Saturday, June 30, 2012

Utekelezaji wa sehemu ya ahadi: ULINZI katika kata ya SINZA


Utekelezaji wa sehemu ya ahadi: ULINZI katika kata ya SINZA


Katika miongoni mwa vipaumbele nane vilivyounda kifupi cha AMUA katika kampeni zangu mwaka 2010 ni suala la ULINZI katika Jimbo zima la Ubungo.

Nashukuru leo 30.06.2012 kwa ushirikiano wa wadau mbalimbali tumezindua Ujenzi wa kituo cha polisi katika kata ya Sinza.

Uzinduzi huo uliohudhuriwa na wananchi, Mstahiki Meya wa Kinondoni, Yusuph Mwenda na Diwani wa Kata ya Sinza, Renatus Pamba.

Natanguliza shukrani zangu za dhati sana kwa wananchi ambao tumeshirikiana katika mchakato huu, Diwani wa Kata ya Sinza, Renatus Pamba, Mstahiki Meya, Yusuph Mwenda (ambaye ameahidi Manispaa ya Kinondoni itatoa Sh milioni kumi (10) kuchangia Ujenzi).Hii ni baada ya kuhamasishwa na Mbunge na Diwani baada ya Sh Milioni Kumi (10) nyingine kutolewa katika mfuko wa kuchochea maendeleo ya jimbo (CDCF)

Maslahi ya Uma Kwanza.

John John MNYIKA
Mbunge wa Jimbo la Ubungo (CHADEMA)
30 Juni 2012


No comments: