Wednesday, December 29, 2010

Mnyika awaanzia yatima mfuko wa elimu

Mbunge wa Jimbo la Ubungo,(Chadema), John Mnyika ameanzisha mfuko wa elimu utakao wasaidia watoto yatima katika jimbo la Ubungo na ameahidi kuweka asilimia 20 ya mshahara wake kwenye mfuko huo.

Alisema hayo jana jijini Dar es salaam alipo kuwa anatoa msaada wa shilingi 100,000 akishirikiana na Ubungo Development Initiative (UDI) waliotoa vifaa vya shule na chakula katika kituo cha kulelea watoto yatima cha Boona-Baana Center for children kilichopo Sinza Mori jijini.

"Watu wengi wanafikiri kuwa mahitaji makubwa ya watoto yatima kuwa ni mavazi,chakula,makazi na kuwatembelea wakati wa sikukuu ila mimi naona sisahihi kabisa, elimu ni kitu cha muhimu sana kwani itawasaidia baadae,"alisema Mnyika.

Mnyika alimpongeza mratibu wa kituo hicho, Marco Barra kwa kuweza kuwasomesha watoto hao ili waweze kujikomboa kimaisha.

Alitoa wito kwa Watanzania kuwasaidia watoto yatima ili waweze kupata elimu itakayo wasaidia kujikomboa kimaisha.

Chanzo: Nipashe 27/12/2010

No comments: