Saturday, May 19, 2012

Kwenda mahakamani 24 Mei na "Get Together" baada ya Hukumu

Nashukuru wote mliojumuika katika mkutano wa leo wa kata na matawi jimboni Ubungo, nimefarijika na azimio lenu la kuja kwa wingi mahakamani tarehe 24 Mei kusikiliza hukumu dhidi ya kura zenu.

Nimevutiwa pia na azimio la kuwa na ‘get together bottle party’ siku hiyo hiyo baada ya hukumu ‘kwa utawala binafsi’.

Kwa swala na sala mlizoswali na kusali leo kwa pamoja, naamini Mwenyezi Mungu atawezesha kutolewa hukumu ya haki.

1 comment:

Bright Sospeter said...

Mungu yuko nawe,na matumaini yangu kesho mahakama itatenda haki.
Hakuna mtu mwenye uwezo wa kuinyang'anya haki ya wanachi.