Thursday, October 21, 2010

Tawi la Nyerere(CHADEMA) katika matawi ya NATO na Kosovo ya CCM na CUF
Kama ishara kuu ya kumuenzi Mwl.J.K.NYERERE siku ya Oktoba 14, 2010 nilizindua tawi la CHADEMA maeneo ya Manzese Bakhressa kwa jina la Mwl. Nyerere. Tawi hilo likiwa eneo sambamba na matawi ya vyama vingine vya siasa nchini yaliyopewa majina kama NATO na KOSOVO.

Nikifungua bendera ya CHADEMA na ipepee kwa wananchi wote ikisimamia ujumbe uliobebwa katika bendera hii ya CHADEMA. Ujumbe mzito na muhimu kwa Taifa zima la Tanzania

Hili ndilo Tawi la Mwl.J.K.NYERERE eneo la Manzese BakhressaWananchi wengi sana walisitisha shughuli zao na kujumuika nasi katika tukio muhimu sana la kidemokrasia kufungua Tawi la Mwl.NYERERE eneo la Manzese Bakhressa


Peopleeeeeeeeeeeesssssssss.......Poweeeeeeeeeeeeeeeeeerrrrrrrrrrrrrr!!!!!!!!!!!!!

1 comment:

Jacob Malihoja said...

Finally you made it!

Hongera sana mdogo wangu, na rafiki yangu. Mungu akujalie uendelee kuwa shujaa na mtu wa watu.

Ninakuamini kuwa utawatumikia vizuri watu wa ubungo, ninakuamini kuwa wewe ni mtu wa watu, mtu wa kutetea na kupigania watu wanaohitaji.

Sisemi mengi ila nakukumbuka miaka 10 iliyopita ulipofika ofisini kwangu na kuomba scholaship ya wanafunzi 10 wajifunze Computer!!

Ulikuja na hoja za msingi, na vijana hao 10 walipata mafunzo ya Computer bure kutokana na juhudi zako... nasema nakuamini! wasiokufahamu wanaweza kusema unafata mkumbo.. lakini mimi nimefahamu juhudi zako na uwezo wako wa kuwapigania watu tangu hujawa mwanasiasa (Sikumbuki kama tayari ulishakuwa umeingia kwenye siasa wakati ule).

Unastahili.. nawapongeza pia wana Ubungo kwa kupata mpiganaji mzuri wa maendeleo!

Best wishes!