Friday, May 4, 2012

Hukumu ya kesi yetu tarehe 24 Mei; tumuombee Jaji

Tumemaliza majumuisho ya kesi dhidi yetu. Hukumu imepangwa kutolewa tarehe 24 Mei 2012. Mawakili wote wawili wa upande wa utetezi wametimiza wajibu wao.


Pamoja na kuwa mawakili kwa ujumla walizungumza kwa zaidi ya saa saba, namnukuu kiduchu Wakili wetu Mbogoro: “Mshindi wa uchaguzi anatokana na maamuzi ya watu wengi, haki ambayo huipata kwa nadra kila baada ya miaka mitano na ni mchakato unaotumia fedha nyingi za walipa kodi. Hivyo kiwango cha uthibitisho wa madai yoyote lazima kiwe bila ya shaka yoyote………mlalamikaji Hawa Ng’umbi amesema mwenyewe mahakamani kuwa hana tatizo na matokeo ya toka vituoni, malalamiko yake sio juu ya nani mshindi. Kwa kawaida kesi za uchaguzi hufunguliwa na wenye kupinga ushindi wanaodai kuwa wangeshinda wao iwapo sheria zisingekiukwa; kama hapingi matokeo ya vituoni ambayo majumuisho yake ndio yamempa Mnyika ushindi; tunaweza kujiuliza tuko hapa kwa ajili gani?”

Tuungane pamoja katika sala na swala kumwombea kwa Mwenyezi Mungu Jaji Upendo Msuya afanye maamuzi ya haki.

4 comments:

Phiemon Kilibata said...

Tuko Pamoja Katika Kumwombea Upendo (Mheshimiwa)

Anonymous said...

nina amini kama mahakama haitaingiliwa na muhimili mwingine wa dola na kufanya kazi yake kwa uhuru na haki,mh.myika atakuwa mbunge halali wa ubungo na mtetezi wawanyonge wa tanzania kwa ujumla,naiomba mahakama itende haki tupu.

Mtumishi wa Mungu na Wanadamu said...

The Lord God will see you through now and then, he will be your companion, he will lead you, he will hold and mould you for his Glory and prosperity of His own people, he will makes you shine like a morning star, No evil shall stand against you, no weapon shall rise on you, no anemy shall defeat you, no obstacle shall pull you back, Its because you have chosen to save only God and his people, The Lord will lift up you name for his own Glory, In The Name of Father and Son and Holly Spririty!!!

Bright Sospeter said...

Ni nana imani kubwa na mahakama,ni chombo huru kinachofanya maamuzi yake bila kuingiliwa,hivyo basi kama wanachi walikuamini kwa kura zaidi ya elfu 60,hakuna yeyote atayeweza kupingana na maamuzi ya wanachi.
Mungu amtangulie jaji atayesoma hukumu hii na ushindi ubaki kuwa kwa mshindi.