Tuesday, October 5, 2010

Vijana wasomi waungana na harakati zangu kuelekea ushindiNiliweza kuongea mengi sana ya msingi kwa maslahi ya wanafunzi na vijana kwa ujumla. Nikifafanua kwa kina hususan kisera na mkakati namna gani nitatekeleza vipaumbele vyangu nane kwa wananchi yaani kwa ufupi "AMUA"; Akili, Ajira, Miundo mbinu, Maji, Uwajibikaji, Usalama, Afya na Ardhi


Nilihamasika sana na utulivu, hamasa na ushiriki hai wa wanafunzi wengi waliojitokeza katika kongamano ambalo waliliandaa wanafunzi wenyewe.


Dkt.Kitila Mkumbo, aweza kushiriki na kuichambua kwa kina sera makini ya chama chetu cha CHADEMA. Miongoni mwa mengi ya msingi aliwaasa vijana kuwa wao ni chachu ya mabadiliko, lazima washiriki bega kwa bega kuhakikisha MNYIKA anashinda kwa kuwa hata kabla ya kuwa mbunge amekuwa mstari wa mbele kuwa sauti yao-kuhakikisha anatetea maslahi ya wanavyuo na vijana wa Tanzania kwa ujumla. Hivyo ni wasaa wao kupata mbunge ambaye atakuwa karibu zaidi nao.


Alikuwa miongoni mwa wanawake wachache makini ambaye hakusita kuhimiza wanawake wajitokeze kwa wingi kuniunga mkono sambamba na hilo wanaume wahakikishe wanawahamasisha dada zao wa mama zao kujitokeza kushiriki katika kampeni na hatimaye kupiga kura

Licha ya Kongamano kuwa ni kwa wanavyuo, Kijana huyu alinihamasisha sana kwa kushiriki kwake ingawa ni mwanafunzi wa Sekondari. Chachu ya mabadiliko inamea na vijana wengi wakisimamia mabadiliko hakika Maslahi ya Umma yatafikiwa.

No comments: