Thursday, August 9, 2012

Maboresho madogo kukurahisishia kuramba (browsing) blog hii.

No. 1
Nashukuru sana kwa kuendelea kuwa nami katika harakati za kuleta mabadiliko ya kweli katika ngazi ya jimbo na taifa. Napenda kutangaza maboresho madogo ambayo yamefanyika katika blog hii kukurahisishia msomaji kuramba au ku-browse.

Maboresho yenyewe ni kama ifuatanyo;
Kurasa kuu za Blog hii; sasa ni rahisi kufungua kurasa kuu za Blog hii. Baada ya kubofya na kuingia katika blog hii, msomaji ataona chini tu ya picha kuu ya Blog eneo la kubofya na kuingia katika kurasa zote kuu. Kurasa hizi ni HOME; CHANGIA na WASILIANA NA MBUNGE. Kurejea katika kurasa kuu yenye taarifa zote zilizochapishwa kwenye Blog hii, bofya katika kurasa ya "HOME". Kupata maelezo ya namna ya kuchangia harakati za Mbunge na Chama, bofya "CHANGIA". Na kupata maelezo ya namna ya kuwasiliana na Mbunge, bofya "WASILIANA NA MBUNGE".

Picha No. 2
Tafuta Kupitia Hapa; taarifa zilizochapishwa katika Blog hii ni nyingi. Inawezekana unatafuta taarifa ambayo ipo katika kumbukumbu na si rahisi kuipata. Tumia eneo la kutafuta taariya. Angalia Picha No. 2 kwa mwongozo zaidi.

Picha No. 3
Zimesomwa Zaidi; Mbunge wa jimbo la Ubungo anachapisha taarifa nyingi katika Blog hii. Wakati mwingine si rahisi kusoma taarifa zote au kujua ni taarifa zipi zimewagusa wengi na hivyo wewe kuzisoma pia. Upande wa kulia, kati kati ya sura kuu ya Blog hii ni eneo lenye orodha ya Taarifa Tano ambazo zimesomwa zaidi katika muda wa mwezi mmoja. Shiriki nawe kuzisoma na wote tuchangie mabadiliko kulingana na uwezo wetu. 
Picha No. 3

Picha No. 4
Taarifa Mpya na Taarifa Zilizopita; tangu kuanzisha Blog hii, Mbunge amechapisha taarifa zaidi ma mara 350 hapa. Unaweza kuramba orodha ya taarifa hizi kwa namna mbili. Mosi ni kwa kutumia kipengele cha "KUMBUKUMBU" upande wa kulia, katikati mwa sura kuu ya Blog hii. Mbili ni kwa kufunua kurasa baada ya kurasa kuziona taarifa zilizopita. Hii unaweza kufanya kwa kwenda chini kabisa mwa Blog hii panapofanana na kielelezo katika picha No. 4



Nazidi kutanguliza shukrani zangu.


Maslahi ya Umma KWANZA.

John Mnyika (Mb)

Bungeni-Dodoma

09/08/2012

No comments: