Saturday, July 21, 2012

Singida:Polisi wasogeza muda.

Polisi wamesema tuongeze muda wa kusubiri kwa kuwa gari la kikosi chao toka  Dar es Salaam imepata tatizo. Tumewaeleza ikifika saa 11 jioni ama RPC aliyetuita atuhoji au turudi Dodoma hicho kikosi kilichokuja kitufate. Nimepata  hapa ushahidi wa nyaraka kuwa pamoja na vijana kikundi kidogo cha vijana wa CCM Ndago,Iramba waliofunguliwa jalada wakamatwe kwa kurusha mawe mkutanoni kuna vijana wengine toka Dar Es Salaam na maeneo mengine ya Singida ambao ni sehemu ya watuhumiwa na viongozi wa CCM wanahangaika kuwawekea dhamana. Taratibu ukweli unazidi kuibuka. Kuna njama zilipangwa na baadhi ya viongozi wa serikali, polisi na CCM juu yangu. Nasubiri nikiona kama wana muelekeo wa kuzitekeleza wakati wa mahojiano na polisi nitaweka mambo hadharani hatua kwa hatua.

Maslahi ya Umma Kwanza

John John Mnyika,
Mbunge Jimbo la Ubungo (CHADEMA)
18.07.2012

2 comments:

Anonymous said...

Asante kwa updatea hizo. Hiyo ndiyo polisi yetu! Sgd kuna polisi ni vipi polisi wa kukuhoji atoke Dar? Kama ni wa upelelezi, kwanini hawakuja kukupeleleza ulipo? Au ndo yale yale tuliyoyasikia wanataka kukulimboka? Be care guy!

Anonymous said...

Mh. Mnyika, kabla ya mahojiano na polisi ulijitahidi kutupatia updates za kinachoendelea. Vipi, mbona kimya kimetawala ghafla? Au kwa kuwa swala tayari liko polisi haliwezi kuongeleka? Tupe kinachoendela.