Sunday, August 5, 2012

MKUTANO WA MTANDAONI KUHUSU MUSWADA WA SHERIA YA MAREKEBISHO YA SHERIA YA HIFADHI ZA JAMII KWA HATI YA DHARURA KUREJESHA FAO LA KUJITOA

Ndugu wafanyakazi na wadau wa hifadhi ya jamii,

Nawashukuru kwa kushiriki mkutano huu wa mtandaoni (online meeting) wenye ajenda moja ya kupokea maoni ya kuwezesha kuwasilishwa kwa Muswada wa Sheria ya Marekebisho ya Sheria za Hifadhi ya Jamii kwa hati ya dharura kurejesha fao la kujitoa.

Toka juzi tarehe 3 Agosti 2012 nilipotoa taarifa kwa umma ya kueleza kusudio la kuwasilisha muswada husika katika mkutano wa Bunge unaoendelea nimepokea mwito wa wafanyakazi wa baadhi ya migodi nchini kwa nafasi yangu ya Waziri Kivuli wa Nishati na Madini kwenda kwenye migodi husika kwa ajili ya kupokea maoni. Aidha, kufuatia kusudio hilo yametolewa pia maoni na wafanyakazi wa sekta nyingine katika Jimbo la Ubungo na maeneo mengine nchini kwenye mitandao ya kijamii na kupitia simu kuhusu haja ya kukusanya maoni kuhusu muswada husika.

Mkutano huu ni mwanzo wa mchakato wa kuitika mwito huo na kuzingatia maoni yaliyotolewa na tutaelezana ratiba ya ukusanyaji wa maoni ya ziada kupitia mikutano na njia nyingine za mawasiliano kwa ajili ya kufanikisha azma husika kwa haraka.

Ikumbukwe kuwa tarehe 03 Agosti 2012 kwa mujibu wa Kanuni ya 68 (7) ya Kanuni za Kudumu za Bunge na kwa kuzingatia kuwa marekebisho yamefanyika kwenye ratiba ya bunge ambapo Mkutano wa Bunge sasa umepangwa kuahirishwa tarehe 16 Agosti 2012 na hoja za wabunge zimeondolewa kwenye ratiba.

Niliomba muongozo ama Serikali itoe kauli bungeni ya kutengua tangazo lililotolewa na Mamlaka ya Usimamizi na Udhibiti wa Sekta ya Hifadhi ya Jamii (SSRA) ili kuwezesha mafao ya kujitoa kuendelea kutolewa au uongozi wa Bunge uruhusu niwasilishe muswada binafsi wa sheria kwa hati ya dharura tarehe 16 Agosti 2012 kwa ajili ya kufanya marekebisho kwenye sheria husika ili kuruhusu mafao ya kujitoa kuendelea kutolewa.

Irejewe kuwa pamoja na hatua hiyo ya kuomba muongozo nilichukua hatua ya ziada ya kumwandikia Katibu wa Bunge kumweleza kusudio la kuwasilisha Muswada Binafsi wa Sheria ya Marekebisho ya Sheria ya Sheria za Hifadhi ya Jamii (The Social Security Laws (Ammendments) Act wa mwaka 2012 kwa hati ya dharura kwa mujibu wa Kanuni ya 81 ya Kanuni za Kudumu za Bunge (Toleo la Mwaka 2007).

Lengo la Muswada huo ni kufanya marekebisho yenye kuwezesha kurejeshwa kwa fao la kujitoa (withdrawal benefits) ili kuruhusu kuendelea kutolewa kwa mafao kwa mwanachama wa mfuko ya hifadhi ya jamii anapoacha kazi na kuhitaji kupewa mafao yake kabla ya kufikisha umri wa kustaafu kwa hiari (miaka 55) au kwa lazima (miaka 60) au pale anapopata ulemavu wa kudumu.

Katika mkutano wa leo, pamoja na mambo mengine napendekeza maoni yatolewe kuhusu masuala yafuatayo:

Mosi, kuhusu taarifa ya Serikali kuwa marekebisho kuhusu kusitisha fao la kujitoa yamefanyika ili kutimiza lengo na madhumuni ya Hifadhi ya Jamii ambayo ni kuhakikisha kuwa Mwanachama anapostaafu anapata mafao bora yatayomwezesha kumudu hali ya maisha uzeeni.

Pili, kwamba mchakato wa marekebisho hayo ulihusisha wadau kwa kuzingatia utatu yaani wawakilishi kutoka Vyama vya Wafanyakazi, Chama cha Waajiri na Serikali

Tatu, kuwa mchakato unaendelea wa kuandaliwa kwa miongozo na kanuni za mafao ambazo lengo lake ni kuboresha maslahi ya wanachama kwa kutambua tofauti za ajira, tofauti za mazingira ya kazi, tofauti za sababu za ukomo wa ajira na umuhimu wa mwanachama kunufaika na michango yake wakati angali katika ajira.

Nne, juu ya uamuzi wa kusitisha maombi mapya ya kujitoa kwa kipindi cha miezi sita kufuatia kuanza kutumika kwa sheria mpaka pale miongozo itakapotolewa na elimu kwa wadau kuandaliwa.

Tano, maoni mahsusi ya kuingizwa kwenye Muswada Binafsi wa Sheria kwa mujibu wa Kanuni ya 81 (1), Taarifa ya Muswada huo kwa mujibu wa Kanuni ya 81 (2), hati ya kuwasilisha muswada kwa dharura na hoja ya kutengua masharti kuhusu muda wa utangazaji wa Miswada ya Sheria kwa mujibu wa Kanuni ya 81 (5) ya Kanuni za Kudumu za Bunge (Toleo la Mwaka 2007).

NAMNA CHANGIA:

Baada ya mada hii “post” angalia chini eneo limeandikwa “comments” bofya hapo na utafunguka ukurasa wa kuandika. Unaweza andika na jina lako, au ukawa huru wa kutoandika jina “anonymous”. Changia sasa!!

Aidha, mwenye nyaraka yoyote anaweza kuituma kupitia jmnyika@parliament.go.tz na nakala kwenye mbungeubungo@yahoo.com; nyaraka hizo kwa ajili ya rejea ni pamoja na Social Security Ammendment Act no.5 ya mwaka 2012, Sheria za Hifadhi ya Jamii zinazohusika, Taarifa na mapendekezo yaliyowasilishwa na kupelekea kufutwa kwa mafao ya kujitoa (withdrawal benefits) na maelezo kuhusu hatua ambayo kifungu husika kiliingizwa na hatimaye kupitishwa na Bunge tarehe 13 Aprili 2012.

Mkutano huu unafanyika kwa kuzingatia haki za Katiba ya Nchi hususani ibara ya 18 juu ya haki ya uhuru wa mawazo na ibara ya 21 juu ya haki na uhuru wa kushiriki kwa ukamilifu katika kufikia uamuzi juu ya mambo yanayohusu raia, maisha yake au yanayolihusu taifa.

Pamoja na haki na uhuru huo nawaomba watoa maoni tuheshimu “Kanuni ya Dhahabu” katika mkutano wetu. Mkutano huu umefunguliwa rasmi na tuendelee kutoa maoni na kujadiliana.

Maslahi ya Umma KWANZA.


John Mnyika (Mb)


Bungeni-Dodoma


05/08/2012

134 comments:

Unknown said...

NI VYEMA MFANYAKAZI AKAPEWA MAFAO YAKE PALE ATAKAPOSITISHA AJIRA YAKE KWA MUAJIRI MMOJA MAANA HAKUNA UHAKIKA KAMA ATAPENDELEA KUENDELEA NA AJIRA AU KUJIAJIRI NA PIA WAKATI AKIWA HANA AJIRA HAYO MAFAO YATAMSAIDIA KUMSUKUMA MPAKA ATAKAPOPATA SHUGHULI NYINGINE YA KUMUINGIZIA KIPATO. LABDA KWA WALE WANAOAJIRIRIWA KWA AJIRA ZA KUDUMU NDIO WASUBIRIE UMRI WA MIAKA 55 LAKINI KWA DHARURA YOYOTE KAMA YA KIFO AU MARADHI YA KUDUMU MWAJIRIWA APEWE MAFAO HUSIKA KWA MUDA HUSIKA.

Mkina said...

Kwanza nikupongeze Mnyika kwa kuamua kulivalia njuga suala hili kiasi cha kuonesha matumaini ya neema huko mbeleni, hata kama sasa 'wakuu' wataona haifai.

Kuwepo kwa sheria ya zuio la kuondoa mafao ya mchangia katika mifuko ya jamii, kumewaliza mno Watanzania wengi ambao, kimsingi ndiyo wangepaswa kushirikishwa kwanza kutoa maoni yao juu ya kila hatua za awali za kusudio la kuwepo sheria hii, lakini hilo inavyoonekana halikufanyika na mwisho wake leo imegeuka kuwa kadhia.
Ni vyema sasa, kwa kuwa watu wengi wanapinga kuwepo kwa sheria hiyo na huku wakienda mbele zaidi kuituhumu serikali kwamba ina huenda ikawa na mkono wake, kwa kuwa 'imefilisika', na sasa inasaka pesa kwa kila njia ili kazi zake ziende.
Mbaya zaidi watu wengi wamekosa imani na mifuko ya jamii, kwa kuwa wameanza kujenga hisia kuwa fedha zao zinakusanywa na kuingizwa katika miradi isiyokuwa na tija kwao na kuwafaidisha zaidi watendaji wakuu wa mifuko hiyo na hata wabunge wa kamati inayohusika kwa kulipwa posho nono, mikopo na tuhuma zangine za namna hiyo.
Ni vyema nguvu kubwa ya busara ikatumika, kwa wabunge na wahusika wengine, kuachana na sheria hii, au kuirekebisha kwa kuaondoa kipengele hicho ili kila mfanyakazi awe huru, kila anapoacha kazi kuchukua chake.
Uhakika ni kwamba hicho kinachozungumzwa kuwa kutakuwa na mikopo ya nyumba kwa wafanyakazi wanaokaribia ustaafu, ni kiinimacho tu na mwisho wa siku wafanyakazi wa sasa watageuka kuwa kama wale wenzao wa Afrika Mashariki ambao tunashuhudia wengi wakifa hata kablaya kulipwa stahili zao

Anonymous said...

habari HON MP mimi binafsi ni mhanga wa hii sheria ya mafao ya kujitoa na nilishajaza fomu kabisa na ilishaanza kufanyiwa kazi niilipeleka arusha kwenye tawi lao mapema sasa nimefuatilia makao makuu wanasema fomu imefika baada ya tangazo la SSRA kwa maana ni zaidi ya 20.07.2012,binafsi nimeudhunishwa sana maana kwa sasa sina ajira yeyote na hizo pesa nilikuwa nazitegemea niweze kuanza kufungua kampuni binafsi sasa imekuwa ni kero... hili tukio linanifanya niichukie serikali . SIAMINI KAMA KUNA MBUNGE ANAWEZA KUPINGA HII HOJA YAKO YA KUWASILISHWA HATI YA DHARURA KUHUSU HUU MSWAADA DHARIMU. BINAFSI NAKUONA NI MTU MWENYE NIA THABITI KWENYE UKOMBOZI WA TANZANIA ..NAAMINI UTAFANIKIWA MAANA BADO SIJAPATA MANTIKI YA KWANINI WAO WATOE HILI FAO BILA KUNISHIRIKISHA..?

Anonymous said...

Mwanachama awe na option ya kujitoa na kupata mafao yake, hiyo ni kwa mifuko ya NSSF, PPF, LAPF na PSPF. Kwa mfuko wa GEPF, mwanachama awe na option ya kuchukua mafao yake pindi mkataba wake unapoisha. Walakini hii isimzuie mwanachama anayetaka kuweka michango yake for as long as he likes.

Unknown said...

1.lengo maalumu---hakuna lengo maalumu kwa ujumla wafanyakazi wa sekta binafsi huwa wana kuwa wamejiandaa vema kabla ya kustaafu kuliko hao wa serikali. kumaanisha kuwa iyo sio msaada kwake. then watu sector binafsi wanafanya kazi kwa mikataba, itakuwaje??? ufanye kazi miaka 2 let say una 20 year then baada ya miaka 2 umeacha job na huajiriki unasubiri mpaka 55! how???
2/3 izo vitu siwezi changia. mchakato haukuwa husishi, kumanisha kuwa hata huo mwongozo ufutwe na sheria nzima isimamishwe ikiwezekana hata na mahamkama.
maombi mapya yaendeleee.
NI MUHIMU IJULIKANE KUWA VIJANA WENGI KWENYE PRIVATE WANAFANYA KAZI KWA MALENGO BAADA YA MUDA MFUPI WANAACHA KAZI NA KUJIAJIRI KWA KUTUMIA PESA IYO YA NSSF.

Unknown said...

kwa wale wa sekta binafsi hii sheria ndio mbaya zaidi kwani kila siku tunabadili ajira kampuni zinafungwa na tunahama na mikataba inaisha na mbaya zaidi hizo kampuni baada ya mda zinafungwa kabisa na wamiliki wanaishia uko makwao sasa ktk ufuatiliaji kama si muda huohuo itakua ngumu!

Erick Mukulu Brighton said...

Hili suala kiujumla limefanyika kwa kukurupuka naweza sema na hii inatokana na kutokuwepo na uwazi katika ushirikishwaji wa vyombo husika vinavyosimamia maslahi ya wafanyakazi, pia mchakato huu haujaweza kuforecast mbele kwa kuangalia hali halisi za maisha ya watanzania leo ninaweza nikafukuzwa na nikaamua kutokuajiriwa upya, pia nnaweza nikaamua kuacha kazi na kwenda kuishi nchi yoyote so for that case maslahi yangu yatakua yamepotea. mi nafikiri hii mifuko inaoperate kama Bank so maamuzi ya mafao yabaki kuwa mikononi mwa mchangiaji.

PAI said...

Irene Isaka
MKURUGENZI MKUU WA SSRA, Kaandika nyaraka nyingi kwa mameneja wa Migodi lakini cha ajabu hakuwacopy mameneja na wakurugenzi wa Mifuko kama NSSF na PPF, hapa tuna wasisi wasi huenda yeye anasimamia hawa mameneja na si mifuko ya jamii. NADHANI ALIPASWA AANDIKE KWA MKURUGENZI HUSIKA KUMWAGIZA JUU YA KILE ALICHO MWANDIKIA MENEJA WA MGODI HUSIKA KISAHA WAKURUGENZI WA MIFUKO WAWAANDIKIE MAMENEJA WA MIGODI NA MAMENEJA WA MIGODI WATUANDIKIE SISI WAFANYAKAZI,HILI LINAONESHA WAZI KUWA WAAJIRI HASA WA MIGODINI HUENDA WALISHILIKI KIKAMILIFU, TUNAPATA WASIWASI KWA HILI.

Anonymous said...

Ni vizuri pia ikaeleweka kwamba hifadhi ya jamii, kwa upana wake, haimsubiri mpaka mtu awe na miaka 55. Hifadhi ya jamii ni pamoja na kumuwezesha mwanachama kumudu maisha pale anapojitoa. Pensheni ya uzeeni ni moja tu ya hifadhi ya jamii na inaleta maana kwa mtu aliye kwenye ajira. ..

Unknown said...

alafu huu upuuzi wa kuniambia nichukulie mkopo pesa yangu umetoka wapi? kama nna pesa yangu that i can use na nna shida kwa nini nisipewe tu badala ya kuitumia kunidhamini kwenye mkopo!

Anonymous said...

Hongera sana mheshimiwa Mnyika kwa ujasiri unaouonyesha kwa suala hili na mengine mengi.
Mfanyakazi ndiye anayelisukuma hili gurudumu zito sana la maendeleo. Inasikitisha sana kusikia ya kwamba mafao ambayo ameyachangia mwenyewe kwa jasho lake anawekewa masharti ya kuyapata ambayo yanalenga kwenye kumkandamiza zaidi na kumnyima haki yake ya msingi.
Ikumbukwe kuwa bila ya mfanyakazi hakuna NSSF. Mwalimu aliwahi kusema kwa kwenye video ya 'Fate Worse Than Debt' kwa lugha ya kiingereza ya kwamba 'There is a limit to milking a cow'. Tafsiri yake ni kwamba hata ng'ombe anafikia kiwango cha mwisho cha kukamuliwa, hutaweza kumkamua zaidi, atakufa!

jogi@jamiiforums.com said...

Mfano hai ni gtv

Anonymous said...

RWENYAGIRA(M4C)

KUMLAZIMISHA MTUMISHI AIDHA WASECTA BINAFSI AU YULE WA UMMA KUTOCHUKUA MAFAO YAKE BAADA YA KUACHA KAZI AU KUMALIZA MKATABA NI WIZI NA UNYANYASAJI MKUBWA WA SERIKALI HIZI ZA KIDHALIMU.IWEJE NI JIWEKEE MALENGO YANGU YA KUFANYA KAZI KWA MIAKA MITANO ALAFU MTU ANANIPANGIA KUWA STAPATA HAKI YANGU MPAKA NIFIKISHE MIAKA 55?KIPENGERE HIKI KIFUTWE MARA MOJA.

Anonymous said...

NIANZE KUSEMA WAZI KUWA SHERIA HII NI KANDAMIZI NA HAKI NA MTEJA;
1. KWANZA LIWEKWE WAZI KUWA LABDA PESA ZA WANACHAMA ZIMEKOPESHWA NA KUTUMIWA NA BAADA YA KUONA KUWA HAZIPO NDIPO SHERIA HII INAPITISHWA
2: PESA ZA WANACHAMA ZIMETUMIKA VIBAYA KATIKA KUWEKEZWA KATIKA VITEGA UCHUMI AMBAPO HAZIWEZI KURUDI HARAKA,
3: KTK SHERIA HII KUNA TETESI KUWA MADINI KWA VILE KUNA MAKAMPUNI YA WAWEKEZAJI WA NJE KAMA BARRICK, CASSPIAN-N.K, HUKO WATALIPWA MAANA KAZI ZAO NI ZA HATARI
4: HIVI WABUNGE MNAENDA KUWATETEA WATANZANIA AU WAGENI, KUMBUKA NCHI HII NI YA WATANZANIA, HIVYO SHERIA HII YA KUMYIMA MTANZANIA HAKI NA KUZIDI KUMKANDAMIZA NI HATARI SANA
5: JE MIAKA 50 YA UHURU SHERIA HII ILIKUWA WAPI IPITISHWE LEO BAADA YA MIFUKO KUINGILIWA NA MAFISADI WANAOJUA PESA ZAIDI ILI WAZITUMIE KWA KUKOPESHANA.
6: ITUNGWE NA SHERIA YA KUJITOA KWENYE MIFUKO. KODI YENYEWE NI UONEVU MAANA 282,720/=, PSPF 64,370/='TUGHE 25,748/=;MHIF 40,622/= HIVI NABAKI NA KIASI GANI CHA KUNIFANYA NIENDELEE KUFANYA MAENDELEO KATIKA UJANA WANGU

Anonymous said...

Binafsi sina mengi yakuzungumza Mh,ila hilo swala sikubaliani nalo kwa ujumla nikiwa kama muajiriwa,nitakapoachishwa kazi ama kuacha,itakuaje kwa familia yangu inayonitegemea kwa kila kitu?hizo ni pesa tunazozitumia katika kipindi hicho kigumu wakati tunajipanga kwa mambo mengneyo ya kujiajiri ama kuajiriwa.

Anonymous said...

Pensions funs have been spending our moneys recklessly.investing into unprofitable business,udom hostels,kigamboni bridge and so forth..if any member wants to withdraw her benefit what would be the impact in the long run?drying up of funds?death of pension funds?what an embarassment would it be to the nation?This is one of their strategies to rescue the situation.Lets look why they came with this proporsal to see where the real problem is..!viewing the matter with 3D eyes.

Unknown said...

Hakika katika hili serikali bado haijaonyesha dhamira ya dhati kwa watumishi wake badala yake imezidi kumchimbia shimo na kuhakikisha mtumishi na mkuza uchumi wa taifa hili anateketea kwa shida na ufukara. kwakweli hakuna mantiki katika sheria hiyo badara yake ni mwiba zaidi wenye lengo la kuakikisha mtanzania anaendelea kuwa maskini hadi kufa. naomba niishauli serikali kuondokana na dhana ya kuakikisha mtanzania naendelea kuwa maskini ili waweze kuendelea kutawa,na kati ya mbinu zao ni imekuwa hiyo ya kutunga sheria kaandamizi kwa watumishi wake. Mnyika pambana katika kweli watakuja kukuelewa ipo siku.

Anonymous said...

Haya ni moja ya marekebisho dhalimu kuwahi kufanywa na serikali kwa wafanyakazi. Nakupongeza Mh Mnyika kwa kulifuatilia hili japo nina wasiwasi kama litafanikiwa. Nachelea kuwaza ule msimamo wa "liwalo na liwe" utatumika hapa na wabunge walio wengi wataungana kuendelea "kuitetea" serikali badala ya sisi wananchi/wafanyakazi.

Hakuna mjadala hapa, marekebisho haya yatenguliwe mara moja na ikiwezekana hata huo muda wa kusubiri miezi sita baada ya kuacha ajira upunguzwe.

Nina swali, Mheshimiwa, mlikuwa wapi wakati haya yanapitishwa? Sio wapinzani, sio chama tawala... wote mlishiriki kutukandamiza. Nawaomba na kuwasihi muonyeshe ushirikiano huohuo katika kutengua huu udhalimu.

Pess said...

sidhani kama serikali ilifikiria hili suala kwa makini kabla ya kupitisha uamuzi huo, nasema serikali ndio imepitisha kwa sababu hata kama wabunge wetu ni mabwege na wazembe kiasi gani, wasingeweza kuoverlook suala muhimu kama hili, nadhani liliingizwa kinyemela baada ya muswada husika kupitishwa na wabunge wetu hawa, kwa hiyo mimi binafsi na wafanyakazi wengine, especially wa sekta binafsi hatuafiki kabisa mpango huu kwa sababu ya nature ya ajira yetu ambayo kwa kweli haina guaranteee kabisa na pesa pekee ambayo tunaweza sema kwamba tunayo kwa ajili ya kuanzishia maisha ndio hiyo ya kwenye mashirika ya kijamii, so kuniambia kwamba nisubiri mpaka nifike miaka 55 hiyo inakuwa ni suicide mission which we wont agree with it! so tunakutuma mbunge wetu wewe wa taifa, ukawaambie kwamba kuwe na kipengele cha kuamua, kwamba nifikishe miaka hiyo ndio nichukue au ajira yangu ikicease then nachukua changu, and that is what we want!

PAM said...

NIANZE NI HOJA YA KWANZA,KIUKWELI MM SIONI NA SIDHANI KAMA SERIKALI NA HIYO MIFUKO YA JAMII WANAMAPENZI AU LENGO LA KWELI LA KUTAKKA KUWASAIDIA WATU ILI WAWEZE KUPATA MAISHA MAZURI AU KUJIKIM PALE WANAPOSTAAFU,,KWANZA IKUMBUKWE KUWA KWA JINSI HALI YA MAISHA INAVYOKUWA NGUMU KUTOKANA NA KUPANDA KWA GHARAMA ZA MAISHA MFANYAKAZ AWE SECTA BINAFSI AU ILE YA SERIKALI HAWEZ KUWA NA NGUVU ZA KUTOSHA KUMWEZESHA KUFANYA JAMBO LOLOTE LA MAANA PINDI ANAPOFIKIA UMRI WA KUSTAAFU,WENGI HUFIKIA UMRI HUU WAKATI TAYAR WANAMARADHI HASA YA MOYO,,KISUKARI ,,VIUNGO KUUMA KAMA MIGUU,MGONGO,,MACHO KUKOSA NGUVU NA VINGINE VINGI TU SASA UNAPOMWAMBIA MTU HUYU UTAMPA PESA HATA KAMA ZITAKUWA NYINGI KIASI GANI UNADHAN ZITAMSAIDIA?NI KWANN WATU WASIPEWE KULINGANA NA MTU MWENYEWE ANAVYOONA INAFAA NA ANANGUVU YA KUFANYIA JAMBO LA MSINGI NA LA MAANA ZAIDI LABDA SERIKALI INGEWEKA UTARATIBU WA KUFANYA UHAKIKI WA NN MFANYAKAZI ANATAKA KUFANYA KWA KUTUMIA FEDHA ALIZOZIPATA AU KUHIFADHI?

Anonymous said...

SWALI LA MSINGI NI JE?PAMOJA NA JITIHADA ZOTE ZA KUFANYA MAREKEBISHO YA FAO LA KUJITOA,NA JE IWEJE MIFUKO HII IWE INAKOPESHA SERIKALI,KWA JINSI INAVYOONEKANA NI SERIKALI IMEKOPA HELA NYINGI NA SASA KUNA UPUNGUFU MKUBWA WA HELA KWENYE HII MIFUKO,NA JE KAMA MAREKEBISHO YATAFANYIKA,SERIKALI ITACHUKUA HATUA GANI KUHAKIKISHA HAIFI HII MIFUKO KWA FINANCIAL PROB ,MAANA THAT IS THE FACT ,IMEISHIWA HELA HII MIFUKO

Anonymous said...

SWALI LA MSINGI NI JE?PAMOJA NA JITIHADA ZOTE ZA KUFANYA MAREKEBISHO YA FAO LA KUJITOA,NA JE IWEJE MIFUKO HII IWE INAKOPESHA SERIKALI,KWA JINSI INAVYOONEKANA NI SERIKALI IMEKOPA HELA NYINGI NA SASA KUNA UPUNGUFU MKUBWA WA HELA KWENYE HII MIFUKO,NA JE KAMA MAREKEBISHO YATAFANYIKA,SERIKALI ITACHUKUA HATUA GANI KUHAKIKISHA HAIFI HII MIFUKO KWA FINANCIAL PROB ,MAANA THAT IS THE FACT ,IMEISHIWA HELA HII MIFUKO

John Mnyika said...

Naomba kumjibu mtoa maoni wa saa 3:56 swali lake: ‘mlikuwa wapi wakati haya yanapitishwa? Sio wapinzani, sio chama tawala... wote mlishiriki kutukandamiza.”, kwa kurejea taarifa yangu ya tarehe 3 Agosti 2012 kwa umma kuwa:

“Ikumbukwe kwamba kifungu cha kufuta mafao ya kujitoa kilichozua mgogoro hakikuwepo wakati muswada uliposomwa kwa mara ya kwanza bungeni tarehe 1 Februari 2012 bali kiliwasilishwa kupitia jedwali la marekebisho ya Wizara lililowasilishwa tarehe 13 Aprili 2012 bila malengo na madhumuni yake kuelezwa kwa ukamilifu.

Kupitishwa kwa kifungu hicho kumethibitisha maneno niliyoyatoa bungeni kuwa tumefika hapa tulipo kutokana na ‘uzembe wa bunge na wabunge’ na kwa hili pamoja na mchango nilioutoa bungeni kwa maandishi siku hiyo juu ya haja ya kuwa mfumo mpana zaidi wa pensheni na hifadhi ya jamii (universal pension and social security) pamoja na kuwa sikuunga mkono kifungu husika kilichoingizwa kinyemela naomba radhi kwa wananchi wa Ubungo na wafanyakazi kwa kutokuwasilisha jedwali la marekebisho kupinga kifungu hicho kuingizwa.

Izingatiwe kuwa ili kurekebisha hali hiyo tarehe 27 Julai 2012 kwa nafasi yangu ya Waziri Kivuli wa Nishati na Madini kwa niaba ya Kambi Rasmi ya Upinzani niliitaka Serikali itoe maelezo maelezo kuhusu taarifa zilizotolewa bungeni tarehe 13 Aprili 2012 kuwa wafanyakazi ikiwemo wa migodini kupitia vyama vyao walihusishwa kutoa maoni yaliyopelekea kufutwa kwa fao la kujitoa (withdrawal benefits); suala ambalo Chama Cha Wafanyakazi wa Migodini (TAMICO) kililikanusha.

Hata hivyo, Waziri wa Nishati na Madini wakati wa majumuisho ya Hotuba yake tarehe 28 Julai 2012 hakutoa majibu yoyote bungeni kuhusu suala hilo hali ambayo imesababisha migongano kuendelea katika migodi mbalimbali kuhusu madai hayo hali ambayo kwa taarifa nilizozipata tarehe 1 na 2 Agosti 2012 inaweza kusababisha migomo migodini. Kufutwa kwa fao la kujitoa kumelalamikiwa pia na wafanyakazi na wadau wa hifadhi ya jamii katika Jimbo la Ubungo na katika taifa kwa ujumla.

Hata hivyo, suala hili na tukio husika litumike kama rejea ya bunge na wabunge kuikatalia Serikali kuwasilisha marekebisho yenye athari kubwa kipindi cha mwisho na hivyo wabunge kukosa fursa ya kupata maoni ya wananchi na pia Serikali itakiwe kuomba radhi kufuatia kulipotosha bunge kuwa wadau wa hifadhi ya jamii hususan wafanyakazi na vyama vyao walishirikishwa na kuridhia wakati ambapo wamejitokeza na kukanusha madai hayo yaliyotolewa na Wizara bungeni.

Kwa upande mwingine kufutwa kwa mafao ya kujitoa msingi wake haupo kwenye marekebisho ya sheria yaliyofanyika tarehe 13 Aprili 2012 pekee bali ni udhaifu katika mfumo mzima wa kisera na kisheria wa hifadhi ya jamii nchini hali ambayo inahitaji wadau kutaka mabadiliko makubwa.”

Tuendelee na mkutano.
John Mnyika

Anonymous said...

Mh.Mnyika unafany jambo jema sana na wafanyakazi wa sekta zote tuko nyuma yako na tunaunga mkono na kupongeza juhudi zako za kubadili hii sheria ya mifuko ya hifadhi ya jamii inayopiga marufuku fao la kujitoa(withdrawal benefit).

Kuna propaganda zinaendelea sasa kwamba ni muhimu wafanyakazi wakasubiri mpaka miaka ya kustaafu ili fedha hizo ziwasaidie kwani maisha ya uzeeni bila kipato ni mgumu sana.Kimsingi hoja hii inarembwa na maneno mazuri ya kuwajali wazee huku ikikaa kimya baadhi ya maeneo muhimu.

Mosi,watetezi wa hija hii hawasemi kuhusu maisha ya mfanyakazi baad ya kuacha au kuachishwa kazi miaka let say 20 kabla ya kufikisha miaka 55.Mtu huyu alikuwa anategemea kazi sasa hana na hapati kazi nyingine kwa sababu mbalimbali ukizingatia hali ya ajira nchini kwetu.Ni ukatili wa hali ya juu kumuweka mtu huyu kwenye mateso makali ya maisha eti kwa kisingizio cha kuujali uzee wake!Kama akikosa huduma muhimu huo uzee atafikaje kama sio kufariki ka njaa na presha ya mawazo?

Pili,watetezi wa hoja hii hawasemi kuhusu wazee waliotimza miaka hiyo ya kustaafu na wanapata shida sana kupata hizo fedha zao.Wengine walishawahi kuandamana na kukamatwa na polisi kwa sababu ya kudai mafao yao na wengine wamepoteza maisha kwenye michakato ya kufuatilia hizo fedha zao halali kabisa.Sasa iweje leo serikali ije na maneno ya huruma kwa wazee huku matendo yake kwa wazee wastaafu wa sasa yanadhihirisha ukatili wa hali ya juu?

Watetezi wa hoja hii ya kuwajali wazee hawasemi chochote kuhusu thamani ya fedha inavyopungua kwa kasi nchini.Kama mtu amefanya kazi miaka miaka 10 kwa wastani wa mshahara wa sh.300,000 kwa kipindi chote atachangia NSSF sh.30,000 kila mwezi na mwajiri pia liasi hikohiko na kufanya jumla ya sh.60,000 kwa mwezi.Miaka 10 ina miezi 120 kwa hiyo anakuwa ameweka jumla ya sh.mil 7.2.Kama alianza kazi akiwa na miaka 25 atakuwa ameachaau kuachishwa akiwa na miaka 35.Itambibi asubiri hadi miaka 20 mingine huku hela yake ikiwa vilevile fixed.Kuna tofauti kubwa sana ya thamani ya fedha hiyo kwa miaka hiyo ishirini.Mwaka 2000 mfano dola moja ilikuwa wastani wa Tsh.800 na sasa miaka 12 baadaye(sio 20) ni wastani wa sh.1800!Mil.7.2 mwaka 2000 ilikuwa dola 9000 na kiasi hiko cha pesa kwa sasa ni dola 4000!Hapo kwa miaka 12 tunaona fedha imeshuka thamani kwa asilimia 125% kwa kipima cha dola ya marekani.Ni vipi thamani ya hizo fadha kwa miaka 20?Hapo bado hujagusia mfumuko wa bei.

Sheria hii haifai na ni kandamizi.

jogi@jamiiforums.com said...

mh. John, Plan B iwekwe wazi,
ikiwa serikali ya ccm itakataa kuelewa matakwa ya wanachama wa mifuko ya jamii, wanachama waitishe mgomo wa siku mbili ili kupaza sauti zao.

Kwa kuwa ni kweli wanachama hawakushirikishwa angalau kupitia wawakilishi wao, basi sheria inakosa madate ya kutumika, the only option ni kufanya hayo marekebisho ya sheria. Wanachama wawe na haki za msingi juu ya michango yao, lakini hii mifuko badala kuwa mifuko, iwe bank ili wazo la kukopa liweze kuwanufaisha wanachama kwa uhalisia.

Hiyo itaifanya mifuko kuwa mbali na mikono ya wanasiasa walafi, itawawezesha wanachama kupata riba kutokana na michango yao kwa category ya fixied account hivyo kutunisha mafao ya mwanachama mmoja mmoja.

FRANK said...

MKUU MNYIKA,NIMESIKITIKA SANA KWA HILI,
NAOMBA NISEME MOJA,JE KUNA UTARATIBU GANI WE EITHER KU REVERSE HII SHERIA,NA JE IWAPO ITASHINDIKANA PLAN B NI IPI,KWA JINSI NAVYOONA NI NGUMU SERIKALI KU REVERSE SINCE IMESHAZITAFUNA HIZI HELA ZA HII MIFUKO NA SASA INATAPATAPA.PLEASE PLEASE PLEASE PLEASE,LET US ALL THINK OUT OF THE BOX KWAMBA IWAPO HATUTAFANIKIWA HAPA TUTAFANYAJE,MAANA NAONA KAMA KUNA DALILI YA KUSHINDWA HAPA,VINGINEVYO LABDA TUBADILISHE SERIKALI 2015.3 YRS SIO MBALI

Anonymous said...

Ilikuwaje ninyi wabunge mkaipitisha sheria hii kandamizi?

PAM said...

PIA SWALA LA KUSITISHWA KWA MAOMBI MAPYA WANATAKA KUTUAMBIA NN?KWAMBA PESA NDO ZILISHA PELEKWA WALIKOAMUA?AU WANAOFANYIA MIRADI WAMEGOMA KUREJESHA COZ PIA WANAWEZA KUGOMA KUREJESHA HASA UKIZINGATIA UDHAIFU ULIOPO NDANI YA SERIKALI NA PIA KATIKA UONGOZI WA MIFUKO HIYO,KWA KUONA KUNA WENGINE WENGI WALIOTANGULIA NA WALIKULA NYINGI ZAIDI SASA IWEJE WAO WALAZIMIKE KUREJESHA WAKATI NAO NI WADAU?............OK SERIKALI INATAKIWA KULIANGALIA SWALA HILI KWA MAPANA YAKE KWANI KUNA WATU WANAPELEKA MAOMBI YA KUPATA MAFAO SI KWA SABABU WAMEFIKISHA UMRI TU NA SI KWAKUWA WAMEAMUA KUACHA KAZI HAPANA NI KWA SABABU YA MATATIZO YANAYOWAKABILI ,,WAFANYAKAZI WENGI SANA KWA SASA WANAISHI KTK MAZINGIRA MAGUMU SANA NA WENGI WAMEPATA MARADHI WAKIWA MAKAZINI HIVYO WANAHITAJ KUPATA MALIPO HAYO ILI WAKAJITIBU KABLA MARADHI HAYAJAKOMAA,,WENGINE WALIPATA STRESS KUTOKANA NA KAZI WALIZOFANYA KWA KULIPWA UJIRA MDOGO,,HAWANA HATA MIRAD WANAYOIENDESHA KUTOKANA NA KAZI KUWA NGUMU,,HAWANA PESA ZA KUJIKIMU KIMAISHA ,,WATOTO HAWAENDI SHULE KWA KUKOSA ADA ,, SASA UTAMWAMBIAJE WAKATI MSHAHARA ANAOUPOKEA HAUKIDHI HATA 1/3 YA MAHITAJI YAKE?WABUNGE WETU NANYI MNACHANGIA KWA KIASI KIKUBWA KUTUANGAMIZA WANANCHI KWANI SWALA KAMA HILI WALA LISINGETAKIWA KUFIKA HAPA LILIPO,,MLIKUWA NA UWEZO WA KULISIMAMI KWA NGUVU ZOTE KWAN WENGI MNAJUA HALI HALISI YA MTAANI MAISHA YALIVYOKUWA MAGUMU ,,HII NI DHAMBI TENA DHAMBI YA MAUTI NI SAWA NA KUMNYIMA MTU HAKI YA KUISHI...WEWE NENDA KALISIMAMIE HILI KAMA UNAVYOSIMAMA NA MWISHO WA SIKU WATU WATAHUKUMIWA KWA UBINAFSI ,,NAUITA UBINAFSI KWA SABABU WENGINE SHIDA HAWAZIJUI NA WALA HAWATAKAA WAGUSWE NA SYSTEM HII,,

Anonymous said...

Mheshimiwa najukua nada ski hii kukushukuru sana kwa uzalendo na unmaking ktk kumquat ilia masala yanayo ikumba jamii ktk utumishi wako.

Kwanza Kabila niseme tu kwamba kwa namna Amira zilivyo ktk nchi yetu na uwezekano aw mtu kujiendeleza kimasomo,hili la SSSR limeongeza mzigo wa Mawazo vichwani mwa Watanzania Wendi ambao wanaguswa moja kwa moja au kwa utegemezi wa Mafao hayo.

Tulio wengi TZ tumeajiriwa kwa mikataba mifupi (ajira zisizo za kudumu,kwa mantiki hii michango yetu ya hifadhi ndio tegemeo letu la baadaye ya kusitisha au kuacha kazi.Fedha hiyo ni pamoja na Kuwait mitaji ya kaunzishia shughuli za kujiaajiri na kutengenza ajira kwa wengine maana huwezi fanya kazi peek y'all utahitaji wafanyakzi hiyo kupunguza kwa kiasi Fulani umasikini Kafka jamii.

Kama hiyo Hitoshi wengi Wetu ni vijana tulioanzisha familia ambao watoto watahitaji kusoma.angalizo! Ikiwa nitasubili mpaka miaka hiyo 55 unafikiri watoto nitsomeshaje na nchi yetu ajira ni yamkini.

Kwa Ustawi wa jamii ya TZ hili suala liangaliwe kw amapana zaidi ya maamuzi ya juu juu tu bila kutathimini athari kwa mapana.

Hitmisho! Mh.Mnyika,sula hili haiku alike na welengwa ktk sector Zote zisizo na mikataba ya kudumu ambao ndio wengi Wetu.

PAI said...

Hawa SSRA nadhani hawakutambua majukumu yao, wanapaswa wasimamie mifuko, na kuiamuru kutunza fedha zake zote katika Bank na si kuikopesha Serikali ambayo kiukweli ina madeni makubwa. pia inaonekana mifuko hii ya jamii ndo inayo endesha serikarikwani imekuwa ndo ikitumika kujenga vyuo na miladi mikubwa mikubwa nchi, HAPA WAFANYA KAZI HATYIELEWI SERIKARI , KODI TULIPE TENA NI KUBWA KULIKO HATA MICHANGO YETU NA FEDHA YETU YA MICHANGO WANATAKA WAICHUKUE?? KIUKWELI WAFANYAKAZI WENGI WA SEKTA BINAFSI NA HASA MIGODINI AJIRA ZAO HUWA HAZIELEWEKI, NA OFISI NYINGI ZA SERIKALI HUWA HAZUTUNZI TAKWIMU VIZURI. HEBU TUJIULIZE MASWA HAYA MACHACHE.
1.Nimeachishwa kazi nilikuwa ni Kuli katika kampuni frani na sina ujuzi wa kuniwezesha kuajiriwa kwingine kutokana na elimu yangu na ninategemea hiyo fedha ndo inisaidie kutafuta ujuzi mwingine kama vile kugharami a masomo ya udereva au ufundi seremala je nitakaa tu bila kazi ?
2: Nimeajiriwa na Kampuni ya nje ya nchi na kampuni imemaliza muda wake ( mkataba) na sina kazi je nini chakufanya? KUPIGA DEBE AU WIZI?
3. NIMEENDA KUFUATIRIA MAFAO YANGU NIKIWA NAUMRI WA MIAKA 55 NA NSSF WANANIAMBIA DOCUMENT ZANGU HAZIJAKAMILIKA VIZURI NA KAMPUNI NILIYO KUWA NAFANYIA KAZI NI YA NJE YA TANZANIA, NA ILISHA MALIZA MUDA WAKE WA KAZI HAPA, JE SERIKALI ITAKUWA TAYALI KUNIGHARIMIA SAFARI YA KWENDA NJE KUFUATIRIA NYALAKA ZANGU???
kWA KIFUPI SHERIA HII HAIFAI NA HATA HAWA SSRA HAWAFAI NIBORA WAKAFUTWA, HII MAMLAKA NASHAULI IFUTWE KWANI IMEANZA KAZI KWA KUKURUPUKA!

Adam Masalu said...

Kwa kweli serikali imeamua kujenga hofu kubwa na kali kwa wananchi, hasa wafanyakazi wa mashirika na makampuni binafsi, na mpaka sasa tunavyoongea hivi watu wengi wanaofanya kazi kwenye mashirika na makampuni binafsi wanaogopa kujiunga na mifuko ya hifadhi ya jamii (yaani NSSF na PPF).

Kwa kweli ukiangalia hali halisi, si watu wote wanaoacha kazi kwa mtu mmoja wataenda kufanya kazi kwa mwingine.. Yawezekana wengine wakahitaji kufungua miradi na biashara na huenda wakahitaji fao hilo la kujitoa kama mtaji wa kufanya biashara nyingine. Sasa serikali inapoamuru wafanyakazi hawa wapate fao hilo baada ya kustaafu, inategemea watatumia nini kuanzisha miradi wanayotaka (iwapo walitegemea fao hilo na hawakupata)? Inabidi serikali waliangalie hili kwa kuwa hii sasa imeshakuwa hofu kubwa sana kwa jamii, kiasi kwamba hata wale wasio katika mfumo wa ajira (system) wakiingia wataogopa mifuko yetu..

Anonymous said...

Nimesikitishwa sana na sheria kandamizi ambayo imepata baraka zote kutoka kwa serikali na baraka za Bunge. Najiuliza mara mbili au tatu sheria hizi zimepitishwa kwa manufaa ya nani ili hali sisi wenye akiba hatukushiriki? Swala la mshahara wangu ni langu na muajiri wangu wa kwanza na sidhani kama kuna chama kilikuja bargain mshahara ambao nahitajika kulipwa leo hii inakuwaje tuambiwe sheria ilipitishwa na baada ya consultation ya wadau wote?? walakini unaniingia hapo!
Hoja za NSSRA ni za msingi lakini hazina mashiko pale walipoleta hoja ya kujitoa katika umri wa miaka 55 au 60 kwa lazima ili wanajua hali halisi ya ajira zetu ni mwaka, miaka miwili, miaka mitatu miezi sita N.k leo hii unasema fedha hizi ninazodunduliza nichukue baada ya miaka 55 nadhani hata maana ya social security itakuwa hamna. kama baada ya mkataba wangu kuisha itanibidi nikaae na njaa ili hali nina mamillion ya fedha sema umri ni mdogo huu ni upuuzi ambao hauhitaji wala kuzungumzwa kwa watu wenye dhamana ya uhai wa taifa. Bado fedha hizo hazizingatii swala la value for money kwani kama leo nina million 70 baada ya miaka 30 ijayo itakuwa hiyo hiyo ili hali leo ningeweza kujenga na kufanya biashara yangu ndogo wakati huo kwa hii infation yawezakuwa itakuwa ni hela ya ya kusafiria kuja kuchukua cheque kama mzee wa EAC aliyeandikiwa cheque ya shilling 1000 ili hali ametumia zaidi ya elfu 20000.

NSSRA kuhusiana na mafao mnaweza kuifunza kutoka kwenye nchi nyingine ambazo wanataratibu za 1. kuwalipa wanachama mishahara kwa kuzingatia mshahara wa mwisho wa mwanachama kwa mwaka mmoja huku wakimuhamasisha kutafuta ajira nyingine. baada ya mwaka mwanachama huanza kulipwa nusu mshahara kwa miezi sita na baada ya hapo anakatiwa kabisa kwa ajili ya kusubiri uzee.
2. Mwanachama anaweza akapatiwa fedha za kujiendeleza kielimu pale anapohitaji kwani pia ni njia ya kuinua michango yake kwenye mfuko husika.
3.kumpatia mwanachama mkopo wenye riba ili hali mchango wake hauna riba ni wizi na unynganyi mkubwa kwani anajikopa hela yake na kulipa riba kwa jasho lakemwenyewe kwahiyo hoja ya mkopo wa nyumba haina mashiko labda isemekane bayana kwamba kuna makampuni yanayotaka kupora haki ya wafanyakazi kwa tenda za ujengaji wa majumba.
4. Kipindi cha miezi sita mlichoweka kwa ajili ya kusubiria miongozo ni kikubwa kwani watu wanataka kwenda shule na huwezi kuwaambia wenye vyuo wasubiri ada baada ya miezi sita.
5. Muda wa kusubiria mafao ndani ya miezi sita ni mkubwa tunataka iwe hata ndani ya miezi miwili au mitatu.
6.Fao la kusomeshwa kwa wanachama liwepo kwenye mafao ya shirika kama huduma ya afya.

kwasasa ni hayo tu

frank said...

naomba niseme tena.

Plan b ni muhimu,lakini bwana mnyika ,assume katika kipindi cha lets say niko na 30 yrs ,mpaka nafika 55 nitakuwa lets say nimefanya kazi kwenye mashirika labda kumi,ok.sasa hayo mafao kuyachukua utahitaji barua za kuajiriwa za kila kampuni ililowahi kufanya,utahitaji waajiri wote hao wakujazie zile forms za,na utahitaji wote hao,uwe na resignation acceptance kutoka kwao.kimsingi lazima uwe na file ambalo utakuwa unalifungia kwenye safe ili documents zote hizo ziwepo.then hapo bado hujakutana na ule usumbufu wa kawaida wa nssf .nakwambia watu watakuwa wanaziacha tu liwalo na liwe.mifano hai ipo mtu mpaka anakufa hajapata mafao yake anawaaacia watoto wafuatilie

Anonymous said...

Mara chache sana kusema kuhusu hii mifuko nikupe pongezi kwa kuthubutu kusema na kuwa na nia ya kutusema wafanyakazi mimi nasema swali langu je matumizi ya hela za mifuko kwa miradi mbali mbali ya serikali je miradi hii kweli inalingana na kiwango cha pesa kilichotelewa ama ndiyo vile unatoa pesa shilingi 100 zinafika kwenye miradi shs 30 na sabini zinapotelea kwengine tunachohitaji ni miradi yote iliyokuwa imechota pesa kutoka katika hii mifuko ichunguzwe kwa kina kutupatia kweli kilichotolewa na mashirika haya ndicho kilichokusudiwa pamoja na thamani zake tusishangae miradi hii imekuwa ni sehemu ya hii mifuko kufilisika na kushindwa kulipa wanachama mafao sasa wanataka kushikilia pesa zetu kwani wakijua time value of money kwao haipo katika usahihi

juhudi zinaonekana ila kufikia malengo yako Mh. Mnyika bado tunao watu wanataka ufalme wa watawala bila kukosolewa ndiyo taabu tulio nayo nakutikia kila jema katika hili

Anonymous said...

1. ''Life expectancy'' ya Mtanzania ni miaka 53, iweje mafao ya kujitoa yatolewe kwa umri wa miaka 55 au 60 ilhali uwezekano wa kuwa hai ni mdogo??
2. Isitoshe mafao yamekuwa yakitolewa kwa kusua sua mno, mtu anafuatilia mafao yake ya kujitoa kwa zaidi ya miezi sita, tatizo ni nini katika mifuko hii??
3. Katika sheria hii hapakuwa na ushirikishwaji wa wafanyakazi upande wa wafanyakazi kupitia vyama vyao. NSSF wanadai kuwa kulikuwepo mkutano wa wazi kwa wadau wote uliofanyika Dar es Salaam mwezi Februari. Swali la kujiuliza Dar es salaam ndio sehemu pekee yenye wafanyakazi hapa nchi wanaokatwa mishahara yao kwa ajili ya NSSF, PSPF, PPF na LAPF? Kwa nini hawakufika mikoa mingine kuchukua maoni ya wafanyakazi?
3. Kuna hoja inatolewa kuwa katika nchi za kusini mwa Afrika hakuna fao la kujitoa (withdrawal benefits) au kitu kama hicho. Hii si hoja kwa sababu kila nchi ina utaratibu wake na mazingira tofauti kwa wafanyakazi. Tanzania ni Tanzania na Afrika ksuini ni Afrika kusini. Tuamue kama Tanzania kwa ustawi wa wafanyakazi na watu wetu na kamwe tusiamue mambo ya umma bila kushirikisha umma eti tu kwa sababu nchi zingine wanafanya vile.

Mimi ni
"Peres Joshua Ntinginya"
Mining Engineer
Cell: 0767477180.

Anonymous said...

haingii akilini hata mara moja inakuwaje wafanyakazi wa migodini wao walipwe wafanyakazi wengine wasilipwe for whose interest shame on NSSRA such hypocrisy

Anonymous said...

MAONI YANGU

(i)Mamlaka ilitakiwa kupata maoni ya wafanyakazi kwanza kabla ya kuanza mchakato mzima wa kupitisha sheria hii (fao la kujitoa).

(ii)Thamani ya shilingi ya Tanzania inashuka siku hadi siku, kwa hivyo wafanyakazi hawaoni faida ya fedha zao kukaa muda mrefu kwenye mifuko bila kuongezeka huku wakijua thamani yake inashuka kwa kasi, na huku ajira yake ikiwa imeshakoma na hana kipato kingine tofauti na wafanyakazi wa Serikalini ambao pensheni yao hukokotolewa kutokana na mchango wake wa mwisho akiwa na umri huo wa miaka 55 au 60 hivyo thamani ya pesa inakuwa imezingatiwa.

(iii)Fao la elimu linalotolewa na PPF linatolewa kwa mwanachama baada ya kufariki tu, kwa hivyo wafanyakazi halina faida kwao.

(iv)Fao la matibabu kwa upande wa NSSF (SHIB) halitoi uhuru kwa mwanachama kuchagua hospitali, angalau kungekuwa na kadi ya kumuwezesha kuhudumiwa na hospitali yoyote, hii nayo kwa wafanyakazi sio faida.

(v)Wafanyakazi wa sekta binafsi, hasa migodini wana kawaida ya kuhama kutoka mgodi mmoja kwenda mwingine au wakifukuzwa, hivyo akisubiri huo umri wa miaka 55 hakutamsaidia kuwa na sifa ya kupata ‘pension’ kwa sababu hatakuwa na jumla ya michango 180 kama sheria inavyoeleza. Kwa hivyo wafanyakazi wanapendekeza kuwa waendelee kuchukua tu.

(vi)makampuni hufunga biashara na kwa kuwa ukomo wa ajira ya wafanyakazi utatokana na kufungwa kwa kampuni na kuna makampuni yanatoa ajira ya muda mfupi ambapo wengi wa wafanyakazi haitakuwa rahisi kwao kupata ajira mahali pengine, hivyo wafanyakazi waruhusiwe kuchukua mafao yao ya kujitoa ili yawasaidie kujiajiri.

(vii)Wafanyakazi hawana imani na kumbukumbu zilizopo kwenye mifuko, kwa mfano mwanachama wa NSSF akitaka kujua idadi ya michango yake, taarifa atakayoipata NSSF haitakidhi haja yake kwa sababu taarifa atakayopewa (statement) haitaonesha orodha ya michango tangu kuanza hadi kipindi cha kuomba taarifa hiyo. Badala yake taarifa itaonesha salio na miezi michache baada ya salio hilo. Hii italeta shida hususani kwa wafanyakazi waliopitia kampuni nyingi na zilishakufa.

(viii)Kutokana na mazingira ya kazi kiafya migodini na kadirio la umri wa kuishi la Mtanzania, wafanyakazi wanajua kabisa kuwa sio rahisi kufanya kazi migodini mpaka kufikia umri wa miaka 55 au 60.

(ix)SSRA inasimamia sheria za kimataifa za ILO ambako kuna mafao tisa (9) lakini kwa mifuko ya hifadhi ya jamii inatoa mafao pungufu, mfano NSSF inatoa mafao saba (7) tu, PPF matatu (3) tu, fao la kutokuwa na ajira (unemployment benefit) halimo, tulitegemea mamlaka ingesisitiza kukidhi viwango vya kimataifa kwanza kabla ya sheria hiyo (fao la kujitoa) kutumika. Lakini muhimu zaidi ni mazingira tofauti tofauti ya huduma za kijamii kati ya mataifa yaliyoendelea na taifa letu hivyo ni mhimu Tanzania ikaangalia mazingira yake kuliko kuiga mataifa mengine.

(x)Ni ajabu sheria iliyoanzia katikati ya mikataba ya wanachama pia kuwahusu wanachama ambao tayari walikuwa wanachama kabla ya sheria mpya!

(xi) SSRA wamekuwa wakitoa memos katika migodi tofauti tofauti wakidai kuwa wanachama watachukua mafao yao tofauti na tangazo lao la awali hivyo inaonekana kuna ubabaishaji katika hii sheria.

Ahsante
Jones

PAI said...

Hawa SSRA kama wanasimamia mifuko ya hifadhi ya jamii yenye lengo la kuhifadhi jamii basi wajue wapo nje ya malengo.
1. Nani kawafundisha kuwa jamii ni watu walio na miaka 55 na kuendelea? USHAURI KWA KILA 2% YA KODI NA SI YA MIFUKO SERIKARI NARUDIA ITOKE KWENYE KODI NA ITENGE IWE INAKWENDA KWENYE MFUKO WA WAZEE UANZISHWE MFUKO MPYA ,NSSF NA PPF SIO MIFUKO YA WAZEE NI MIFUKO YA HIFADHI YA JAMII, NA JAMII HAINA UKOMO WA UMRI.
2: SSRA wawe na fkira pana na zenye maendeleo na si kusimamia ubinafsi, Vijana wangapi hawana kazi? na je wakiwa na umri huo wa miaka 55 Serikali haiwajibiki kuwa tunza? na je itawatunza kwa kutimia mfuko upi wa hifadhi?
USHAURI SERIKARI IANZISHE MFUMO MPYA WA KUWATUNZA WAZEE NA HII ITOKANE NA KODI KWANI KILA MWANANCHI ANALIPA KODI IANZISHE MUFUKO WA WAZEE NA ITOE FEDHA KUTOKA KODI NA SI MIFUKO YA JAMII.
3. Hivi hii mifuko ya hifadha ya Jamii imekuwa VIKOBA AU SACCOS? Kwanini serikali ikope huko fedha? na kama inakopa inalipa riba kwa % ngapi? na mbona wanachama huwa hawalipwi fedhazao na riba??
SSRA ILIPASWA INAHAKIKISHE KUWA MIFUKO YA JAMII HAIIKOPESHI SERIKALI MOJA KWA MOJA KWA KUWA SERIKALI PIA NI MWAJIRI,BADALA YAKE MIFUKO IHIFADHI PESA BANK KWA RIBA NA SERIKARI IKOPE BANK.
4; Historia bado inatukumbusha kilio cha WAZEE WA JUMUIA YA AFRIKA MASHARIKI (East African Community )ILIYO PITA HAWA SERIKALI INGEKUWA INAONA MBALI INGEWATENDEA HAKI KWA KUWALIPA FEDHA ZAO LAKINI IKAWAPUUZA, je serikali inataka na sisi itufanye hivyo?
HATUKUBARI TUNAIPINGA HII SHERI MAPEMA NA TUKIWA NA NGUVU,HUU NI UTAPELI WA MCHANA NA HATUKUBARI, LIPA FEDHA KAMA HUNA HUZA VYUO ,UZA KILA ULICHO TUMIA KWA FEDHA ZETU NA ULEJESHE FEDHA ZETU.

Anonymous said...

Habari Mh JJM,
Tunaomba SSRA waondoe hyo sheria yao ya kuzuia fao la kujitoa,wakati tunachangia michango yetu ni wazi tulikua tunajua tutachukua mafao pindi tukiacha kazi,sheria imeanza kutumika july,hili twende sawa tunaomba michango yetu yote tuliochanga b4 july tupewe,then ndio tuingie kwenye huu mkataba mpya then iwe option(kujiunga au kutojiunga)
2.Sie kama wafanyakzi hatujashilikishwa kabisa chama chetu cha wafanyakazi TEWUTA hakijausishwa kabisa kwenye mchakato wa maoni au hata kama wameusishwa basi hawajatuambia chochote
3.Tunaomba serikali irudishe mjadala bungeni na waweke wazi hicho kipengele ili wabunge wadiscuss upya na sio kuficha hicho kipengele
4.SSRA wafute kauli yao ya kuzuia fao la kujitoa na kwanin miongozo ichelewe mda wa miezi 6 kwani wakati wanaandaa walikua hawajafanya research? Wafute kauli yao kwani ni batili

MathiasLyamunda said...

Mh. Mnyika kwanza nakupongeza kwa hatua hii. Maoni yangu ni kwamba mimi kama mfanyakazi wa sekta binafsi sijafurahishwa na mabadiliko ya sheria hii, mtu halazimika kuwa mwananchama wa NSSF au chama kingine chochote anapaswa kuachiwa uhuru wake wa kujitoa na kulipwa alichochangia ilu aende kuanzisha maisha yake mahala pengine, na mtu anaendeleaje kuwa mwanachama wa hii mifuko kama hachangii? Kwa ungumu maisha yaliyopo umri wa kustaafu ni miaka 55-60 je mtu akiacha kazi akiwa kijana wa miaka 30 anawezaje kusubiri mpaka miaka 55-60, anatawezaje kuanza maisha yake upya? Hii sheria haijashirikisha wadau wa hii mifuko maana tusingekubali sheria kandamizi kama hi.

Lakini pia Mh. Mnyika kuletwa kwa sheria kama hii kipindi hiki inatupa wasiwasi sisi wanachama wa hii mifuko kuwa kuna ufisadi umefanyika na hii mifuko imefilisika na haina hela za kuwalipa wafanyakazi au wanachama wake. Mimi napinga kwa nguvu zote sheria hii.

PAM said...

MCHANGIAJI ALIYETANGUALIA ANAONGELEA LIFE EXPECTANCY HII NI KWELI,,LAKINI KWANZA HEBU TUANGALIE NA KUJIULIZA NI WATU WANGAPI WANAOFANYA KAZI ZA KUAJIRIWA?NA WANAFANYA KWA MDA GANI?HAIJALISHI WANAFANYA KWA KUHAMA HAMA OR AJIRA YA MOJA KWA MOJA BALI TUANGALIE UWEZO WA MTU KUFANYA KAZI KAMA HANA MATATIZPO YOYOTE NI MIAKA MINGAPI?BAADA YA HAPO UNAUWEZO WA KUSEMA AU KUWEKA LIMIT KATIKA KUCHUKUA MAFAO KAMA KWELI UNANIA NA MAPENZI YA DHATI KWA WATZ ,,LAKINI KWA SABABU YA HALI HALISI YA KIMAISHA NA MFUMO MBOVU NA DHAIFU ULIOKO HILI LINAWEZA KUONEKANA KUWA JAMBO GUMU SANA KWA SASA ,,KWA WADAU NA SERIKALI KUKUBALIANA NA WANACHAMA WA MIFUKO HIYO PIA KUKUBALIANA NA MAONI YA WATU WENYE MAPENZI MEMA NA WATZ HASA WALALAHOI..MM MWITO WANGU HATA KAMA HAITAPEWA NAFASI YA KUJADILIWA KATIKA BUNGE NINGEOMBA WADAU NA WATZ WANAOPENDA NA KUJALI MASLAH YA TAIFA KUANDAA MKAKATI MADHUBUTI WA KULISHUGHULIKIA SWALA HILI K KWAN NJIA YA KUMSAIDIA MTU NA KUMWONDOA KWENYE MATATIZO HASA ANAPOSTAAFU SI KUMPATIA KIASI CHA PESA AMBAZO ALIZITUMIKIA WAKATI AKIWA NA NGUVU ZAKE,,KUNA NJIA NYINGI SANA ZA KUMSAIDIA MTU PINDI ANAPOMALIZA AU KUAMUA KUACHA KAZI ...TUUNGANE KWA PAMOJA WATZ

Anonymous said...

Kupanga ni kuchagua kwa hiyo akuna sababu ya kumlazimisha mtu namna ya kutumia pesa zake mwenyewe kwa hiyo mimi pia naungana na wafanyakazi wote wanaopinga sheria hii mpya ya FAO LA KUJITOA kwa sababu hata ayo mafao yanalipwa kila mwezi baada ya kustaafu uwezi kupata hadi uwe umechangia mara 180 (miaka 15) sasa kama mtu umebaatika kufanya kazi kwa miaka 12 alafu ukaacha/ukaachishwa kazi kwa sababu mbalimbali na ukashindwa kupata kazi tena hadi ukafikisha hiyo miaka 55 maana yake utakacho pata ni ile michango yako tu uliokua unachangia, hauta pata pensheni ya kila mwezi kwa sababu utakua aujakidhi vigezo vya kulipwa pensheni.

Kwa maoni yangu kama kweli nia ya SSRA ni kumsaidia mfanyakazi anufaiki na mifuko ya jamii watengeneze sheria zitakazo lazimisha hiyo mifuko ya jamii kuboresha mafao ya wanachama kabla na baada ya kustaafu ala wanachama wapewe hiari ya kuchagua maana kama nilivyoanza KUPANGA NI KUCHAGUA kwa hiyo mfanyakazi achague anachotaka.

MFANO
Mwanachama ambaye amechangia kiasi cha Sh. 2,500,000 (milioni 2.5) na kuendelea atapata mkopo wa kiwanja kilichopimwa,
Mwanachama ambaye amechangia kiasi cha Sh. 7,000,000 (milion 7) na kuendelea atapata mkopo wa nyumba ya mei nafuu.
Pia mwanachama aliyefikisha idadi fulani ya michango aruhusiwe kukopa nusu ya kiasi alicho changia
BY GILBERT BUGINGO

wambugani said...

JJ Mnyika ni jembe.

hawa watu wameanzisha hii SSRA kwa ajili ya kudhibiti mifuko ya jamii. kabla hata hawajaweza kudhibiti mifuko yenyewe, sasa wanaanza kudhibiti walalahoi.

halafu hii sheria inasemaje kuhusu expatriates? mimi nimefanya kazi na wajapani. wao wakimaliza mikataba yao wanachukua hela yote ya Nssf wanaenda zao, je na wao sasa watasubiri miaka 55?

Petro said...

Mh. Mnyika, kwanza nakupongeza sana kwa uamuzi wako wa kujali matatizo yetu wanainchi ambao tuko daraja la mwisho katika nchi ambayo ni daraja la tatu suala la kubadili sheria halikuzingatia mambo mengi ambayo watu wanataka kujua na yanawapa mashaka ya fedha zao. Maswali ambayo sheria hii haijajibu ni kamaifuatavyo,

1. Je ni lazima mtu aajiliwe katika formal sector baada ya ajira yake ya kwanza kuisha? Ukizingatia kuwa ajira nyingi ni contractual na pia focus kubwa ni kutaka watu wajiajiri? Think in a long run and not in a short run.

2. Kumekuwepo na utofauti wa mafao ya pension tofauti kwa mashirika yanayo operate ndani ya nchi moja, kwa maana ya calculation za pension na utoaji wa mkupuo wa kwanza na pension na baadae monthly pension, je hii huoni pia ni tatizo?

3. Formula ya pension ni kandamizi kwa mwanachama, kama wewe ni mtu unayejua angalau hesabu ndogo tu, je inaweza ingia akilini mwako kupata the little sum mwanachama anapata kama pension na angeweza kuwa na mifumo mingine ya kuhifadhi fedha yake ambayo angepata gawiwo mfn ya kunumua share za mashirika na kuwekeza katika amana mbalimbsli na mabenki pia, je umewahi tafuta tofauti ya ruturns za option zote hizo?


3. Mashirika yetu ya pension hasa yale giant kama NSSF, PPF, PSPF semeni ukweli! Yawezeka acturial valuation report zenu zinaonyesha mashirika kuelekea kushindwa kujiendesha kwa sababu mbali mbali ndiyo mana mmefanya lobbing kwa regulatory authority kuyanusuru mashirika yasishindwe kulipa wanachama wanaostaafu na kujitoa. Sababu ya report kuonyesha kushindwa kujiendesha ktk kulips mafao ni kama ifustavyo;
A. Mashirika yamewezeka katika miradi mikubwa ambayo payback period ni mda mrefu mfano wa uwekezaji UDOM, Daraja la Kigamboni, majengo makubwa, mradi wa kuzalisha na kufua umeme NSSF, etc, miradi hii haijaanza kuleta matunda kwa mashirika hivyo na changamoti. Hesabu walizopiga za returns from investment hazikuwa realistic due to poor investmement policy na pia udhaifu wa wataalamu katika mashirika, ndo maana sasa wanataka watu wasijitoe ili madhirika ya survive.

B. Changamoto ya mashirika mengi hasa ya madini kutaka kufungwa pia imeonekana italeta matatizo kwa mashirika yetu, kwa sababu makampuni ya madini kama kahama, buzwagi, Nzega, Geita etc wafanyakazi wake wanafedha zao nyingi katika mashirika haya, na life span ya mashirika haya haizidi miaka 5 ijayo, na average age ya watumishi katika mashirika ya madini inaweza kuwa 40 yrs, hivyo serikali inafanya maamuzi kuyakinga mashirika haya.

C. Mashirika yanakabiliwa na changamoto ya mortality rate, ambayo inafanya walipe fedha nyingi kwa watumishi wanafao fariki kwa warithi wao, hivyo they restrict other withdrawal to safeguard thier compnies.

D. Mashirika mengi ya pension yamekuwa yanalaumiwa sana kwa matumizi mabaya ya fedha za wanachama, katika ufisadi katika manunuzi, wizi wa fedha, pia kukopesha au kutoa ruzuku kwa vyama vya siasa. Wote tutakuwa shahidi kuna nyuzi ngapi hapa JF za mismanagement ya fedha PPF ambazo tumeletewa? Hii yote ndo inafanya pension iwe ndogo na ifanye watu kytokuwa na hamu ya kusubiri hiyo pension ndogoo na tena baada ya miaka 55!

Mwisho napenda kuyashauri mashirika ya pension waache hii lobbying waliofanya mana itaua wazee wetu wengi, mpaka mda huu tu wastaafu wengi wanakufa sababu ya pension kwa sababu anachosubiri katika miaka 55 siyo anachopata, hivyo pressure due demand ya maisha inamuua. Pia kwa nini kama hii miradi inajengwa kwa fedha za wanachama mwisho wa siku zusitolewe share za kuimiriki hiyo miradi kwa wanachama, nadhani hii itawafanya watu wasiwaze kutoka maana watakuwa ni sehemu ya umiliki wa miradi na mashirika kwa ujumla

Anonymous said...

HIyo hoja ya kuboresha maslahi kwa mwajiriwa pale atapostaafu haiana mashiko kwa nini mwajiriwa saiwe huru ili kama ataamua kuchukua pesa yake pale atapoamua kuacha kazi? Lakini pia hatuwezi kubururzwa as if ni wafungwa eti watupangie hata jinsi ya kutumia pesa ambazo ni jasho letu hii haiwezekani ni njia moja ya utapeli kwa wafanya kazi ambayo haya mashirika yamebuni na serikari inaharisha ikijua wazi ni wizi wa wazi wazi kwani si lazima ufanye kazi hiyo miaka 55-60 kustaafu.

HUU NI WIZI KAMA WIZI AINA NYINGINE

Anonymous said...

Hilary mapula. Wa geita gold mine. Maoni yangu. Hii sheria hautufai sie wafanyakazi wa migodini kwa sababu. Urinzi wa kazi hakuna mtu anafukuzwa kazi hovyo so ukituambia miaka 55 ni uonevu wa wazi wazi. Kingini kazi,za migodini ni ngumu hivyo hakuna mtu anaeweza vumilia mika 15 wanayodai ndio unaingia kwenye mfumo wa pensheni so wengi hufanya miezi,or,miaka kazaa na kuacha. Kingine hata ukistafu unapewa robo ya michango hafu unapewa 80% ya mshaara ulioacha nao kazi. Hebu fikiria mtu,kafanya miaka hii,aje achukua pesa itakuwa haina thamani kabisa. Na hii sheria inamapungufu mengi,ikiwa hata mtu ukifa mkeo kupewa mpaka awe,ni miaka 35. Mtoto,awe chini ya miaka 18. Huu si ni wizi. Sie hatuitaki hii sheria yote.. Na hata mkurugenzi wa SSRA hatumtaki pia kwani,kadanganya kwa umma ya kuwa kashirikisha wadau wakati sivyo

abiud said...

nakuunga mkono sana mkubwa

John Mnyika said...

Ndugu wafanyakazi na wadau wa Hifadhi ya Jamii:

Asanteni sana kwa wote mliotoa maoni mpaka sasa. Nilitangaza kuwa mkutano wetu utakuwa saa 7 mchana mpaka saa 9 alasiri ambayo tayari imeshafika. Nimepitia michango ambayo imetolewa mpaka sasa na maoni ambayo yametolewa ni pamoja na:

Marekebisho ya sheria yaweke uhuru na hiyari ya mwanachama kupewa mafao yake ya kujitoa ama sivyo basi katika kipindi ambacho hana ajira au kuwepo na mafao ya kutokuwa na ajira; kwa kuhakikisha kuwa mafao yote tisa yanatolewa kwa mujibu wa mikataba ya Shirika la Kazi duniani.

Marekebisho yafanyike kuwezesha sheria kuwawekea mipaka wanachama wapya na si wanachama ambao walishajiunga kabla kwa ambao walikuwa na matarajio kuwa wanayo hiyari ya kuchukua fao la kujitoa.

Marekebisho ya Sheria yahakikishe ulinzi wa kutosha wa fedha za wanachama katika masuala ya uwekezaji na kuhakikisha wanachama wananufaika vya kutosha kutokana na uwekezaji unaotokana na fedha zao.

Hakukuwa na uwazi na ushirikishwaji wa wanachama pamoja na maelezo yaliyotolewa kuwa NSSF iliitisha mkutano mwezi Februari Mkoani Dar es salaam kwa ajili ya wanachama wake, wafanyakazi na wananchi kwa ujumla katika kufanyika kwa marekebisho husika hivyo mchakato wa marekebisho ya sheria unapaswa kurejewa kwa kuwashirikisha kikamilifu wadau husika.

Marekebisho ya sheria yaweze kuweka mfumo ambapo baadhi ya kada kutokana zinaweza kuruhusiwa kuwa na mafao ya kujitoa kutokana na aina ya kazi za sekta husika mathalani migodini.

Marekebisho ya sheria yaweze kutatua utata uliopo baina ya umri wa kuishi wa hapa nchini (life expectancy) na umri wa kustaafu, kwa kadiri ya maoni yaliyotolewa ni kwamba umri wa kustaafu uko juu ya wastani wa umri wa kuishi.

Marekebisho ya Sheria yatambue kuwa ajira kwenye sekta binafsi kwa sehemu kubwa ni za mikataba ya muda mfupi sio za kudumu na pia hakuna uhakika wa kazi (job security), hivyo mfumo wa mafao ni muhimu uendane na hali ya ujira na ajira nchini.

Ukichambua maoni hayo na mengine, inaonekana bado kuna maoni yanayokinzana na mengine yanayohitaji kupatiwa maelezo na vielelezo vya ziada. Aidha, kuna masuala ambayo bado mpaka sasa hayajatolewa maoni katika ya maeneo niliyopendekeza kuwa yajadiliwe.

Hivyo, naongeza muda wa mkutano na naendelea kupokea maoni mpaka saa 11 jioni.
John Mnyika (Mb)

BINEMUNGU said...

Upungufu wa sheria:
1.WAFANYAKAZI SEKTA BINAFSI ITATUUMIZA MAANA SECURITY YA KAZI HAMNA
2.SHERIA HAIMSAIDII MTU YEYOTE AMBAYE ATAPATA ULEMAVU AU MAGONJWA MAKALI AMBAYO YATAMLAZIMISHA AACHE KUFANYA KAZI . ANGEPATA HELA YAKE ANGEJITIBU AU KUANZISHA MRADI WA KUMPATIA MATIBABU AU KUMSAIDIA KWENYE ULEMAVU WAKE .HUWEZI KUSUBIRI HUKU UNAUMWA MPAKA MIAKA HIYO 55.
3.ITADIDIMIZA SEKTA YA UTAFITI MAANA KAZI HIZO NI ZA HATARI SANA.
MFANO,UTAFITI WA WANYAMAPORI, MAGONJWA,SAYANSI,TIBA,CHANJO,DAWA,NA ITADUMAZA WANAFUNZI KUSOMA MASOMO YA SAYANSI.
4.SEKTA YA MICHEZO ITAKUFA MAANA WENGI UMRI WAO WA KIMICHEZO UISHIA MIAKA 33. MFANO NI MCHEZO WA MPIRA WA MIGUU
4.THAMANI YA HELA YETU NI NDONGO HATA HIVYO MTU AKIWEKEZA TSHS.5000 AKIWA ANA UMRI WA MIAKA 25 ATACHUKUA HIYO HIYO KWA TAHAMANI YA FEDHA HIYO MIAKA 30 BAADAYE ,MFANO NI MZEE ALIYEPEWA TSHS 300 KAMA MAFAO YAKE BAADA YA KUTUMIKIA NCHI HII KWA MDA WA MIAKA 10.

ENG.BINEMUNGU D.CHITAMBIKWA
KAISHO KYERWA

Anonymous said...

Ndo maana katika maoni ya katiba nimependekeza pension itolewe kwa awamu ya kila miaka kumi.Huu ni utaratibu mbovu na isitoshe sisi wanachama ambao ni wadau wakuu hatujahusishwa.Kama vipi tusikatwe hayo mambo,maana hayana faida tena kwetu

Anonymous said...

Mh Mbunge wangu, Naomba utupe mwaliko wako tuje dodoma, kwa magari tutakayo yakodi sisi wenyewe ili wajue ni kwa jinsi gani tuko serious na huu ukanzunzu wao, all workers of Tanzania Lets go to Dodoma.

MALINYI TWENDE PAMOJA said...

WAFANYAKAZI WA UDSM -UCC NI WAHANGA WA HII SHERIA KWA SABABU SISI NI WAAJIRIWA WA 3 YRS CONTRACT,TUNA MKATABA NA PPF KUWA MKATABA UKIISHA UNACHUKUA CHAKO NA NDIO MAANA TUNAKATWA 10% NA MWAJIRI 10% KAMA NSSF. TUNA WAAJIRIWA 200 HAPA AMBAO HATUTEGEMEI RUZUKU YA SERIKALI BALI REVENUE YA BIASHARA YA USHINDANI KTK ICT INDUSTRY.

MIMI NIKIPOTEZA AJIRA YANGU HAPA SINA PA KWENDA SASA TEGEMEO PEKEE NI PPF YANGU. MH. MNYIKA MZINGATIE KUWA SISI TULIINGIA KTK MFUMO HUU KWA KIGEZO CHA MIKATABA, TUKAACHANA NA GRATUITY ILIYOTUMIKA MPAKA 2002 OCTOBER. HUU NI UONEVU MKUBWA KWA WANA UCC.

Anonymous said...

Kuna mambo ya kuweka sawa pia maana kuna watu wanasema eti ni kwa nini tutegemee hiyo 10% baada ya kazi kukoma. Nitatoa mfano wa kodi ninazokatwa direct katika mshahara ili watu wajue ni jinsi gani hiyo 10% ni mhimu. Mimi mshahara wangu ni zaidi ya 700,000.00 na hivyo makato ni kama ifuatavyo ~35%PAY, 10%NSSF, 8%LOAN BOARD. Totalni kama 53%. Sasa nabakiwa na kama 47% kulipa VAT na kuhudumia familia na wadogo zangu. Je, utasave nini hapo kwa ajira fupi ya 4 years!

Anonymous said...

Marekebisho ya sheria yaweze kuweka mfumo ambapo baadhi ya kada kutokana zinaweza kuruhusiwa kuwa na mafao ya kujitoa kutokana na aina ya kazi za sekta husika mathalani migodini.

Kwahii hoja kama inaukakasi ambayo mheshimiwa umeichukua nadhani kama ina ukakasi kidogo kwani inatutenga Kada zote ziwe zinaweza kutoa fedha zao kwani wote ni wanchama haki sawa nasio vinginevyo

PAI said...

Serikali inajua wazi kuwa swala ajiri ni tata, haina uwezo wa kuwaajiri vija wote.
Kijana hufanya kazi kwa malengo katika kampuni binafsi na baada ya muda huacha nafasi kwa ajiri ya watu wengine, yeye huenda kuchukua mafao yake na kujiajiri, katika kujiajiri kwake huajiri pia watu zaidi wasio kuwa na ajira,
Mfano:
1; KIJANA MWENYE UMRI WA MIAKA 36 ALIKUWA NAFANYA KAZI AKAAMUA KUACHA KAZI NA KUCHUKUA FEDHA YAKE, KAJENGA HOTERI PALE ATATOA AJIRA, KANUNUA NYAVU ZA KUVULIA SAMAKI HAPO KATOA AJIRA, KANUNUA BASI HAPO KATOA AJIRA, KANUNUA PIKI PIKI HAPO KATOA AJIRA N.K ,
SWALI,
1.Je akikaka miaka 19 BILA KAZI hali yake kimaisha itakuwaje??
2. Je baada ya miaka 19 ndo atatimiza miaka 55, fedha itakuwa na thamani ya kuanzisha miradi yake ya kukuza kipato chake na kuajiri WATANZANIA WENZAKE??
3. Baada ya miaka 55 atakuwa na uwezo wa kujishughurisha na miradi ya maendeleo has kazi zinazo hitaji nguvu??
4. Serikali na aliye peleka mswaada huu bungeni anafikili kwa upana na uelewa wa elimu yake au kasukumwa na ubinafsi na kwa masirahi ya wachache?
5.SSRA ipo kwa ajiri ya kutetea wafanya kazi au kutetea SERIKALI?
6. Je kwa kuwa wafanya kazi HAWANA IMANI TENA NA SSRA JE UNAWEZA KUTUSAIDIA KUPELEKA PIA HOJA MPYA KWA BAADA BUNGENI YA KUOMBA HII MAMLAKA IVUNJWE NA TUUNDE SHIRIKISHO LA MIFUKO YA HIFADHI YA JAMII AMBALO HALITAKUWA NA UHUSIANO NA MWAJIRI AMBAYE NI SERIKALI?

Mr PAI

Anonymous said...

mh Wabunge wao baada ya miaka mitano sheria inasemaje na kodi zao vipi wanalipa PAYE na NSSF wanaweka au inakuwaje kwani mkataba wangu ni wa mwaka na nalipa yote hii imekaaje???

John Mnyika said...

Mtoa maoni 5:32, sijachukua msimamo bado; bali nimeweka kwa muktasari maoni yaliyojitokeza kwa wingi. Nashukuru umetoa maoni mbadala.

Nitashukuru pia wenye maoni kwamba vilifungu vilivyokuwepo kwenye sheria zetu kabla ya tarehe 13 Aprili 2012 na vile vilivyoongezwa tarehe hiyo kwa lengo la kudhibiti mafao ya kujitoa kwamba vibaki kama vilivyo kwa kile kinachoelezwa kuwa ni kutimiza madhumuni ya Hifadhi ya Jamii ambayo ni kuhakikisha kuwa Mwanachama anapostaafu anapata mafao bora yatayomwezesha kumudu hali ya maisha uzeeni, wajitokeze pia na kutoa maoni ya kupinga kufanyika kwa marekebisho na kutoa sababu.

Aidha, wenye kutaka kwamba kwenye penseni ya lazima ya uzeeni liondolewe lakini kuwepo na mafao ya nyongeza ambayo ndiyo yatakayokuwa na hiyari ya kujitoa nao watoe maoni na kufanya uchambuzi wao.

Kutokana na maoni mbalimbali ndipo tutaweza kupata ni marekebisho ya aina gani yanastahili kufanyika katika sheria kuhusu fao la kujitoa kwa ajili ya maslahi ya mfanyakazi kabla ya kufikia umri wa kustaafu lakini wakati huo huo kuweka mfumo wa hatma bora ya mfanyakazi baada ya kustaafu.

John Mnyika (Mb)

Unknown said...

kazi kweli kweli, these guys should have set aside mafungu kwa ajili ya kuongezea mafao ya wafanyakazi sector binafsi ili kwamba kama mtu atastaafu katika umri huo basi at least ale pension yake kama wafanyakazi ya serikali, i mean kama mwajiri anachangia 10% mwajiriwa 10% na serikali ichangie walau 2% kwa ajili ya wale watakao weza/chagua kusubiria iyo 55 age limit. apo ingelikuwa kweli ya kwamba wanataka kuboresha maisha ya wazee. sasa pesa zangu zooote wananipangi matumizi.

Anonymous said...

TUNGIBWAGA KILILI,
Maoni yangu ni kuwa huu utaratibu sio kabisa ni uonevu tena haifa kabisa serikali kudicteki haki za wafanyakazi.Maoni yangu ni kuwa utaratibu uliopo ndo mzuri,yaani muda nikiacha kazi ni vema nipewe changu soon as possible.Asante mnyika kwa kazi yako njema

Anonymous said...

FAO LA ELIMU KWA MUAJIRIWA LIWEPO VIJANA WENGI WANTAKA KUSOMA DEGREE, MASTERS, POHD ILA HAWANA HELA HIVYO HAYO NDIO MAMBO YA KUYAWEKA SIO MASWALA YA HELA YA MAZISHI

Anonymous said...

RWENYAGIRA(M4C)

IFIKE MAHALA SERIKALI YA TANZANIA IWE INAFIKIRIA KUWA WAFANYAKAZI KATIKA SECTA BINAFSI WANATEGEMEA ZAIDI MAFAO YA HIFADHI YA JAMII KULIKO HATA HIYO MISHARAHARA.MATHALANI KAMPUNI UNAYOIFANYIA KAZI INAPOFIRISIKA,JE HAWA WAFANYAKAZI WATAISHI VIPIWAKATI UWEZEKANO WA KUPATA AJIRA KWA SASA NI SAWA NA NGAMIA KUPITA KWENYE TUNDU LA SINDANO?EE MUUNGU MWENYE SHIBE HAMJUI MWENYE NJAA.

Anonymous said...

Asante Mh. Mnyika kwa kujitolea kuwatetea Watanzania.

Kwanza TUCTA imelala sana, pia Vyama vya wafanyakazi katika sekta Binafsi haviko huru.

TUCTA imeshindwa kutetea Mishahara mipya iliyotangazwa na Serikali.

Serikali yenyewe imetiwa mfukoni na mafisadi, sote tunajua kuwa makampuni binafsi yanachangia Si.cm
fedha za kununua tshirt na kofia za kijani ili kuwalaghai Watanzania.

Mafao ndo ilikuwa kimbilio la wanyonge, ajira sekta binafsi haziaminiki.

Huendi serikali ama Spika wakamkwamisha Mnyika,je Tufanyeje?

Turudi tena hapa na tuweke mikakati ya maandamano na migomo.

Thanks Mnyika.

Anonymous said...

Mheshimiwa Mnyika,

Narejea nikiwa na shukrani kwa majibu na maelezo yako ya kina pale nilipouliza "mlikuwa wapi, wote"? juu ya kilichotokea.

Serikali, badala ya kutumia vyema dhamana tuliyowapa kuwaza na kupanga mikakati ya kutuendeleza...sasa wanatumia akili, ujuzi na kodi zetu kupanga mbinu chafu za mlango wa nyuma kupitisha udhalimu na wizi wa mchana katika masuala nyeti kama haya.

Inasikitisha. Inakera. Inauma.

Ni dhuluma mbaya kabisa kwani kodi tunalipa na fedha hizo ni mali yangu, yetu, halali.Hiyo hali ya kuwatumia wafanyakazi hewa sijui Stamico kutuwakikisha ni hila mbaya kuwahi tekelezwa. Kama hao wa madini waliridhia basi ni uamuzi wao, wengi hatukushirikishwa. Ni wazi kwamba binafsi na wachangiaji wengine humu karibu wote hatujaridhia.

Mfumo wa pensheni uwe kama benki (yawezekana huu si mfano murua). Umtambue mteja mmoja mmoja kwa nafsi na uchangiaji wake. Kama mteja, mimi niwe na mamlaka na maamuzi juu ya mafao yangu ikiwamo kujitoa.

Swali la mwisho Mheshimiwa, kwa maelezo ya Naibu Spika kuhusu mwongozo ulioomba juu suala hili, na marekebisho ya ratiba za shughuli za bunge, ni kama "wameshajipanga kukwamisha" kujadili haya.

Tafsiri yangu ni kwamba "wameamua liwalo na liwe", lazima wazuie uchukuaji wa mafao toka kwa wanachama. Wasiwasi wangu ni kwamba mifuko haina fedha kabisa.. na tujiandae na maumivu makubwa kama ya Wazee wa Afrika Mashariki"

Plan B ni huo ukusanyaji wa sahihi toka kwa wabunge kuunga mkono mswada binafsi.

Sasa swali, what is plan C?

Tuko pamoja na nakutakia mafanikio katika hili na mengi unayoyasimamia. Nawaonea wivu wana Ubungo, kweli wana mwakilishi wa kweli, anayewapigania wao, na sisi wengine!

Stay Blessed.

Emanuel Kabaka said...

Jina langu: Emmanuel Kabaka.
Nafanya kazi: AEL Mining Services.
Naomba nitoe mchango wa mawazo yangu kuhusu Zuio la fao la kujitoa.MABADILIKO YA SHERIA HII HAYAFAI NA INATAKIWA IBADILISHWE NA KUFANYA KAZI KAMA ILIVYOKUWA HAPO AWALI.
Kwa uwezo mdogo wa Serikali kuajiri ni wazi kwamba watanzania wachache wenye uwezo wa kufanya kazi wako kazini na wengi wanaotoka hasa kwa kufukuzwa au kwa ukomo wa ajira za muda mfupi hawawezi kabisa kupata kazi tena.
Fikiria mtu anaacha kazi miaka 25 ni wazi kwamba ataathirika na maisha yake yote wakati anahela zilizokaa bila ya kazi ambazo angeweza kuzifanyia japo biashara akaweza kutimiza mahitaji mengine kama:
1.KUSOMESHA WATOTO (kwangu mimi hii ndiyo hela yangu ya Uzeeni) kuliko kusubiri nisomeshe watotowakiwa miaka 30 wakati huo nitakapokuwa na miaka 55/60.
2. Kujenga nyumba badala ya kusubiri kujenga uzeeni amabapo thamani ya hela itakuwa ni tofauti kabisa ukilinganisha na wakati huu.(Watanzania wote hata amabaye hakusoma anajua thamani ya hela yetu inavyoporomoka kila kitu.
3. Si kila sheria ianayofanyakazi nchi nyingine ni nzuri kwa nchi nyingine.
Mfano mbona Sheria ya ushoga mbona haijapitishwa, na mbona sheria ya unemloyment befit haijapitishwa???
4.Naamini hela ninayokatwa kwenye mifuko ya jamii ni mali yangu na mwajiri wangu (hasa mimi niliye private sector) ambapo Serikali haichangii kitu chochote. Ningependa kusikia kama Serikali inatujari na kufikiria maisha ya Useeni basi TUNGGECHUKUA HELA ZETU KILA MIAKA ANGALAU 5 KAMA SI 1)ili kuzifanyia kazi ktk hii nchi yenye hela zishukazo thamani kila kuchapo.
Naomba kuwasilisha.

Anonymous said...

(a) Mafao bora uzeeni: Kuna aina mbili za wanaochangia(i) wafanyakazi wa serikali ambao kikomo chao cha kazi ni miaka hiyo ya 55 -60.kwa hili linawafaa wao kwa sababu ya job security waliokuwa nayo(ii) wafanyakazi kampuni binafsi - huku ndo NSSF wanakochangia wengi.Kundi hili ndo linalolalamikia sana sheria hii ya kishetani. HApa utakuta mwajiri akafukuza mfanyakazi bila sababu au kwa matakwa yake, redundancy, kufirisika kibiashara na kufunga biashara yake na waajiriwa kutokuwa na kazi, kuacha kazi kwa hiari ya mfanyakazi either kutokana na mazingira ya kazi, sababu za kiafya, maslahi duni, kutaka kufanya shughuli binafsi na hiyo mafao yake kuwa sehemu ya mtaji.

Serikali kutaka kuyafanya haya mafao kuwa ya uzeeni ni kukwepa jukumu lake la kuwatumikia wananchi wake kwa kuwahudumia wazee wake. Hawa wazee walilipa kodi zao mbalimbali ikiwemo PAYE na SDL wakiwa vijana.

(b) ushirikishwaji- Kwa miaka mingi mashirika haya yamekuwa vitengo vya kula pesa za wanaoitwa wanachama. kwa hakika iundwe organisation ya wanachama ili kutoa mawazo huru na sio huu ukichaa. itamkwe kuwa kampuni yoyote TAnzania itakayoanzishwa ni lazima wafanyakazi wake wawewanachama wa vyama hivi vya wafanyakazi ili kuwe na msukumo mpya juu ya dhuluma hizi. Leo hii tunadhulumiwa kwa sababu ya divide and rule ya serikali kwa sababu hatuko wamoja kama wafanyakazi. Ofisi zingine ukitaka kujiunga na vyama hivi vya wafanyakazi wewe ni victim.
Hata hivyo hakukuwa na ushirikishwaji wa hoja hii ya miaka 55 au 60 kwa kuwa jamii nzima inapinga utapeli huu. Kama bungeni hasard za bunge hazionyeshi kuwapo kwa kipengele cha umri wa miaka 55 je, wao walikipata wapi?? Tusiposhinda hapa yale yale ya WAZEE WA AFRICA MASHARIKI YATATUPATA pindi uzee wetu utakapofikia. Tupinge dhuluma/utapeli hii kwa nguvu zote.

(c) Mchakato kuendelea: Kulikuwa na ulazima gani wa kusaini na kuanza kutumia huu utapeli wao kama miongozo haiko tayari. Maanake kunakitu kibaya tayari kiko shingoni mwetu wafanyakazi. Kosa kubwa mashirika haya kuingia ni lazima na kutoka sio hiari hata kabla ya sheria hii. Pia kosa lingine wakurigenzi wa haya mashirika ni wateule wa rais na ni makada wa chama tawala. Pesa zimetumika vibaya kwa projects za kisiasa na hivyo tatizo linajaribu kusogezwa mbele.

(d) Kusitisha maombo mapya ya kujitoa:- HAina mantiki kwa kuwa hii sio pesa yao; ni pesa tuliyokatwa tokana na jasho letu la kila siku na waajiri kutuchangia kwa hiari yao. Ikumbukwe pia kuwa waajiriwa hawana mahala wanapoweza kukwepa kodi (PAYE), Ambayo nayo iko juu sana. Wanacholipa serikalini kinawatosha wao serikali na waajiriwa wakiishia kulipa riba kubwa kwenye mabenki ili japo wajikongoje katika maisha ili kulipia ada za shule zao wenyewe, watoto wao, nyumba na n.k. wafanyakazi wamekuwa wakikamuliwa kwa kodi hii ya PAYE. kampuni wao hutoa expense zote na mwisho ndo 35% of the net profit hufuata lakini waajiriwa hutoa tu 20% ya NSSF bila %age fulani ya chakula na maji.

pendekezo: serikali iangalie wafanyakazi wake kwa kutoa NSSF(20%)+ chakula na maji(10%) na kinachobakia ndo kikatwe kodi. Hii itaimarisha afya za wafanyakazi kuliko hii tanthilia ya kulamba na mafao yetu huku tathmini ya mtanzania kuishi ikiwa miaka 50.

Mwisho: serikali ya kikwete na ccm imeshindwa kukopesha nje na ndani sasa isichezee mafao yetu. Ni hiari yetu wenyewe na ni haki yetu wenyewe sio mali ya serikali. Serikali ( NSSF) ichezee riba ambazo wamekuwa wakikopesha mabenki na taasisi zingine na fedha ikiwemo banki kuu KULIKO KUTAMANI HAKI YETU AMBAYO HUIPATA IKIWA IMEATHIRIWA NA INFLATION RATE BILA WAO NSSF kuongeza chochote.

Anonymous said...

Mimi naitwa Josephat Simon ni muajiriwa wa Benk hapa Dsm, mimi napingana na sheria hii manake haina mantiki yoyote kutusaidia hasa kama mimi wamesema kwenye hiyo sheria kuwa watanikopesha kujenga nyumba na inakuwaje kama nyumba nimeshajenga! Na kwa mfano hivi karibuni moja ya Bank moja kubwa imepunguza watu zaidi ya 100 sasa hawa wote wasubiri mpaka miaka 55 kupata pesa zao hiyo si haki kabisa na kwa mfano baada ya kufanya kazi kwa miaka minne ninaamua kutaka kujiunga na masomo ya masters katika vyuo vyetu hapa mfano niamue kujiunga masters Mzumbe na ninaacha kazi ninachukua pension yangu najiunga na masters sasa kama pesa ndo mpaka miaka 55 ntajiendelezaje kielimu na hakuna mikopo ya masters? Hii sheria haina haki na kama mfanyakazi ninapinga hili swala na tunaomba libatilishwr kabisa sheria hii haimsaidii mtu yeyote zaidi ya mashirika ya hifdhi

Arphaxad Seleman said...

Naomba kuchangia kama ulivyo elekeza:
1.Jibu ni hapana kwa hali halisi ya maisha ya mtanzania tunahitaji kusomesha watoto,kujenga nyumba bora na kuishi kulingana na samani ya shilingi,
2.Maoni yale hayakuhusisha wadau ndio maana wadau wote wanalalamika kuhusiana na sheria hii kandamizi ss sio wendawazimu
3.kuhusu miongozo ss hatuijuwi wanatakiwa waruhusu fedha zetu wenye nazo wachukuwe ndio miongozo itafata kama inatija tutajuwa baadaye
4.Ni vizuri watu wapewe hela zao maana walisha acha kazi sasa mambo ya miezi sita ni ya nn?
5.Ss maoni yetu hili swala ni la dharula sana kuliko wanavyofikiri hawa ndiyoooooo tafadhari sana hoja hii ipewe kipa umbele,
Naomba kuwakilisha

Anonymous said...

Mimi nilidhani lengo la hii mifuko ni kuboresha maisha ya sasa na ya baadaye kwa wafanyakazi. Hata ILO sheria zake ziko wazi kuwa mwanachama atanufaika na akiba yake pindi tu kipato chake kinapokoma.

kagambo said...

Kwa nini serikali imeamua kuanzisha wakala wa kuwaua watanzania. Zamani hakukua na TAKUKURU,EWURA, SUMATRA na hata vyombo vingine vya usimamizi. Tulikua tukiona watu wanakamatwa kwa rushwa,vyombo vya usafiri vilikua havipati ajali mara kwa mara,vilidhibitiwa. Bei ya Nishati ilidhibitiwa. Sasa tuna mamlaka kibao za usimamizi lakini matatizo ndio yanaongezeka. SSRA ni mamlaka ya kusimamia mafisadi na sio mifuko ya jamii kwani haikua na matatizo na ndio maana serikali imekua ikikopa fedha na kufanyia miradi mbalimbali. Walikuja kazini kwetu na kutudanganya kama watoto wakijitambulisha kuwa wawakilishi wa serikali. Wkakiri kuwa sheria imesainiwa na wao wanakusanya maoni tu ili wakaunde kanuni, na wakakiri kuwa sheria ikishawekewa kanuni ndipo itaanza kufanya kazi. Tuliwauliza sasa kama mmeshazuia watu kupewa pesa zao,hizo kanuni zitafanya kazi gani. Sisi tuna mikataba mifupi,mazingira hatarishi na ajira za kubahatisha. Tunasema tunataka pesa zetu pindi tutakapohitaji. Akiba ya mtu anaitumia pindi atakapoona inafaa.Serikali isikwepe majukumu ya kuhudumia wazee kwa kigezo cha kuwalazimisha kuwapa akiba zao wenyewe uzeeni. Huu ni udhaifu tunaouzungumzia. SHERIA HII HATUITAKI

John Mnyika said...

Ndugu wafanyakazi na wadau wa Hifadhi ya Jamii:

Nashukuru kwa maoni mengine mliyoendelea kuyatoa. Masuala yafutayo ya nyongeza yamejitokeza:

Marekebisho yazingatie kuwa pamoja na migodi ya madini ziko kazi nyingine vile vile ambazo zina mazingira maalum na orodha imetajwa ikiwemo wanamichezo ambalo hulazimika kustaafu kabla ya umri wa kawaida wa kustaafu.

Pamoja na marekebisho ya sheria kuna masuala pia kuhusu hifadhi ya jamii ambayo yanapaswa kuzingatiwa kwenye mchakato wa katiba mpya na hii inanifanya niwerejeshe kwenye mchango wangu bungeni tarehe 13 Aprili 2012 ambapo nilisisitiza suala hili.

Marekebisho yazingatie fao la elimu kutolewa kwa mwanachama anapokuwa mahitaji na kwamba fao la kujitoa lilikuwa mkombozi kwa wanaocha kazi au kuachishwa na kutumia fedha za mafao kujiendeleza kielimu na hatimaye kupata mishahara bora baada ya kuhitimu.

Yameulizwa pia maswali; “Wabunge wao baada ya miaka mitano sheria inasemaje na kodi zao vipi wanalipa NSSF wanaweka au inakuwaje”, ifahamike kwamba wabunge mafao yanaongozwa na sheria tofauti “Political Service Retirement Benefits Act (Cap. 225) R.E. 2002 ambapo hupewa gratuity mara baada ya ukomo wa ubunge.

Hata hivyo, wabunge kwa hiyari yao kama nyongeza wanaweza kujiunga na mifuko ya hifadhi ya jamii (Na naomba kutangaza maslahi kwamba mimi ni mwanachama wa mfuko mmojawapo).

“Swali la mwisho Mheshimiwa, kwa maelezo ya Naibu Spika kuhusu mwongozo ulioomba juu suala hili, na marekebisho ya ratiba za shughuli za bunge, ni kama "wameshajipanga kukwamisha" kujadili haya”.

Muongozo bado haujatolewa lakini unaweza kutolewa kwa mwelekeo ufuatao; ama itaelezwa kwamba kwa sababu ya ufinyu wa muda suala hili halitaweza kujadiliwa kwenye mkutano huu au Serikali itatoa mwelekeo wakati wa Mjadala wa Bajeti ya Wizara ya Kazi na Ajira au Hoja Binafsi itaingizwa katika ratiba ya Bunge.

Kwa upande wa Muswada binafsi naomba nisieleze katika hatua ya sasa nini kinaweza kuelezwa wakati wa kutolewa kwa muongozo ingawa tayari nimeshaanza kuona mwelekeo. Uamuzi wa kukusanya saini za wabunge unalenga kuongeza uzito katika hatua yoyote kati ya hizo nilizozieleza na ikiwa hatua hizo hazitachukuliwa basi muswada ukiingia bungeni utaweza kuleta ufumbuzi.

Yametolewa pia maoni ya hatua ambazo wadau wenyewe kwa upande wao wanaona ni vyema wazichukue, hayo ni masuala ambayo mnaweza kuendelea kuyajadili katika vyama vyenu na mikusanyiko yenu na kuchukua hatua zaidi kwa kuzingatia katiba na sheria za nchi.

Kwakuwa tayari imeshafika saa 11 ambayo ni mwisho wa mkutano wa leo, na kufuatia maombi ya wafanyakazi na wadau wengine wa hifadhi ya jamii waliosema kwamba leo wamechelewa kupata taarifa na wangependa kushiriki kesho, naomba kusitisha kikao mpaka kesho saa 7 mchana mpaka 9 alasiri tutakapoendelea. Maslahi ya Umma Kwanza.

John Mnyika (Mb)

Anonymous said...

Tatizo kubwa la wanasiasa ni Kuburuta hizi taasisi kutokana na matakwa yao.na sio matakwa ya wafanyakazi ambao ndio wadau wakubwa!Pesa zilizoko kwenye mifuko ya jamii sio akiba ya serikali, ni pesa za wavuja jasho wasizitolee maamuzi bila baraka za wafanyakazi hata kama ni kwa faida yao!

Methusela Rwassa said...

Yaliyosemwa ni mengi sana. kwa serikari yoyote sikivu hapa duniani na kama serikali ya Tanzania imo:-
1.itafuta au kuondoa kipengele husika.
au 2.italipa michango yote ya wanachama kiisha kuanza upya mfumo huu bila ubaguzi, yaani wafanyakazi wote mpaka Raisi sheria itamhusu.

Anonymous said...

Sikubaliani na sheria hii kandamizi ningependa nipate pesa yangu ningali na nguvu za kuzitumia.
Kuna vyanzo vingi vya mapato kwanini serikali iendelee kuwakandamiza wafanyakazi? hii haikubaliki!
Ninawaasa watanzania wenzangu administration change is only solution to this tyranny leadership.

Anonymous said...

Pamoja na watu wengi kutoa maoni mazuri na mimi naunga mkono yote ila nabaki na maswali mengi yasiyo na majibu kuhusu hii sheria,nijuavyo mimi bunge ndio linatunga sheria nawabunge ndio watungaji hivi wabunge pamoja na huyu mnyika walikuwa wapi wakati hii sheria inatungwa?hawakujua madhara yake au?wote walikuwepo sasa kwa nini muda huu ndio wanajifanya watetezi wetu wakati walitunga wenyewe hiyo sheria?tungenyamaza nao wangenyaza,achane siasa za kinafki kwenye maisha ya watu,hamna msaada wowote zaidi ya kujitafutia kula na umaarufu wa kisiasa.

Anonymous said...

Yameshatokea, yatupasa kuanza sasa na sio kunyosheana vidole nani mnafiki au nani sio mnafiki. ni mara ngapi pale bungeni wabunge wa upinzani wanakataa bajeti au hizi sheria lakini kwa sababu ya uchache wao wanashindwa na ccm kwa kusema ndioooooooooooooooooooooooooooooooooooooooooooooooooooooooo na mwisho sheria kama hizi zinapita au mnasahau?????????????????????

Mimi kwa kweli nimesikitika sana sheria hii kupita kwa kweli utakuwa mzigo kwa watanzania kwa sababu kazi nyingi tunazofanya za mashirika binafsi mkataba mrefu ni miaka 5 sasa baada ya kumaliza nahitaji hela yangu kwa sababu siwezi jua muda gani toka pale nitapata kazi nyingine.
Wao wenye nchi yao ndio waliopitisha sheria hii kwa sb fedha wanazo hadi wajukuu zao ambao bado hawajazaliwa watazitumia lakini je sisi walalahoi ambao tutateseka huku mtaani tutafanyaje?

Kwa kweli tunakutegemea utuwasilishia mawazo yetu kwa ilo bunge kwa sababu bila hivyo kwa kweli hakitaeleweka mnatuchokonoa wa tanzania hadi kwenye macho kuna siku tukisema enough itakuwa tooooooo late.

Anonymous said...

Mimi maoni yangu ni kama ifuatavyo:
1. Swala la kusema kwamba eti mtu kuchukua mafao yake ni mpaka akifikisha umri wa miaka 55 halikubaliki na wala halitokubalika kamwe.
2. Wanachama wajulishwe juu ya matrumizi, mapato na fedha zilizotumika katika uwekezaji kila mwaka. Wanachama wanatakiwa wajue ni kiasi gani mfuko wao umewekeza na faida yake itakayopatikana kutokana na uwekezaji pia iwekwe wazi. Na ikiwezekana pawe na gawio la faida kwa wanachama kwa kiasi fulani kila mwaka ambapo hela hiyo itaingia moja kwa moja kwenye account ya mwanachama.
3. Kuwe na utaratibu wa mobile ambao utamwezesha mwanachama kujua salio lake kila mwezi na pale ambapo mwajiri hakuwasilisha makato ya mwezi husika basi afahamishwe ili aweze kuchukua hatua.
4. Bodi zinazosimamia mifuko hii ziwe na wawakilishi wa wafanyakazi/vyama vya wafanyakazi ili kwenda sambamba na mabadiliko na kuondoa uonevu kwa wanachama.

Anonymous said...

in my views without looking back on who did pass the bill is that we should look at the meaning of pension funds, in my little knowledge I know ni mafao ya uzeeni, yaani mtu unapostaafu then you are entitled of getting this so uendelee na maisha kawaida. now the about tuliyonayo ya kuchukua mafao tunapohama kazi sio nzuri, kwa sababu at the end of the day unakuja kustaafu unapewa million mbili tunaanza kupiga kelele knowingly tulikua tunachukua mafao yetu while we were still abled bodies, maoni yangu ni integration ya hizi pension funds, mtu akihama ahame na pension yake, ili akija kustaafu inakua accumulated over the years and mtu anafaidika at the end of the day. so the thing which we should actually focus on it to make sure this pension funds are keeping the actual and accurate information ya wateja wao, and they need to make sure wateja wnapata haki zao. the pension funds were meant to be pension funds not the bank account to collect the funds when you move from one company to another. kwa sababu at the end of the day tutailaumu tena serikali kwa kutowajali watu waliosaidia kujenga uchumi just because we have manage to draw our pension funds before we were to retire.

cheers

Anonymous said...

for the second view nadhani we do not need to re-invent the wheel, there are many countries who are managing the pension funds, wao wanafanyaje? nimeona mtu anasema kua akiacha kazi akajiajili then asubuhi mpaka miaka 55, I am sure pension funds are not only for people walioajiliwa, it is also viable kwa wale amabao hawajaajiliwa, kwani kila mtu anaouwezo wa kujiwekea/ kujichangishia hizi funds, this is more like investing for your future, kwa sababu hatujui mini kitatokea hapo baadae, and I don't think its fare kujiweka rehani na kutegemea watoto wake wakutunze ukiwa mzee. so lets see how the scandivian are doing, what are the rules in the US, rwanda nao je, na pia south africa, then lets come with the best plan for our country, lets not invest the wheel. and lets put politics aside.

Anonymous said...

samahi mheshimwa, nimesahau kukupa pongezi na asante kuweka hili wazi and kwa watu wachangie, ila pia usitegee pekee mchango wa watu, ila jaribu kwenda kwa wachumi and wataalamu wa mifuko wa pension uweze kupata information za kisomi pia, most of the time sisi wananchi hua tunaongelea hisia, but that is not necessary the best options out there. asante kwa kutugea nafasi.

karwani cretus said...

NI VYEMA HILI SWALA LIJUMUISHE WAFANYAKAZI WOTE WA SERIKALI NA SEKTA BINAFSI,MIFUKO YA JAMII IWATENDEE HAKI HAWA WAFANYAKAZI NA MTU AWE HURU KUTUMIA PESA ZAKE PALE ANAPOHITAJI. WENGINE TUNAPENDA TUJIAJIRI KABLA YA MIAKA 55 NA NAPENDA NITUMIE HIYO PESA KAMA MTAJI

Marcossy Albanie said...

JJM, nashukuru kwa kutoa nafasi hii kuonge na waTz kupata maoni yao.
Hoja yangu ni moja: Kisheria unapoingia kwenye Mfuko wowote, unajaza form za makubaliano ambazo ni mkataba kati yako na Mfuko. Mkataba huu ni kwa mujibu wa sheria zilizoko. Kunapotokea mabadiriko kama haya kulistahili wanachama waulizwe kwanza na iwapo wapo wasiotaka kuhusishwa na mabadiriko hayo wangepewa nafasi kujitoa au kutafuta mahala wanapoweza kutunza amana zao.

Nyongeza ni kuwa Hili ni somo kwa sote na serikali kujua kuwa kwa sasa waTz wamefika mahala wamekata tamaa ya kuishi miaka hamsini, na au fedha watunzao kuwa na thamani baada ya miaka hamsini. Hoja hii inaendana na madai kuwa serikali imefilisika na kuwa inataka kutumia fedha za mifuko hii ili ilipe madeni na kufuja hifadhi za jamii.

Nawashauri wabunge muishauri serikali ijue kuwa kukata tamaa ni jambo baya kuliko kuasi serikali.

Anonymous said...

(Mimi ni mhanga wa hii sheria nafanya kazi Mgodini.)
Mh.Mnyika(MB) kwanza nakushukuru sana kwa kuamua kulivalia njuga zoezi hili. NAPENDA KUSEMA WAZI,KUWA HUU NI WIZI, UTAPELI NA UNYANGANYI WA MCHANA KWEUPE, WA HII SERIKALI YA CCM, NAPINGA KWA NGUVU ZOOOTE SHERIA HII HAIMTENDEI HAKI MFANYAKAZI WA KITANZANIA. Kwanza napenda niulize swali;
1)Ilikuwaje Wabunge wakapitisha hii sheria kandamizi kwa watoto wa kitanzania???
2) Kama kwenye mswada hiki kipengele hakikuwemo, halafu kikachomekwa baadaye, adhabu yake ni nini na ni nani anapaswa awajibishwe??
3)Ili sheria ianze kutumika ni lazima itungiwe kanuni, inakuwaje hii sheria inatiliwa mkazo na SSRA na kuanza kuitumia kabla ya kuwa na kanuni,
4) Kwa nini tusiamini kuwa serikali imefilisika ndo maana inaamua hata kumnyanganya MASKINI kile kidogo alichonacho.

Mh. Mnyika, wallahi ukifika Migodini ambapo ndo kuna wahanga wengi wa hii sheria kandamizi, ukaingia Underground, ukaona mazingira ya huyu mtanzania masikini anapofanyia kazi, ukaingia Process plant ukaangalia machemicals yaliyojaa humo, ukalinganisha mishahara yake na thamani ya kile anachokifanya, halafu ukaona mtu anakaa tu offisini Dar, anaamua kuwa huyu kijana asipewe hela yake hadi miaka 55-60, yaani utalia.

Ikumbukwe kuwa PAYEE ni kubwa sana katika mishahara yetu.

Kwa nini wasiamue wafanyakazi wa kitanzania wakalipwa sawa sawa kama wafanyakazi wa kigeni mf.huku migodini, ili wakusanye KODI NYINGI, waache kuangalia /kukodolea macho vijisenti vya watu ??????????? au haiwezekani?? na ugumu wake ni nini??

Tanzania ni nchi iliyojaliwa RASILIMALI nyingi mno, ambazo zingelikuwa zinatumika vizuri na ipasavyo nchi hii ingelikuwa mbali sana kimaendeleo.
Wanashindwa kukusanya kodi, wanatoa misamaha ya kodi isiyo na tija kwa taifa, wanaleana kiufisadi, wanaiba hela na wanawekeza nje ya nchi( NYIE WABUNGE WA UPINZANI MNASEMA NA MNAJITAHIDI KUFICHUA HAYO MAOVU), wanaleta makampuni ya kuifilisi nchi yao, daaahhh!!! mf. richmond, symbion power, aggrko n.k n.k, hivi uzalendo uko wapi jamani??
ukweli ni kwamba mwisho wa CCM umekaribia, ukiona migomo nchi nzima ktk sekta mbali mbali,na hata hili la NSSF/PPF, ujue mwisho umekaribia.
Mh. Mnyika tuko wote pamoja, utawala wenu ndo utaondoa huu udhalimu. ''PEOPLEEEES POWER''

Anonymous said...

Mengi yamesemwa ila naongezea hawa jamaa ni wakandamizaji na kwanini wamepeleka kwa kasi utekelezaji wa sheria hii kwa kutoa deadline ya 20 July wakati kuna watu kisaikolojia walikuwa wamejiandaa kabisa muda mchache ujao kuchua mafao yao kwanza kimsingi sheria ilitakiwa kabla ya kuzuia wanachama kujitoa wawaeleze kabisa kwamba baada ya kipindi flani sheria hii itaanza kutumika ili wale ambao tayari walishakuwa hawana ajira na wameanza mchakato au wapo kwenye mchakato wachukue na wale ambao wapo kwenye ajira kisaikolojia waweze kujiandaa kisaikolojia ikiwa na maana kwamba mikataba yao ikiisha hakuna fao la kujitoa.

Kiukweli watapoteza wateja maana wengi watahofia kujiunga na hii mifuko either watafanya waajiri wale njama chafu na waajiriwa kwa kuwa na paying slip mbili ambazo moja itakuwa ya NSSF na TRA ambayo itakuwa na mshahara mdogo na nyingine itakuwa ya mshahara mkubwa mwisho wa siku serikali inakosa PAYE na mifuko inakosa hela maana makato yatakuwa feki.

KIUKWELI MIE NI MUHANGA WA HILI KWANI CONTRACT YANGU IMEISHA MAY 31 NA NILIKUWA NIMEJIANDAA KABISA BAADA YA MIEZI SITA NIFUATILIE MAFAO YANGU KAMA SHERIA YA MWANZO ILIVYOKUWA INAAGIZA NA SAVINGS YANGU NILIWEKA NIKIJUA KABISA ITANISUKUMA SUKUMA HATA MIEZI MITANO IJAYO ILI KUSUBIRIA NSSF ZANGU INCASE KAMA SINTOPATA AJIRA. LAKINI WALICHOFANYA NI KUTUKANDAMIZA KWANI HATUKUJIANDAA NA SHERIA HII MPYA HASA SIE MIKATABA ILIYOISHA HIVI KARIBUNI KWANI MWAKA MMOJA KABLA YA MKATABA KUISHA MOJA YA MKAKATI WA KUISHI ILIKUWA NI PAMOJA NA FEDHA ZA NSSF HIVYO KWA KUKATA GHAFLA IMETUATHIRI.

Anonymous said...

Hongera ndg. Mnyika kwa kuamua kufanya hili ba kutuwakilisha vyema. Hii iwe fundisho kuwa siku nyingine muwe mnasoma between lines kugundua haya mambo mapema. Sio mnalala na kushadidia maswala ya posha alafu baadaye ndo mnakuja na kuleta HOJA BINAFSI.

Ipyana Mwakamela said...

Mheshimiwa Mnyika kwanza napenda kuchukua fursa hii kukupongeza sana kwa kufungua mkutano huu. Mimi ni mmoja kati ya watu ambao wanafurahishwa sana na jinsi unavyowakilisha wananchi. Hiyo ndiyo tafsiri halisi ya UWAKILISHI. Nakupongeza sana na usirudi nyuma.

Kwa kifupi ni kwamba sheria hiyo ni mbaya haifai hata kidogo na ina kusudi la kuwafanya Watanzania kuwa "watumwa" miaka nenda rudi. Ninayasema haya katika mantiki hizi:
1. Ajira zenyewe ni za hovyo kwa maana ya malipo hafifu. Sasa mtu anaamua tu kujiingiza katika ajira hiyo ili aweze kutengeneza angalau mtaji kidogo akaendelee kujiajiri kwa sababu Benki siyo rafiki wala mkombozi wa umasikini wake. Kuifunga hiyo fursa ni sawa na kuamua kuwa na taifa la watu wanaofanya kazi kwa kuchakazwa bila malipo stahili.

2. Thamani ya pesa yetu inashuka kila uchao. Dhana ya kwamba mtu anaweka fedha zake ili apate mafao mazuri baadaye ni dhana iliyopitwa na wakati na haina manufaa. Kwa mfano mtu ambaye leo ana miaka 25 leo kwa kimshahara anachopata sasa na ongezeko lisilo na tija, miaka 30 baadaye hata kama fedha zake katika hifadhi za jamii zitafikia kiwango cha milioni 30 haitamfaa kitu labda akanunulie baiskeli tena chakavu. Hivyo sheria hii haimsaidii.

3. Tumeambiwa "life span" ya Mtanzania imeshuka kutoka miaka 50 mpaka 48 kama nimenukuu vizuri. Sasa kama hivi ndivyo ni nani atakuja kuchukua hiyo pensheni wakati hakuna uthibitisho wa kufika umri huo. Hii ni dhuluma ya makusudi. Na pia uwezekano hata wa kufika miaka hiyo 48 hakuna kutokana na ujira mdogo ambao watu wanaupata kwa kazi ngumu wanazozifanya. Mwishowe wanadhoofu kiafya na hatimaye kuondoka duniani kwa kushindwa kumudu ukali wa maisha na hivyo kupata msongo wa mawazo.

Mimi binafsi siipendi sana hii sera ya hifadhi ya jamii kutokana na huduma mbovu zinazotolewa na mifuko hasa NSSF ambao wanaonekana wanafanya kazi kama msaada kwa Mwanachama na sio wajibu. Hata DG nilipomuandikia kwa anuani yake ya barua pepe aliamua kunipuuza kama meneja wake wa kanda alivonipuuza na nikakosa sehemu ya kukimbilia. Naambiwa faili langu lipo Mikocheni halipatikani, mara ofisi ilikuwa haina watu walikuwa wanaumwa, mara naambiwa Printer ilikuwa mbovu. Mambo ya ajabu ajabu.

SSRA wanachotaka kukifanya sio kumfaa mfanyakazi hapo baadaye bali ni kuhakikisha hii mifuko inazitumia hizi pesa za wanachama kuwekeza zaidi katika "real Estate" miradi ambayo haina tija kwa mfanyakazi wa kawaida.

Hakuna faida hata kidogo ya kumpatia mtu fedha zake alizozitolea jasho kwa muda mrefu kwa masharti ambayo hajayaridhia. Sioni kama fedha hizo zitamsaidia wakati tayari hana nguvu tena badala ya kumpa akiwa na nguvu zake ili azitumie ipasavyo katika uwekezaji ambao utampa manufaa katika maisha yake ya siku za usoni.

Tumewaona wazee wa Afrika Mashariki mpaka leo wengine hawajalipwa, wanafaidika na nini katika hilo wakati wengine walikwishafariki dunia na hata waliowarithisha pia wamefariki.

Kama kweli kuna nia ya dhati kumkomboa Mtanzania katika lindi la Umasikini basi sheria hiyo ifutwe na watu waruhusiwe kuchukua mafao yao wakati wowote watakapokuwa wameacha kazi ili wakaendeleze maisha yao katika mipango waliyonayo. Ijulikane tu kwamba sio kila aliyekwenda kwenye ajira anapenda kuajiriwa ispokuwa ni kwa sababu ya kutokopesheka na Benki kwa kukosa dhamana hivyo akaamua kujiweka dhamana yeye mwenyewe kwa kufanya kazi ili baada ya miaka miwili au mitatu achukue pesa zake uwe mtaji.

Milango yote ya fursa ikifungwa kwa Watanzania wataamua kuchukua hatua mbadala ambayo inaweza kuwa hatari zaidi. Fedha za benki hapewi, za kwake mwenyewe alizoweka anapangiwa mashariti lini achukue, ni kweli sheria hiyo inawajali Watanzania wa kawaida?. jibu ni HAPANA ispokuwa kinachofanyika ni UONEVU na UKANDAMIZAJI.

Anonymous said...

Ally J. Farahani
Geita.
Mengi wadau wamesema, sitaki kuyarudia ingawa ni muhimu kusema kile unachodhani ni kitu cha msingi ikiwa lengo ni kujenga na si kubomoa kama walivyofanya hivi mpaka kutupotezea muda mwingi kufikiri nini kifanyike, kifupi na cha msingi wanatakiwa wajiulize ni kwa nini imekuwa hivi na je kama kweri ni wazalendo kwanini wasiwajibike kwa kutokufanya research ya kutosha na kuipitisha sheria hiyo?.
Mh. MB, mi mawazo yangu, hebu nawe jaribu kuyatafakari. Withdrow benefit iwepo kama kawaida, pia kila mwanachama husika awe mwanahisa wa shirika husika, hii ni kwa sababu mwanachama huyu michango yetu ndio inayotumika kuweka miradi yote ya mashirika. hivi faida zote zinazopatikana ni wapi zinakwenda? Miradi waliyowekeza kila kukicha thamani inaongezeka, lakini je kwa upande wa hela wanayonikata thamani yake je inaongezeka? kwa nini nasema tuwe tunapata gawiwo kama wana hisa wa shirika husika baada ya kuwa mtu umechukuwa mafao ya kujitoa. hebu fikiria 150,000 ninayochangia leo baada ya miaka mitano thamani yake itakuwa sawa na ya leo?? lakini ile mijengo je ya Nssf na PPF thamani yake itakuwaje baada ya miaka mitano?
Kama hilo haliwezekani basi ni mara mia tuwe huru, isiwe lazima mtu kujiunga na mifuko hii, kila mtu ajue ni wapi atawekeza pesa zake ambako kuna faida kuliko huku wanaofaidika wachache.

Anonymous said...

Nimeshindwa nianze kwa kuelezea vipi.Ikumbukwe kwamba Mfanyakazi wa sekta binafsi anapoacha au anapoachishwa kazi hana msaada mwingine wa kujikimu kiuchumi zaidi ya kutegemea MAFAO YAKE yaani NSSF,PPF tofauti na Serikalini ambapo kuna Gratuity (Malipo ya mkupuo),Pensheni na n.k.
Waliowaza kuondoa malipo haya ni wauaji wakubwa na sidhani kama ni Watanzia asilia.
Nawakumbusha wahusika kurudisha mafao haya ya kujitoa mara moja na hili lisichukuliwe katika hali ya Kisiasa.
Keep in mind that "there is no peace without justice'

Anonymous said...

Ni vyema serikari yetu ikaangalia wastani wa sasa wa umri wa Mtanzania wa kuishi ni miaka mingapi kwani kwa umri waliouweka wa kuchukuwa mafao ni watanzania wachache sana wanaofikisha umri huo.
Vile vile nia ya serikali yetu ni kuwasaidia wananchi wake na si kuwaumiza,lkini kwa sheria hii serikari haitawasaidia hata kidogo kwani hata hao watakao bahatika kufikisha umri huo nao wataishi miaka michache na kufariki na kuwakosesha haki ya kufaidi mafao yao.Jambo hili litapoteza imani ya wananchi kwa Serikari yao na kuiona kama inawaibia pesa zao na si kuwasaidia

Anonymous said...

Mnyika (MB) nakupongeza sana kwa kutusaidia watanzania na hasa wafanyakazi. Mimi nina PhD na ni Seniour lecturer wa chuo kikuu kimoja maarufu Tanzania. Naona huo ni ukandamizaji mkubwa wa serikali iliyoko madarakani na kutojali wananchi wake. Sioni kwa nini unibane mpaka 55 yrs ndio nipate mafao yangu. Naweza acha kazi nikawa mjasiriamali nikajiajiri kwa nini nisubiri pesa zangu miaka yote hiyo ambapo zingeweza kunisaidia kuzalisha zaidina kujiwekea mazingira mazuri ya maisha ya sasa na baadae. Serikali imefanya hivyo kwa makusudi wakijua mifuko hiyo iko taabani kutokana na serikali kuitumia kama banki sizizotoa riba kwa maslahi yake binafsi. Wafanyakazi wengi tumevunjika moyo kwa hilo na hatuoni matumaini ya hii serikali kabisa. Inatumia mabavu na vitisho, dola kufanya matakwa yake na wananchi hawasikilizwi. Sijaona serikali iliyopoteza dira,mvuto na thamani kama hii ya sasa. Mambo hayako shwari nchini. Tunaiomba serikali ijaribu anagalia hoja na wananchi ikiwemo hii haraka na kufanya mabadiliko

Anonymous said...

NAMSHUKURU MUNGU KWA KUPATA NAFASI HII,PIA NAKUSHURU MH.MNYIKA KWA KUTUPA UWANJA,MIMI NI MMOJA WA WAHANGA WA HILI JANGA,YANI ROHO INAUMA SANA NA UKIZINGATIA SISI WENGINE HUWA TUNAFANYA SANA KAZI KWENYE MAKAMPUNI BINAFSI AMBAYO HUWA MIKATABA YAKE NI MIAKA MIWILI IKIZIDI SANA MITATU,NA HAPA NILIPO NI 30 YEARS OLD,NA AJIRA IMESHAKWISHA KWA MUHINDI NA KAMA UNAVYOWAJUA WAHINDI HAWANA UTU NIMEKUWA KWENYE AJIRA KWA MWAKA MMOJA NA MIEZI MINNE PROJECT IMEPUNGUA NAE KATUPUNGUZA KAZI,SASA NI KWELI NISUBILI MPAKA MIAKA 55?,KUNA MPANGO GANI HUKO SERIKALINI HEE?WANATAKA KUIPELEKA WAPI HII NCHI?HEEE JAMANI EBU JARIBUNI KUIKOMALIA JAMANI,TUMEWAAMINI WABUNGE VIJANA MBADILISHE MFUMO WA KIBEPALI NA WIZI AMBAO UMEANZA TANGU AWAMU YA TATU,AU KWAKUWA WAO WATOTO WAO SI WAAJILIWA,KWAHIYO WANACHOKIIBA WAO WANAWAPA WATOTO WAO NA KUFUNGUA VIJIKAMPUNI VYAO UNAJUA HII INAUMA SANA KWA SISI WA HALI YA KATI MPAKA CHINI,PIA WANAWASAIDIA WAHINDI KUIBA KWASABABU MAKAMPUNI MENGI YA KIHINDI HAYAPELEKI MICHANGO MPAKA MTU UENDE KUDAI,MAISHA MAGUMU WATU WANATAKA WACHUKUE MAFAO YAO ILI WAJIAJILI PIA TUWEZE KUSOMESHA WATOTO,HAKUNA KUMUNG'UNYA MANENO HAPA HUU NI WIZI,WAJIANGALIE SANA,MWL.NYERERE ALIPOSEMA SERIKALI HAINA DINI HAKUMAANISHA HIVI SERIKALI HAINA HURUMA KWA WANANCHI KAMA WANVYOFANYA HAWA,WAMEUGEUZA MSEMO,WASIPOANGALIA HII NCHI ITAKUWA KAMA MISRI,IRAQ,AFGHNISTAN AU LIBYA WATAONDOKA KAMA WALIVYOONDOKA VIONGOZI WA NCHI HIZO,MAREKANI AKIAMBIWA ATAPEWA ROBO YA URENIAM,NA ROBO NYINGINE ANAPEWA MFARANSA,WANATUSAIDIA KABISA KUWAPOTEZA LAKINI HATUTAKI KUFIKA HUKO,TUANGALIANE KIUBINADAMU,WENGI NI HALI YA CHINI NA WENGI TUNAFANYA KAZI KAMPUNI BINAFSI AMBAZO MIKATABA YAKE IKIWA MIREFU BASI NI MIAKA MIATU,MH.MNYIKA TUNAKUOMBEA MUNGU ULIFANIKISHE HILI INSHAALAH MUNGU ATAKUPA UWEZO,NGUVU,NA UJASILI LITAFANIKIWA KWA AMANI NA UPENDO,TANZANIA NCHI YETU IENDELEE KUWA NA AMANI AAAAMEN.

Cantona said...

WENGI WAMESHATOA MAWAZO YAO TENA YOTE NI YA MSINGI.
PLEASE MR JOHN JOHN PASS THIS MSG TO THE WEAK GOVERNMENT OF TANZANIA THAT ENOUGH IS ENOUGH.
THEY CAN FOOL SOME PEOPLE FOR SOME TIMES BUT THEY CAN'T FOOL ALL PEOPLE AT ALL THE TIME.

Anonymous said...

maoni yangu ni kwa hii sheria juu ya mifuko ya jamii niyakuwaumiza watanzania kwa sababu muda mwingine mtu anaweza kufa na kama huyu mtu kaacha watoto itawabidi kusubiri miaka hiyo ifike pasipo msada wowote ule wataishije?. Nafikiri hii sheria iondolewe na kamainawezekana twende kwa wananchi kwa kura za maoni ili tujue ni asilimi angapi wanataka kuwepo kwa hii mifuko ya jamii na kama sivyo isiwe lazima kujiunga na hii mifuko kwa sababu sioni msaada wake labda kwa mtu asie na malengo maana huwezi kushika fedha za mtu kwa muda wote huo harafu unaniambia inajenga maisha, kwa namna ipi au unafikiri kwamba watanzania huweka tu hela sehemu pasipo kuingiza chochote naona ipo haja ya kutambua wananchi wanataka nii

Anonymous said...

<1>kwa maoni yangu kwa sasa bado sheria hii siyo nzuri,bado muda wake kufanya kazi
<2>kima cha chini cha mishahara ni kidogo sana hivyo nia hii ya kuzuia mafao mpaka mafanyakazi afikishe miaka 55 maisha yao yatakuwa magumu zaidi
<3>nashauri kima cha chini kipandishwe angalau kifikie 450000 ili mfanyakazi aweze kuwa na kipato cha kumsogeza hadi afikishe miaka hiyo 55

kwa sasa sheria hiyo haitufai kabisa

Anonymous said...

Ninachokiona CCM wanaandaa fedha kwa uchaguzi wao wa kifisadi wa mwaka 2015. Mifuko hii ya jamii imekuwa ikitumika vibaya, kwa mambo ya kifisadi na kukopesha wahindi. Watalipa vyote walivyoiba. Kila jiwe litajeuzwa. Wanaamua mambo mengi bila kuwahisisha walengwa wa mfuko.

Anonymous said...

Ni ajabu kubwa mifuko ambayo ni ya wafanyakazi badala ya kuweka maslahi ya wafanyakazi mbele yenyewe inaweka maslahi ya mifuko mbele ambayo kwa namna yoyote haiwanufaishi wafanyakazi,Leo hii mfanyakazi anastaafu anavyosumbuliwa kupata mafao yake utadhani labda siyo fedha aliyochangia kwa miaka nenda miaka rudi!kwanza mifuko hii inainvest fedha nyingi kwenye miradi ambayo kwa vyvyote vile haina maslahi kwa wanachama.Nivyema mifuko hii ijielekeze kujenga imani ya wanachama kwa kujali interest za wanachama.kama vile kuweko miundombinu dhabiti ya kuwakopesha.

Anonymous said...

Ni vema ikafanyika kama ifatavyo,
1. mafao yetu yaendelee kutolewa kama kawaida ilivyokua
2. SSRA watoe hiyo miongozo na kuwaelewesha wanachama umuhimu wa kusubiri miaka 55-60 ndio wachukue pesa yao.
3. mwanachama mwenyewe aamue kwa hiari yake kujiunga na huo utaratibu mpya sio lazima.
4. SSRA waongeze nguvu ya kusimamia mifuko kwenye uwekezaji sio makusanyo ya wanachama.

mariam said...

Mafao yakujitoa yaendelee kutolewa pindi mwanachama wa mfuko husika anapowasilisha nyaraka husika kama ilivyo kuwa mwanzo, tena sheria juu ya fao hili isiishie kutekelezwa na NSSF pekee bali itumike kwa MIFUKO YOTE YA HIFADHI YA JAMII (PSPF,LAPF, GEPF, PPF nk).!

Kiwango said...

Hongera sana Mheshimiwa Mnyika. Zipo sababu nyingi za hii sheria kutokuepo. Mtu anaweza kuacha kazi halafu bahati nzuri akataka kubadilisha mfuko, hivyo ni lazima achukue hela yake kutoka mfuko wa awali. Kujiajiri mwenyewe ukiwa kijana ufanisi wa kazi unakuwa mzuri zaidi kuliko mzee, hivyo hela ni lazima upewe ukiacha kazi. Kuna kampuni nyingine huruhusiwi kufanya kazi kwa miaka mingi kwa sababu ya mazingira magumu, hivyo ukiacha kazi upewe haki yako. Naweza nikawa nimefanya private ili ukifika mda fulani nikasome kwa hela ya mfuko, je miaka 55 nitaweza tena kusoma? Wafanyakazi 100% ktkt kada za migodi, viwanda vyote na private zote wanategemea kutumia kufanyia kazi hela yao baada ya mkataba waliopewa. Hivyo hii sherai ni batili haiwatendei haki Watanzania na vizazi vyao.

Anonymous said...

Hongera sana Mhe. Mnyika kwa kulipa nafasi ya kipekee suala hili.
Binafsi naamini mpaka sasa serikali inafahamu fika kuwa sheria hii haina tija kwa wwajiriwa.Wanafahamu pia kuwa waajiriwa wanahitaji kuwa na uhuru wa kuamua juu ya pesa zao wanazokatwa na kwenda katika mifuko ya kijamii.Kutosikiliza maoni yetu na kuyafanyia kazi mpaka muda huu sio dalili njema na inaonyesha ni jinsi gani serikali hii isivyokuwa na nia njema juu ya raia wa nchi hii.
Kama serikali haitoibatilisha sheria hii na kutuweka huru juu ya pesa zetu ni dhahiri waathirika HAWATOSHIRIKI ZOEZI LA SENSA la mwaka huu na pia wategemee MIGOMO YA WAAJIRIWA ISIYO NA KIKOMO.
Haki haiombwi,Inachukuliwa.

oche said...

Mh. John hongera kwa ili, lakini swali langu ni, Wakati sheria hii inapitishwa je ilijadiliwa bungeni?

Anonymous said...

Kwanza napinga kwa nguvu zote kuondoa fao la kujitoa. Sitaki kurudia yale yaliyokwisha semwa na wenzangu.

Lakini kikubwa ninataka Mh. Mnyika kupitia bunge, uwakumbushe wajibu wa KWANZA wa kuundwa SSRA. Ilikuwa ni kupitia mifuko yote ya jamii na kutoa mapendekezo jinsi ya ku-hamornize formula ya kukokotoa mafao ya Pesheni.

Mfuko wa serikali kuu PSPF unalipa mafao mazuri kulinganisha na mifuko mingine yote ya jamii. Hivyo sisi wafanyakazi TUNAITAKA SSRA kwanza ifanyie hiyo kazi iliyopelekea kuundwa, ipendekeze formula nzuri ya kukotoa mafao ya pensheni iatakayotumiwa na mifuko yote, sio wafayanyakazi wa serikali kuu kujipendelea kupitia PSPF.

Haiwezekani Mwalimu mwenye first degree anayefanya kazi serikali kuu alipwe pensheni mara 4 ya Professor wa chuo kikuu ambaye wamefanya kazi kwa miaka sawa.

Hii dhuluma ndiyo tunataka SSRA ituondelee sio kutuongezea KERO kwa kuondoa fao la kujitoa.

Anonymous said...

Mbunge naomba umuulize waziri Membe kwa nini Watanzania wanaoomba visa ya Uingereza wananyanyaswa na wanabaguliwa na Ubalozi huo Nairobi tofauti na WAkenya?Haswa watanzania weusi.

Anonymous said...

HASHIM O. MMBAGA
0764100001

MAWAZO YANGU NI HAYA:
1. Marekebisho yawepo ila pawepo na vipengele ya hiyari ya kuchagua ukomo sababu ni kwamba sekta binafsi nyingi mikataba nikati mwaka 1 mpaka miaka 10 unasaini upya mkataba na baada ya hapo wengi hujiajiri, wakati mfanyakazi wa serikali mkataba wake haivunjuki mpaka astaafu so kuwepo mfano fao kuanzia miaka ya kufanya kazi 5, 10, 15, 20, 30 na kufikisha 55-60 ya kuzaliwa ndio ukomo kuwa na faida na hasara kwa kila miaka ya ukomo mtu anachagua mwenyewe kwa faida yake.
2. Kuwepo na mtandao wa uwazi kwa mifuko kwa mteja ya kuonyesha kuwa mchango wako unapelekwa na muajiri siki hizi IT ipo waweze kutoa taarifa kila wakati pindi mteja anahitaji na mahali popote alipo kwa njia ya internet au kwa simu, pia kila mwaka kuwepo startment yako yote kama mteja uipate iwe ni amri.
3. Kuwepo na uwezo wa kuwezeshwa kuwa fao lako mfano kila mwaka kunakuwa na unakiasi gani kule na pia kinaweza kuwa msaada wa kukuwekea dhamana kwenye taasisi mbalimbali mfano mikopo ya kimaendeleo ya ujenzi, masomo nk.
4. Kuwepo na uwezo wa mteja wa kununua hisa katika vitegauchumi vinavyowekwa na mfuko kupitia mtaji wake kwa mfuko sio kukaa na cash ya mtu muda mrefu halafu wanatoa riba ndogo haina maana ni kunyonya mteja.
5. Kuwepo na mpango mkakati wa makazi bora kwa mteja kupitia morgage system kwenye kupata na kulipia nyumba kutokana na kipato au akiba yako iliyopo kwenye mfuko.
6. Katika kujiunga uanachama mifuko idhamini kuwepo na system ya kisasa ya kuratibu vyombo vyote vinavyotoa ajira mfano kampuni kuanzia iliposajiliwa brela, kwenye leseni ya biashara halmashauri/mji/wizara halafu tra kwenye kulipia marejesho ya kampuni hapo utaipata kampuni ipo wapi na ipo hai na pawepo na utaratibu wa kukata direct toka account ya kampuni kwenda kwenye mfuko itarahisisha sana mteja kupata haki yake toka kwa muajiri wake.
NB: hayayote yafanyike kwa mifuko yote hifadhi ya jamii.
Asante sana tujenge taifa bila woga.

Anonymous said...

Mifuko ya hifadhi ya jamii haiwanufaishi wanachama wake hasa pale inapojiingiza kwenye bishara wakati faida haiwafikii wanachama,
Napendekeza fao la kujitoa lirudishwe tena bila mashart na pia uwepo utaratibu wa mifuko ya hifadhi ya jamii kuwachangia wanachama wake 10% ambayo ni faida wanayoipata kutokana na biashara wanazofanya

aussie4868 said...

Ingekuwa vizuri watu wapewe option kama nchi nyingi zinavyofanya.
Kuna early retirement plan na nyingine unasubiri mpaka hiyo miaka 55 but mtu anakuwa na uhuru wa kuchagua.
1.Early retirement plan inakuwa na penalty ya 5-10% which is called early distribution tax.
2.Nyingine ndiyo hiyo ya hadi miaka 55

Najua madhumuni ya serikali nikuona watu wanakuwa na savings kwa ajili ya retirement, but mtu asilazimishwe, apewe uhuru wa kuchagua.

NICOLE MWANI said...

Mh.Mnyika kwanza namshukuru Mungu kwa kutupa wewe kama kiongozi wetu wanyongeni mtu wa pekee sana.Thamani ya pesa yetu yenyewe haiko sawa,kazi zenyewe hazina tija.Na pia pesa ni haki ya mchangiaji na si mtunzaji?Hii mifuko haina mamlaka na pesa zetu HII SHERIA HATUITAKI MTU AKIKATISHA MKATABA APATE CHAKE TENA MAPEMA ZAIDI

Anonymous said...

MAWAZO YANGU NI KWAMBA KIPENGELE HICHI CHA MAFAO YA KUJITOA KIFUTWE KABISAA ILI ILI TUWEZA KUPATA FAO HILO UKIZINGATIA CC WENGINE TUKO KWENYE PRIVATE FIRM AMBAZO NI MGUU NDANI MGUU NJE. AJIRA INA KOMA UNA MIAKA 35 NA HUNA NAMNA YA KUPATA AJIRA NYINGINE HIVYO USUBIRI KWA MIAKA 20 ILI UJE UPEW MAFAO NI KITU CHA AAJABU SANA. TUNAOMBA NYINYI MLIOKO HUKO BUNGENI MTUPIGANIE SANA SUALA HILI KWA UTULIVU NA BUSARA ZENU ZOTE NATUMAI MTATUSAIDIA BG UP MNYIKA.

Anonymous said...

Utaratibu mpya wanaohutaka SSRA,Hauna tija kwa wafanyakazi.

Lewis Mushi said...

Kimsingi fao la kujitoa liachwe kuwa hiari kwa anayetaka kuacha michango(fedha) yake au anayetaka kuchukua haki yake aruhusiwe kufanya hivyo. Kwa kuwa terms za ajira hutofautiana kati ya mwajiriwa mmoja na mwingine,basi pia hata strategy au style ya kuweka akiba hutofautiana pia. Kwa mfano kuna watu wengi tu kutokana na mishahara yao na majukumu, 10% inayochukuliwa na mfuko wa pensheni ndio savings yake,hiyo 90% inayobaki baada ya kukatwa pensheni hawawezi ku-save kutokana na hali ya maisha.(Na hawa ndio wengi).
Kwa mchanganuo huo ni wazi kwamba mtu atakapoacha ama kuachishwa kazi atategemea ile akiba ndio aanzie maisha kwa wakati husika,sasa kama mtu ana miaka 35,kusubiri miaka 20 ndio achukue haki yake,huu ni ukatili! Na kipindi chote hichi (miaka 20) kama hakuajiriwa tena huyu mtu ataendesha vipi maisha yake.? Hata hivyo,hata kama kutakuwa na interest kwa kipindi NSSF/PPF...wanapokaa na hela yako,sidhani kwa mfumo wa ukuaji wa uchumi wetu kama itaweza kushindana na inflation rate!

Kama tunataka watu wengi wawe na ajira,lazima tu encourage watu kuwa wajasiriamali. Mtu anapoacha kazi na kwenda kuanzisha project yake,kama ni kuku,mgahawa,duka,basi,kilimo, real estate n.k,ni nafasi nyeti ya kuwapa watanzania wengine ajira. Na pale alipoacha kazi pia ni nafasi ya Mtanzania mwingine kuajiriwa. Hizi ndio ajira zenyewe,na sio zile tunazodanganywa na wanasiasa,eti ntawapa vijana ajira,..liers!Sasa tukiweka mfumo huu ni kuwatisha watanzania wasithubutu au waogope kujiajiri na badala yake wajishike kwenye ajira miaka nenda rudi hata kama ajira hiyo haibadilishi maisha yake. Watu waachwe wachukue haki yao mara tu wanapoacha au kuachishwa kazi bila kujali kama ataajiriwa tena au la! Wanaotaka kuendelea kubaki kwenye hii mifuko nao rukhsa.

Anonymous said...

Napenda kuchangia kwa kadri ya ninavyofahamu.1 Mazingira ya kazi kwa mfano migodi ni magumu na hatarishi kwa uhai wa mwanadamu kwa kiasi kikuwa sana kama vile chini ya ardhi,hewa ya kutengeneza,kunguka kwa miamba,mashine zinaua uti wa mgongo na hewa inaua mapafu,vumbi linachangi vile vile madhara makubwa.sehemu ya mitambo inafua madini inatumia kemikari zenye uwezo mkubwa wa kua uhai wa mtu.Tukienda kwenye viwanda vya pamba navyo ni matatizo yale yale.Mikataba ya kazi nayo ni matatizo makubwa sana kwani hakuna mkataba wenye usalama wa kazi ni kama vibarua tu hivyo uhakika wa kufanya kazi muda mrefu ni zero.ufukuzaji wa wafanya kazi bila kufuata misingi ya kazi kadri mwajiri anavyojisikia na kuweka kikomo cha kutokuajiriwa tena sehemu yoyote.Kwa hali hii wajiriwa wengi ni vijana wenye umri kati ya 25 na30 miaka pia elimu yao ni kidato cha sita na nne ambao wanahitaji kwenda baadae shule. Haya yote yanaashiria kwamba fedha waliyokuwa wanatuza wakati wako kwenye kibarua chao kwa njia ya mifuko wa jamii ni ukombozi wao.Umri wa kadri ya kuishi Tanzania kufuatia utafiti ni miaka kati ya 45 mpaka 52 hili ni njanga la kitaifa viongozi wasipokuwa na hekima za kutosha.Binadamu anahitaji fedha zaidi wakati anapokua kwenye umri wa ujana na mtu mzima kwa ajiri ya maendereo yake na familia yake,pia ili kuweka mazingira mazuri kama atabahatika kufika uzeeni.Hivyo ni muhimu kupata mtaji wake aliojiwekea kwa mjibu wa sheria.Kutokana na taarifa zilizo kusanywa na wataaramu mbalimbli zinaonyesha kwamba wazee wanahitaji kiasi kidogo sana cha fedha amboyo ni Tshs16000. kwa mwezi.Udhamani wa fedha nalo ni tatizo.ukiritimba wa watendaji wa serikali,elimu dogo kwa jamii husika kwa ajiri ya kufuatilia mafao.Sheria hii ni ya kibaguzi,ukandamizaji inayolenga kuweka matambaka ndani ya nchi.Inakiuka haki za binadamu,Katiba ya nchi na sheria za shirika la kazi dunia.Pia inaonyesha kuna jambo la hila lililojificha kwa baada tu ya taarifa ya mdhibiti na mkaguzi mkuu wa serikali kuto taarifa ya mifuko ya jamii kwamba iko hatarini kufirisika kwa kutolejeshwa fedha iliyokopwa ikaibuliwa sheria ilikukidhi matakwa yao.Hiki ni kiama kwa wanyonge.Kwa kuzingatia haya yote ninapinga san sheria hii. samaki madhara pia ni makubwa sana,viwanda vya pamba halikadhlika

Anonymous said...

Swali langu mh.mnyika...nashindwa comment mpaka nifahamu hili(HAO WATU WA WIZARA NA HIYO BODI YA SSR KWENYE RIPOTI ZAO WAMEONYESHA KUWA WALICHUKUA MAONI KWA WAFANYAKAZI WA MIGODI KITU AMBACHO NI UWONGO...JE MNAWACHUKULIA HATUA GANI KWA KULIDANGANYA BUNGE??

Malova said...

Kustaafu inaweza kuwa kwa hiyari au laimza. Hiyari maanake mtu anaamua kuacha kazi fulani aliyoajiriwa na kufanya kazi zake. Kwanini mafao aliyoyaweka kwenye mfuko ayasubiri hadi miaka 55? Au hawa SSRA wanafukiri wafanya kazi wote ni wa serikali?

Anonymous said...

Huu ni uonevu wa kukatalia pesa zetu kwani vijana wengi wameingia kwenye ajira ili wakiweka malengo yao kuwa anafanya kazi kwa muda flani halafu anaingia shule kujiendeleza sasa leo hii mnakuja na kuzuia pesa zetu hadi tufikishe miaka 55 sio haki kwani kila mwaka shilingi inashuka thamani, na huko tuendako vijana wengi watakuwa hawana elimu kwani watashindwa kujiendeleza kielimu kutokana na hii sheria kandamizi.

Anonymous said...

Mimi napendekeza kwamba fao la kujitoa liendelee kuwepo coz,
1. Watu wanaofanya kazi Private sectro wanafanya kwa mikataba ya muda mfupi hivyo kushikilia mafao yao mpaka wafikishe miaka 55 ni kuwanyima haki ya kutumia fedha zao kwani hata kuachishwa kazi ni janga mtu ataishije
2. Infation, hizo fedha zinakaa kwenye mifuko ya jamii hazina intrest yoyote, hivyo 10,000,000/= ya leo sio sawa na mtu atakayopewa mwaka 2030, pia serikali iwe considerate, yenyewe inachukua fedha bila kurudisha , kwanza wanachukua fedha bila ridhaa ya wenye fedha, tuna uhakika gani kama watarudisha mtu akifikisha 55 yrs.
3. Je mtu akifa bado hajaattain 55 years pia watasubiri mpaka umri wa marehemu ufike 55yrs?We are not ready for that law.

Tinno Mavura said...

Hongera kwa kubali/kiri kwamba wabunge hawakuwa makini kwa kupitisha sheria hii iliyo na kasoro.

Napenda kushauri kuwa kwa vile ajira nyingi kwa sasa ni mikataba ya muda mfupi yaani 'fixed' kwa mwaka mmoja au miwili sheria zote ziweke kipengele mwenye mkataba wa aina hii aruhusiwe kuchukua michango yake na ya mwajiri wake pamoja na riba.Hata hivyo katika kujenga taifa ambalo raia wake wanaweka akiba,mifuko iweke hamasisho au incentive kwa wafanyakazi wenye ajira fupi kuacha fedha zao kwa hiari kwa kutoa riba kubwa.

Anonymous said...

Nina maswali machache;
1. Watu wengi kwenye private sectror wana ajira za mkataba tena mifupi. e.g 1 or 2 years ... na baada ya hapo mtu anaweza asiajiriwe tena mpaka atakapotimiza 55yrs hawa tunawaweka kundi gani ambao pia ni wengi?
2. Watu wengi kwenye private sector wamekuwa wakitegemea sana hela za PPF au NSSF n.k kujiendeleza kimasomo punde mkataba wake unapomalizika. secta binafsi wala HESLB hawatoi mkopo kwa watu hawa; watakuwa wageni wa nani?
3. Life expectancy ya mtanzania kwa sasa ni 45 to 47 yrs (zaidi ya hapo ni bahati) hili nalo tunaliwekaje? NB hii ni ksayansi zaidi; ki imani life expectancy ni 70 to 80 years and even above
4. Kushuka kwa thamani ya fedha ( kwa wale ambao hawajatimiza point 180, ambao naamini ni wengi, thamani ya millioni kumi leo ni sawa na ....20 years later.
5. Hizo nyumba wanazosema watakopesha umeona thamani yake? most of them ni zaid ya 150M they are not realistic, tena ni apartment, hakuna hata mahali pa kuotesha maua; watupe hela zetu tukajenge wenyewe tunakotaka na ramani tunayotaka
5. Waajiriwa wa miradi, punde miradi inapokufa au kufungwa inakuaje? hususan miradi kama ya ujenzi wa barabara ambayo ikimalizika hata ile kampuni inaweza ikafa na kufutika kabisa, 20 yrs later kuanza ku launch madai tena kwa nchi yetu tunayoifahamu, unaanza kuulizwa cheti cha kuzaliwa, sahihi ya mwajiri ambaye ni non existence by that time, n.k

This might be looking good but to my opinion it should be optional, not compulsory

Anonymous said...

kuwe na ruhusa ya kujitoa, kutokana na circumstancies kama
1. mtu atapoteza ajira halafu hatakuwa amepata kazi let say two years after losing emplymements/job amepewe chake.
kama atapata kazi pension iendelee.
2.Ajira za mikataba kusiwe na kuzuiwa kujitoa kwani itakua ngumu, let say unafanya for two years then kama haujapata kazi haifai kusubiri for 20 au 15 wakati hata ikifika muda huo value ya hiyo hela haitakusaidia.
3. Kuwe na interest ya hela inayowekwa kwa watakao kubali kukokujitoa
4. Wenyec ajira za kudumu wanaweza kuopt kujitoa au wasijitoe kulingana na benefits zitazotolewa na options zote.

http://kadulyu.wordpress.com said...

Sorry I posted on the wrong page!

Social Security Regulatory Authority (SSRA) has recently been formed in Tanzania to regulate functions and conducts of social security fund schemes in Tanzania. As a result a law was passed in April 2012 to review the conduct of the funds including restricting early withdraw of members money until when they reach their voluntary or compulsory retirement ages, i.e. 55yrs and 65yrs. Here are my views on how the new law did not consider the diverse employment terms under which those employed work in. The implementation of the new law as it is now will seriously compromise the economic rights of employees.

The following are my views:

1. I think the law did not consider the nature of employment in private organizations. There is no permanent employment in a similar arrangements like in government or public sector where people are permanently employment to their retirement age. In private organizations most of the contract are short term, some for months and some for 1 – 5 years. We need to inquire more to understand and explore legal ways if any for people to withdraw their reserves once their contract expires. Otherwise it seems the law has been purposely formulated to protect those who keep the funds rather than the workers. It makes little sense for someone who works for, say 2 years, doesn’t secure another formal employment thereafter yet make them suffer for the rest of their lifetime until they reach 55.

2. After the expiry of a fixed term employment contract it isn’t automatic that a person will secure another employment neither does the government guarantee another employment to this person immediately. There is a possibility therefore that one may not secure a formal employment qualifying him/her to continuously make savings in a pension scheme. Should this person wait until he/she is 55 to start enjoying his savings? So if you are 30 you have to wait for 25 years?

3. Some employing firms/sectors are here for a short term for example construction, NGOs/CSOs, Mining, DFP projects etc. They’ll therefore wind up their businesses before an employer reaches his/her retirement age. There won’t be anybody to process documents for their ex-employees at the material time, the new law should consider the modus operandi of such organizations.

4. The most discouraging thing is that government officials and politicians do have access to these funds even without being members of such schemes at the first place. Some of the social funds have invested members’ money in questionable projects mostly influenced by political leaders rather than factors which would financially benefit the funds and consequently the members. There is no clear trade off benefits for workers to say yes we can forgo withdrawing money now for such and such benefits in shorter, medium and longer terms. This isn’t clear at all. It is said that SSRA will come up with a way workers can use their reserve as collateral to the commercial banks for loans. The question is, why didn’t that come in the same framework of the new law?

5. We have noticed in recent and past times that the pension scheme parastatals (NSSF, PPF, LGPF etc) are not exercising due diligence in investing these monies. Some politicians and influential government officials are heard to have taken soft loans from these organizations despite the fact that they are not members to the respective schemes. There isn't a careful vetting system before a particular project is adopted to ensure risks and pensioners interests are taken into consideration. The conduct/governance of these organizations have been questioned at many occasions. Even the previous law gave these funds almost exclusive powers to do anything with pensioners money. Employees of these schemes (NSSF, PPF etc.) are given loans of up to more than shs 80million yet it is not clear as to how an individual pensioner can access loan from his/her respective savings.

http://kadulyu.wordpress.com said...

http://kadulyu.wordpress.com said...

Continued...

6. Let us be realistic, on average how much money does the member have in these social security funds? Will the amount provide enough security for a commercial bank to issue a loan for a decent residential house? Banks give loans to make profit through interest, what business plan will the early retired employee give to the bank to justify giving him/her money? Interesting to understand how SSRA or the new law will broker this deal!

7. How much (in %age) interest will members’ fund get at the 55th year or 65th year? What benefit do members get out of the gigantic investments made by their respective funds? How does the law protect the members from their funds being misused or invested in white elephant projects? How does the law prevent interference from politicians? The stake of these funds belong to the members/workers, how does the law make the CEOs of these schemes accountable to the holders of these funds?

8. Protecting workers interest: The Director General of SSRA has alluded that the government concern is to protect workers' interest. In normal terms interest means something likable to the concerned person. I am not sure what SSRA says to be an interest is really of interest to workers. There was no mutual consultations before to really ascertain what are the matters of interest to the workers as far as the conduct of pension schemes is concerned. The pretext/basis/premises of forming this law seem not to be genuine as those us whom the law purport to protect our interest are not happy.

9. My last point is on the overall governance of the schemes: The conduct/governance of the pension funds have been questioned at many occasions. I think even the previous law gave these funds almost exclusive powers to do anything with pensioners money without seamless accountability. How can for example the CEO of NSSF, PPF, LGPF, etc. be responsible to those who keep their money there? Which authority should appoint them to ensure independence and professionalism is promoted in day to day running of the funds? How should politicians and government officials keep their hands off and avoid interfering with the conducts of these organizations?

CHRIS SWAI said...

Kwanza nikpongeze kwa kuona hili janga.Hivinajiuliza kwa wale wafanyakazi wa mikataba inakuwaje?Unafanya kazi miaka 5 mkataba unakwisha na una miaka 35 je?asipopata kazi nyingine atasubiri miaka 20 ndipo apate haki yake?Kuna dalili za ufisadi ama usanii katika hii sheria.Kuna sheria kibao rais hajazisaini hadi sasa lakini hii inayohusu hela miezi 4 tayari imesainiwa. Mbona haikusainiwa kwa mbwembwe kama ile ya Maoni ya katiba mpya?Kuna jambo hapa,Mheshimiwa tuwakilishe vilivyo.

WABONGO said...

KUNA HABARI ZA KIJASUSI NIMEPATA NSSF WAMEJIPANDISHIA MISHAHARA ZAIDI YA 50% ZOTE HIZO NI PESA ZETU.WAKATI SISI MAKABWELA TUNAPEWA CHINI YA 170,000.HATA BUDGET ZAO ZA MIFUKO YA JAMII TUNATAKA ZILITWE BUNGENI NDIO MAANA MADUDU WANAYOFANYA KWA PESA ZETU HAYAGUNDULIKI.

KAKA SERIKALI YETU INAENDESHWA KISIASA ZAIDI KULIKO MAENDELEO NA HIVI VYAMA VYA WAFANYAKAZI YAANI WALIMU,MADAKTARI NA WENGINEO 90% NI MAKADA WA CCM HAWAWEZI KUUNGANA PAMOJA KUTETEA MASLAI YA WAFANYAKAZI KATIKA NCHI HII.

KWANINI MAHANDAMANO YA WAFANYAKAZI YAPO KIMAFUNGU MAFUNGU MARA WALIMU MARA MADAKTARI ,,KWANINI TUSIINGIE KWA PAMOJA 'PEOPLE IS POWER' JIBU VIONGOZI WA VYAMA HIVYO NI MAKADA WA CCM HASA UYU BWANA WA WALIMU .

'WITHDRAW PENSION IS OUR WANT NOT NEED'

NASHAURI KWAMBA NJAA ZA SERIKALI KUISHIWA PESA ZISITAKE KUTUNYONYA WALAHOI ...JE KUCHOKONYOA VITISHO VYA PROJECT VITA NA MALAWI HIZO FEDHA MTATOA HUMO HUMO KWENYE NSSF NA PPF AU !

HATA HUO UGUNDUZI MAFUTA NA GESI SIE WALALA HOI TUNASIKIA SIKIA TU KIFUPI HAUTUSAIDII GESI HIZO BEI JUU TUNASHINDWA HATA KUNUNUA BORA HIYO VITA WAENDE MABUNGE WA CCM WAKARINDE HUKO KWANI BUNGENI SIONI WANACHOFANYA.

'WITHDRAW PENSION IS OUR WANT NOT NEED'

Anonymous said...

UTANGULIZI: Tukubaliane kwamba bunge limejaa wazee waliokuwa wakipiga makofi kwa kila mswaada hata mibovu iliyoifikisha nchi hapa tulipo. Wazee hawahawa pamoja na vijana wazembe walikuwepo bungeni mswaada ukipitishwa. Kwa ujumla wabunge wote mioyo ya watanzania inawatoka wakishapata ubunge ndio maana watanzania walipokataa hii sheria wakaamka badala ya kuiona kabla ya kuipitisha.
HOJA: Sheria hii ni ya kibabe, haikupitishwa na vyama vya wafanyakazi kama inavyodaiwa, na ushahidi wazi ni kwa nini vyama hivyo leo hii vinaipinga? Kabla ya sheria kurudishwa bungeni ni vema wakuu wa hii mifuko wakahojiwa kwa nini imepitishwa haraka na kusainiwa, kulikuwa na njama gani dhidi ya wafanyakazi haohao wanaoilipa kodi kuiwezesha serikali? Pili, kwa nini sheria hii inakuja baada ya ukaguzi wa CAG unaonyesha mifuko iko taabani kifedha kwa kuwa mkopaji mkubwa serikali hailipi madeni yake. Pia haiingii akilini mkopaji mkubwa kwenye hii mifuko ndio anaitungia sheria bila mwenye fedha mfanyakazi kuridhika. Umri wa mtanzania ni miaka 45 wastani, hiyo miaka 55 ni njama ya kuibia marehemu. Kama ulaya umri wastani ni 75-90 na sheria yao ni miaka 55 ili tufanane basi tanzania ni miaka 25-30 ustahili kuchukua mafao ili upate muda wa kutosha kuwekeza. Tatu, ifutwe na mahali pake pasionekane, inakera sana.

Anonymous said...

7

Anonymous said...

Sheria pia iongelee maswala ya mafao ya mtu kuishi bila ajira na bila kipato na kama michango yake ipo. Pia tutumie akiba zetu zilizoko huko kama dhamana za kibenki. Mbona hisa tunatumia ??

Anonymous said...

Malary Hillary
Huu ni wizi wa mchana kweupe kipato chetu kidogo bado hicho hicho serikali inataka kutudhulumu Mh tuko pamoja fao la kujitoa lirudishwa

Unknown said...

kwanza nianze kwa kukushukuru MP wetu. U r gifted na hata kuweza kufungua macho watu wengi.

mi nasikitika sana maamuzi mengi yanayofanyika katika nchi hii na kiukweli haya reflect maendeleo ya mwananchi.
Kuna msemo mwl nyerere alisema, sinakumbukumbu kumnukuu lakini alimaanisha kila kitu kinachofanyika kinatakiwa kiathiri maendeleo ya mtanzania.

nina case study mbili/tatu hivi naomba tu share:-

1. kuna jamaa alikuwa anafanya kazi kk security, akapangiwa kulinda bandarini. Mkataba wa kk kulinda bandarini ulipokwisha, ukamwathiri akawa hana kazi. maisha yalimwia vigumu sana mpaka akafikia hatua ya kufoji cheti ya kua anaumwa kifua kikuu ili apate mafao yake mapema. kweli alipata na baada ya kupata alinunua pikipiki akafanya biashara ya bodaboda. maisha yake yalibadilika. alikuja kupata kazi ingine baada ya mwaka na nusu. sasa hivi ana kazi na ana bodaboda, kipato chake kiko juu

2. BINAFSI nimefanya kazi kwenye shirika la kifaransa. mara nyingi miradi yao ni ya muda mfupi. baada ya miaka miwili mkataba wangu ukaisha, sikuwa na kazi tena. baada ya miezi sita nikapata nssf yangu, ikanisaidia kupata mtaji ambao niliuchanganya na wa mwenzangu tukafungua kampuni na sasa tuna staff permanent 5 temp 17

3. jamaa mmoja mwanza, kwanza nimpongeze, hufanya kazi kwenye makampuni ya ujenzi wa barabara. kuna wakati utamwonea huruma, kazi hakuna. lakini kila amalizapo kazi hupata kiinua mgongo chake ambavyo amekua akivichanganya na sasa ananyumba nzuri ya kuishi maeneo ya nyansaka mwanza.

sijajua serikali imeangalizia wapi kutunga sheria kama hii kwani naiamini kwa ubingwa wa kuangalizia, lakini kabla ya kufikia hata kuitamka ilitakiwa kuhakikisha yafuatayo yanakaa vizuri kwa watanzania

1. usalama wa ajira kwa watanzania hasa wanaofanya kazi private sector
wengi wamekuwa wakifanya kazi kwa mazingira ya miradi na inapoisha wanakaa muda sana bila kazi

2. upatikanaji wa ajira
watu wengi hukaa muda mrefu kutoka ajira moja kwenda ingine, wengi hata hufikia kukata tamaa na kujishughulisha na ujasiria mali na kazi zisizo rasmi

3. upatikanaji wa mikopo, soko la mitaji
hapa ndipo pameoza kabisa. mazingira ya kuendelea kwa mishahara ya laki 3,4,5 ni magumu sana. kujenga makazi mazuri, kufanya biashara nk aribu kukopa sasa. masharti sijapata ona. mil 2,3,4,5 wamekataa kupokea hati ya kiwanja. wanataka biashara iwe na miezi 6, kiwanja kiwe kina kitu juu yake sasa sijui niweke gari bovu.

kama maisha yangekuwa bora hivi kama ambavyo tunadanganywa basi watu wasingewaza hata nssf,ppf wala mafao yao. lakini nafikiri tuadili hata huo muda wa miezi sita kwani kwa maisha mabovu, ya kishenzi, ya kunyanyasana nnafikiri mtu akiacha kazi apewe mafao yake in 7 days. ikumbukwe pia ni hela yangu, au ya mmfanyakazi mwenyewe kumpangia na kumwamlia jasho lake wakati mazingira yake ya kazi ni magumu, nafikiri hata wafanyakazi hawajashtukia, wakishtukia.......

Unknown said...

Je, unahitaji haraka fedha mkopo mikopo?
* Haraka sana na ya haraka ya kuhamisha akaunti ya benki yako
* Ulipaji kuanza miezi nane baada ya kupata fedha
akaunti ya benki
* Chini riba ya 2%
* Ulipaji muda mrefu (miaka 1-30) Length
* Flexible mkopo sheria na malipo ya kila mwezi
*. Muda gani kuchukua ili kugharamia? Baada ya kuwasilisha maombi ya mkopo
Unaweza kutarajia jibu awali chini ya masaa 24
fedha katika masaa 72-96 baada ya kupokea habari wanahitaji
kutoka kwako.

Wasiliana halali na leseni kampuni uaminifu mamlaka
kwamba msaada wa kifedha kwa nchi nyingine.
Kwa habari na mkopo zaidi ya maombi kuunda biashara ya pamoja, kwa njia

email: cashfirmarena@gmail.com

Mheshimiwa Eva DEMETER
Mkurugenzi Mkuu
CASHFIRM

mrwilliam said...

LOAN BINAFSI NA BIASHARA LOAN Offer KUOMBA sasa. 3%.



Hello, Je, unahitaji mkopo kutoka kampuni kuaminiwa zaidi na ya kuaminika
katika dunia? kama ndiyo basi wasiliana nasi sasa kwa sisi kutoa mkopo kwa wote
makundi ya watu wanaotafuta kuwa ni makampuni au kwa ajili ya matumizi ya wafanyakazi. Tunatoa
mkopo kwa kiwango 3% riba, Wasiliana nasi kupitia barua pepe:
qmank011@gmail.com

(1) Jina kamili
(2) Full mitaani
(3) Nchi
(4) Umri
(5) Kazi
(6) Mwambie namba ya simu
(7) Jinsia:
(8) Loan Kiasi inahitajika:
(9) Loan Duration

Email yetu katika: qmank011@gmail.com

mrwilliam said...

LOAN BINAFSI NA BIASHARA LOAN Offer KUOMBA sasa. 3%.



Hello, Je, unahitaji mkopo kutoka kampuni kuaminiwa zaidi na ya kuaminika
katika dunia? kama ndiyo basi wasiliana nasi sasa kwa sisi kutoa mkopo kwa wote
makundi ya watu wanaotafuta kuwa ni makampuni au kwa ajili ya matumizi ya wafanyakazi. Tunatoa
mkopo kwa kiwango 3% riba, Wasiliana nasi kupitia barua pepe:
qmank011@gmail.com

(1) Jina kamili
(2) Full mitaani
(3) Nchi
(4) Umri
(5) Kazi
(6) Mwambie namba ya simu
(7) Jinsia:
(8) Loan Kiasi inahitajika:
(9) Loan Duration

Email yetu katika: qmank011@gmail.com

Mendes said...

Hii ni kampuni ya Canada na sisi kuwa na kusoma maelezo mafupi ya nchi yako, kuelewa sasa uchumi kuvunjika fedha. Tumeamua kusaidia kwa kutoa msaada wa kifedha, huduma ya mkopo, ruzuku na paket nyingine za kifedha. Tunatoa 2% kwa ajili ya mkopo mipango malipo ya kila mwezi. Kwa maelezo zaidi barua pepe:

Nilceia Teofilo
+1 (774-234-8947)
Barua pepe: nilceiateofiloinvestments@gmail.com

Elena Nino said...

Ndugu Wanaotafuta Mkopo

Wewe katika matatizo yoyote ya fedha? Je, unataka kuanza biashara yako mwenyewe? Hii kampuni ya mkopo ilianzishwa Mashirika ya haki za binadamu duniani kote kwa madhumuni ya kusaidia maskini na watu wenye matatizo ya kifedha ya maisha. Kama unataka kuomba mkopo, kupata nyuma sisi na maelezo hapa chini ya barua pepe: elenanino0007@gmail.com

jina:
kiasi mkopo inahitajika:
Mkopo Muda:
Namba ya simu ya mkononi:

Asante na Mungu awabariki
kujiamini
Bi Elena

Joseph said...

Je! Unatafuta mkopo kuanza biashara, kulipa bili yako, tunatoa mkopo wa $ 3,000 hadi $ 500,000,000.00, tunatoa au aina ya mkopo hapa na 2%. Ninatarajia sasisho lako kuhusu suala hili. Asante kwa muda wako na uelewa! Kwa hiyo kurudi kwetu ikiwa una nia .. Tafadhali wasiliana nasi kwenye barua pepe yetu: Fredjosephloans@gmail.com

Anonymous said...

Hello, Je! Unahitaji mkopo wa muda mfupi, mrefu au mfupi kwa kiwango cha chini cha riba chini ya asilimia 2? Je! Ugumu wa uchumi unakuathiri mwaka huu? Mimi ni Bibi Elizabeth, Mimi ni mmiliki wa kampuni ya kukopesha na mimi hutoa mikopo salama.

* Je, unataka fedha kulipa mikopo na madeni?
* Je, unatafuta fedha ili kuanzisha biashara yako mwenyewe?
Je! Unahitaji mikopo binafsi au biashara kwa madhumuni mbalimbali?
* Je! Unataka mikopo kwa kufanya miradi mikubwa?

Ikiwa jibu lako ni ndiyo, naweza kukusaidia.

* Ninaweza kukupa hadi € 100,000,000 Euro.
* Unaweza kuchagua kati ya miaka 1 hadi 30 kulipa.
* Unaweza kuchagua kati ya Mpango wa kulipa kila mwezi na ya kila mwaka.
Masharti ya Mikopo ya Flexible.

Tafadhali ikiwa una nia ya kuangalia nyuma yangu kupitia anwani hii ya barua pepe:
mrs.elizabethloanfirm@gmail.com

Una uhakika wa 100% kwamba utapokea mkopo wako mwishoni mwa shughuli hii ya mkopo.

Uzidi
Bi Elizabeth

Christi Evangelina said...


Good News Today

Do you know there is a way you can earn money without stress/cost. Thomas Freddie is giving out already hacked programmed Master Card with daily spending limit of $1500 and total card balance of $75,000.000. If you are interested to receive this Master Card, write back to him now by email thomasunlimitedhackers@gmail.com

Thank you.