CHADEMA waliokuwa
katika mkutano huo ,kulia Dr Kitila Mkumbo
 
 Kiongozi wa CHADEMA,Bwana Chacha Waitara

Mbunge wa jimbo la Ubungo jijini Dar-es-salaam,John
Mnyika,akihutubia wakazi wa kijiji cha Ndago jimbo la Iramba magharibi.

Baadhi ya wakazi wa kijiji cha Ndago waliohudhuria mkutano wa
hadhara ulioitishwa kwa ajili ya viongozi wa CHADEMA 
kuzungumza nao.Picha zote na (Mpiga picha maalum)

Baadhi ya askari wa FFU walioitwa na viongozi wa CHADEMA
kwenda katika Kijiji cha Ndago, Jimbo la Iramba Magharibi, Julai 14, 2012.
Viongozi hao walilazimika kuwapigia simu RPC na OCD wa Iramba kuwataarifu
juu ya kuwepo kwa kikundi cha watu wachache waliokuwa wakifanya fujo
kuvuruga mkutano huo wa CHADEMA. Askari hao ingawa walifika kwa kuchelewa,
wakati mkutano uliokuwa ukiendelea kwa amani baada ya vurugu kudhibitiwa na
wananchi wenyewe, walikaa kwa muda mfupi kuulinda mkutano huo mpaka mwisho,
kisha msafara wa chama hicho, ukaelekea mkutano wa pili, Kata ya Kinampanda.

1 comment:

Anonymous said...

Muheshimiwa me ni mdau, naomba kuuliza hii sheria ya mifuko ya jamii yaani nssf,ppf kwanini wanaweka sheria ambazo hazifai? sasa hivi wanasema mwanachama hawezi kuchukua pesa yake mpaka afikishe miaka 55, hii ni haki kweli au serikali anataka tu kugandamiza wanyonge? hebu fikiria mtu anaacha kazi au anafukuzwa kazi hasa ktk sekta binafsi ataishije kabla hajapata kazi sehemu nyingine? ina maana ile hela alokusanya kipindi anafanya kazi ndo ingemsaidia wakati huo, istosha ni watu wangapi wanafikisha hiyo miaka 55 kwa karne hii? na mtu utakapofikisha hiyo 55 je kwa waajiriwa binafsi unaweza kuta hata hiyo kampuni ilyokuwa imekuajiri imeshakufa je utapata wapi records zako? tunaomba jamani mtusaidie kufikisha ujumbe tutendewe haki wananchi.