Nimetoka kwenye kikao cha RCC.
Itachukua muda kwa uozo aliouanika
kwenye UDA, kituo cha mabasi Ubungo, soko la Karikoo, fidia ya wahanga wa
mabomu Gongo la Mboto, EAMTCO kushughulikiwa!
Nchi hii ina uozo sehemu nyingi
hali inayohitaji mabadiliko ya utawala ili kuharakisha maendeleo. Kadiri
tunavyojifungia DSM na kuleta maendeleo kidogo mjini, huku vijijini wakididimia
kwenye umaskini ndivyo watu wengi hukimbilia DSM na vijana kukosa ajira na
miundo mbinu ya maji, barabara na mengine mengi kuzidiwa DSM. Hatimaye DSM nayo
itaendelea kuwa jiji lenye kero. Kwa hiyo, tunao wajibu pamoja na kuisimamia
serikali kwa maendeleo ya DSM, tuna wajibu pia wa kuunganisha nguvu kuwezesha
vuguvugu la mabadiliko vijijini. Leo naelekea Morogoro, kesho nitakuwa Iringa
na kesho kutwa nitarejea DSM kuendelea na kazi za maendeleo jimboni Ubungo kwa
mwezi mzima wa Septemba.
Maslahi ya Umma Kwanza.
John
John Mnyika
Jimboni
Ubungo
27
Agosti, 2012
No comments:
Post a Comment