Wednesday, December 12, 2012

Uzinduzi hospitali ya Sinza na ufafanuzi sahihi wa suala la Sekta ya Afya






Jana, 11 Desemba 2012 Nimeshiriki uzinduzi makabidhiano ya jengo la huduma za mama na mtoto katika hospitali ya Sinza (ipo Sinza-Palestina) kwa msaada wa Korea ikiwa ni sehemu ya kuboresha huduma za afya.

Ipo haja ya kuongeza watumishi wa afya ikiwemo madaktari kwa kupanua wigo wa elimu kwa ujenzi wa Chuo Kikuu MUHAS, eneo la Kwembe Mloganzila.

Hata hivyo, nilitarajia Rais Kikwete angeeleza serikali ilivyojipanga kuboresha maslahi ya madaktari kwa kurejea taarifa ya kamati ya huduma za jamii iliyoundwa baada ya mgomo wa madaktari ili kuepusha kasi ya madaktari kwenda nchi za nje, badala yake Rais ametoa kauli nyingine tata.

Aida, Rais amepotoshwa kuwa wanasiasa wa upinzani wamepinga ujenzi wa MUHAS na kuahidi fidia ya usumbufu. Ukweli ni kuwa aliyewaahidi wananchi fidia ya ardhi ni aliyekuwa Waziri wa Ardhi, Bwana John Chiligati mnamo mwaka 2009 na 2010 kwa ajili ya CCM kupata kura kwenye uchaguzi za serikali ya mitaa na Uchaguzi Mkuu. Wananchi wanachodai ni waliyoahidiwa na serikali.

John John Mnyika,
Mbunge wa Jimbo la Ubungo,
12/12/2012 


*Shukrani kwa blogu ya HakiNgowi na IssaMichuzi kwa picha

No comments: