Tuesday, February 1, 2011

Shukrani kwa Kongamano la Maji

Ndugu wananchi, wadau wa maji(wataalamu na taasisi),

Napenda kutoa shukrani zangu za dhati kwa mwitikio mzuri mliotoa kwa Kongamano la Maji 31.01.2011. Nawashukuru wote ambao walishiriki katika tukio, pia ambao walitoa mchango na maoni yao kwa njia ya simu, facebook na blogu. Asanteni sana!

Muda si mrefu, taarifa ya kina na picha za tukio zima zitakuwa humu kwa matumizi ya umma.

Hakika Umoja ni Nguvu, Tuzidi kushauriana, na kuungana katika kutafuta suluhu ya kero ya Maji na kero nyingine zinazokabili jimbo letu la Ubungo.

Daima maslahi ya Umma Kwanza.

©John J. MNYIKA.

6 comments:

Unknown said...

This is what we wanted big up kaka

SILAYO,A said...

Big up kaka, hiyo ndo nguvu ya umma, haizimwi kwa maji wala mchanga.Pamoja tusonge mbele

Unknown said...

Hongera sana Mheshimiwa, pia hongereni wananchi mliofanikiwa kufika kwnye kongamano hilo muhimu sana kwa maendeleo si ya Ubungo tu bali ya Taifa kwa ujumla.

We hope to hear from Mheshimiwa soon.

Active said...

Mkuu naomba na tatizo la barabara ya Mbezi luis mpaka mbezi Beach ,Mbezi Luis mpaka uwanja wa ndege pugu road tafadhali nayo ongeza nguvu tangu Kaenja mpaka leo Haijawa Natuin wewe tu utaweza kufanya ki ukweli maana ni muhimu sana tunapita kwa shida na inaoka foleni ubungo MKUU TAFADHALI jitahidi sana mambo ni mengi ila ndo hivyo mkuu TANAKUTUMAINIA SANA WAPIGA KURA WAKO AHSANTE.

Bill Muge said...

Mimi nasubiria huo mrejesho. But honestly ongera sana kwa ideas maana wapo wengi walishindwa kuandaaa vitu kama hivi. Ni mwanzo mzuri sana katika njia yako. Humo humo kwenye mstari.

Anonymous said...

hongera sana muheshimiwa kwa juhudi zako binafsi unazozionyesha pamoja na hayo yote kunakilio kingine kwa watu wa mlonganzila kibamba karibu na eneo ambalo muhimbili wamelichukua muheshimiwa eneo hilo halina umeme ila limezunguukwa na umeme tanesco waliisha kuja tangu mwaka juzi na kuweka alama za nguzo za umeme cha ajabu mpaka leo hakuna cha nguzo wala dalili za kuwekwa nguzo hizo mimi binafsi nipo nje ya nchi kimasomo nakuja huko wakati wa mapumziko ya kila mwaka mi nimkazi wa sehemu hiyo diwani wetu ni mama mmoja jina silifahamu sababu wakati wa zoezi la uchaguzi nilikuwa sipo huko tunaomba muheshimiwa jaribu kutuondolea kero hiyo samahani na pole kwa usumbufu nakuomba usituchoke