Tuesday, June 19, 2012

Msimamo wangu wa sasa juu ya Kauli yangu bungeni!


Nitatoa tamko la kina baadae kuhusu kilichotokea lakini kwa ufupi ubovu wa bajeti hii ni matokeo ya udhaifu wa Rais Kikwete, yeye ndiye aliyesaini Mpango wa Taifa wa miaka mitano kama Kiongozi Mkuu wa Nchi tena kwa wino mwekundu kama Amiri Jeshi Mkuu. Na yeye ndiye Mwenyekiti wa baraza la mawaziri, bajeti hii iliyoacha kuzingatia mpango wa Taifa imepita kwenye baraza alilloliongoza, pia kushindwa kutekelezwa kwa bajeti iliyopita ni matokeo pia ya udhaifu wa taasisi ya Urais.
 
Pia kwa mujibu wa Katiba Rais ndiye ambaye anapeleka bajeti bungeni, Waziri mwenye dhamana anapeleka tu kwa niaba. Rais amepewa mamlaka makubwa juu ya bajeti ibara ya 99 imeweka mipaka kuhusu mambo ambayo bunge lina mamlaka nayo huku ibara ya 90 inasema bunge likikataa bajeti rais ana mamlaka ya kuvunja bunge. Hivyo Rais Kikwete anapaswa kuagiza Waziri wa Fedha bajeti iondolewe irudi kwenye baraza la mawaziri ikafanyiwe marekebisho!


John Mnyika
19 Juni 2012

70 comments:

Anonymous said...

tunapoelekea watanzania sijui....................

fidelis said...

viongozi wasomi hasa wana sheria wana mchango mkubwa wa kueleimisha umma nakubaliana nawe kwa dhati

Anonymous said...

mmh..!!?Nchi inaelekea kuzimu

Anonymous said...

HAPO NA WEWE SASA UMEPOTOKA, TULIKUAMINI SANA KUMBE NA WEWE NI POM POM KAMA ALIVYOKUWA MBUGE WETU MUNGU MBARIKI LEMA.

Kagaruki said...

Pole kwa kutolewa bungeni leo, nasuburi maelezo ya kina hapo baadae. Tupo pamoja.

Anonymous said...

Pole,misimamo pia yahitajika kuonesha msisitizo kwamba tumechoshwa na "upuuzi" na "udhaifu" za wazi.
Mungu bariki juhudi zote za kuleta mabadiliko na maendeleo...

Kisaka said...

Mimi nakupongeza kwa kusema ukweli na kuusimamia.Kumwita mtu dhaifu wala sio tusi,alichopaswa kukuhoji Ndungai ni ufafanuzi wa Rais ni dhaifu katika kitu gani.
Wasichojua ni kuwa kwa kukutoa nje wameipa hoja yako kuwa Rais ni dhaifu kupata uwanja mpana wa majadiliano na hapo ndio watakapojutia kwa papara zao za maamuzi.

Anonymous said...

upo sahihi na wala sioni kosa lako..M4C (MOVEMENT FOR CHANGA)

Anonymous said...

Ulikua na hoja ya maana bt kukataa kuliondoa lile neno ili uendelee na hotuba ako kuna kujuisha nawewe kwenye kundi la machzi,kanuni zote za bunge ziko wazi sikutegemea wewe tena ulie mwanasheria ufanye yale

Anonymous said...

mimi ndo maana sishabikii siasa,nyie wote ni wanafiki tu,wewe ni mmoja ya wabunge niliokua nakuona ni mstaarabu sasa hizi lugha za kejeli na kuchukiza sijui ulilala wapi,angalia umaarufu huja na kupotea kwenye mambo ya ivi ivi,huwezi kumkashifu rais mi nikushabikie hata kama ana mapungufu yake kama mwanadam

Anonymous said...

Well done mkuu, we will fight mpaka kieleweke. Tupo pamoja

Anonymous said...

Mbona mi sioni kosa katika hii speech? Au waliomtoa nje jembe wana hang over ya rangi za kijani?

David said...

Thats it Mnyika..hatuwezi kila mwaka kitu hichohicho tunajadili bila mafanikio...we are backing u in every move cammander...

Anonymous said...

kaka angalia ya kuzungumza kwani haujiwakilishi wewe Pale una wakilisha wananchi wa jimbo la Ubungo kumbuka sharia zipo na uangalie zinazokubana.......

Anonymous said...

This is proper Bullshit. Mr are you after a publicity stunt or something okay you now have a stupid record of being kicked out of the parliament. Bajeti ya kipuuzi How dare u say such a thing to a national concern. I support the fact that u wer kicked out pure crap

Anonymous said...

hakuna mwanadamu asiye na udhaifu sasa hapo tusi liko wapi? Ila usirudie tena watakufanya kitu mbaya wale machizi

Anonymous said...

Kuna Mtu aliyekamilka asilimia Mia ? Hata rais ana udhaifu yeye si mungu

Hillary E. Sandagila said...

Siku zote huwa nasema kuwa hakuna mtu aliye mtanzania kuliko watanzania wengine kwa kile alichokifanya Mwigulu jana na hiki alichofanya Mnyika leo kwa mtazamo wangu Mwigulu alistahili kuadhibiwa kabisa lkn nyinyiemu wanalindana ktk mambo ya kipuuzi ndo maana tunafikia hapa tulipo. Uongozi wa Bunge ubadilike utoe haki sawa kwa wote.

Anonymous said...

HONGERA MNYIKA ULICHOKISEMA NI KWELI KABISA,WATANZANIA WANAFIKIRI RAIS NI MUNGU LA NI BINADAM KAMA MIMI NA WEWE,ULAYA TUMEZOEA RAIS AU WAZIRI MKUU AKIVURUNDA NAYE ANAPASHWA HAPO HAPO,UNAJUA CCM WENGI WANAFIKI HATA HUYO ALIYEKUTOA NDANI YA BUNGE NAAMINI KABISA MOYONI KWAKE YUPO NAWE ILA UTARABITU WETU NDIYO ULIYO MFANYA AFANYE HIVYO,NA HUENDA RAIS MWENYEWE YUPO NAWE BAJETI BOMU HIYO:TUPO PAMOJA NAWE
YA JANA WAMESAHAU YULE MWIMBAJI WA KWAYA ETI ANADAI WABUNGE WAPIMWE YEYE MZIMA ANAJUA NINI ZADI YA CCM
TANZANIA INATAKA WABUNGE WANAOKWENDA NA WAKATI HUSUSANI NA MAENDELEO YA ULAYA ,MAREKANI NA DUNIA NZIMA, ´WABUNGE WENGI WA CCM WAMEZOEA IMEPITA HIYO,

Unknown said...

Kuna haja ya ukatafakari vizuri kutokana na kauli yako, mbali na watu wanaoshadidia tu bila ya kujua kanuni na sheria zake za bunge zinasemaje kuhusu hilo.

Unknown said...

Kijana umetumwa na wananchi uende kuleta maendeleo kwa ajili ya jimbo lako na tanzania kwa ujumla, sasa kwenda kumuongelea mheshimiwa rais kana kwamba ni mtu tu kama vile wa mtaani kwa kweli umekosea na ndio maana hata mheshimiwa naibu spika imebidi aangalie sheria na kanuni za bunge zinasemaje kuhusu hilo na kutolewa nje, inabidi uwe na nidhamu hata kama unaenda kufanya mema kwa watanzania.

Unknown said...

DOGO MNYIKA UMEKOSEA SANA NA INABIDI UOMBE MSAMAHA NA UFUTE KAULI YAKO, KWASABABU KANUNI NA SHERIA ZIMEKUBANA. KUWA MWANGALIFU TUNAKUAMINI UTATUSAIDIA SANA KATIKA KULETA MAENDELEO LAKINI KATIKA KUFUATA KANUNI NA SHERIA BILA YA KUMDHIHAKI MTU YOYOTE.

Unknown said...

I wish you could wear President shoes then ungeelewa wewe Mheshimiwa Mnyika, neno dhaifu tena unaongelea kama vile kitu cha kawaida sana kwa Amiri Jeshi Mkuu mbele ya umati wa watu ambao wengine walikuwa wakikusikiliza kupitia radio na wengine kupitia televisheni na wale waliokuwapo pale Bungeni! Umechemka Mheshimiwa Mnyika inabidi uwe makini sana na kauli zako ndio ushauri wangu kwako.

Unknown said...

MSIOJUA UTAWALA WA HAKI, SHERIA NA KATIBA KAMA ANAOHUFUATA MHESHIMIWA RAIS NDIO UNAOWEZA KUWAPA JEURI KAMA KINA MNYIKA KUWEZA KUMDHIHAKI HATA YEYE AMIRI JESHI MKUU, LAKINI TUKUMBUKE KWAMBA HASUNGEFUATA HUO UTARATIBU AMBAO WAO KINA MNYIKA WANAMUONA DHAIFU SIDHANI KAMA HATA UBUNGE ANGEPATA, KWA HIYO KUNA HAJA KUBWA SANA YA KUMHESHIMU MHESHIMIWA RAIS KWASABABU YEYE NDIO AMEWEZA KUTOA UHURU KAMA HUO AMBAO SASA INAVUKA MIPAKA.

Unknown said...

Mnyika umemkosea Rais. huo sio ujanja badilika.

Unknown said...

I THOUGHT YOU ARE THE YOUNGEST POLITICIAN WHO HAS A VISION JUST LIKE HON. ZITO, BUT TODAY'S YOU HAVE SHOWN SOMETHING STUPID IN YOU WHICH PEOPLE WHO HAS WISDOM WONT TAKE IT. YOU ARE A CRAP!

Anonymous said...

udhaifu wake ndo umekufanya uvunje sheria za bunge kwa maksudi? ki ukweli ulikuwa ni miongoni mwa wabunge wanaoheshimika lkn kwa hilo umejiharibia reputation . .

Anonymous said...

Safi sana Kamanda....M4C..Walioona kwamba umefanya kosa kutamka kauli ile hao ni wafuasi wa CCM..wala hujamkosea Rais UKWELI UNAUMA jamani ndiyo maana mwasema kafanya kosa..embu mwachen Mbunge wetu..pamoja sana Kamanda Mungu azidi kukupigania na kukuinua ktk kazi zako za kuitetea jamii..Jackie

Anonymous said...

You are right John! No need to apologize that is a true political feedback.

Anonymous said...

keep go on my dia no need of apology! just prove to them.

Anonymous said...

sioni TATIZO LA MANENO YA MNYIKA MAANA SI TUSI WALA SI UCHOCHEZI ILA NI UKWELI ILA TATIZO LA KUWAFANYA WATU WENGINE MIUNGU WATU

Neilson said...

I am good fan of you Hon Mnyika, my belief on what happened today is that you used political rally language(lugha ya kisiasa) katika wrong platform.Ungetumia lugha kama Mhe raisi amekua mpole,si mwepesi kuchukua hatua, au hata anaendesha seriali kisiasa zaidi, mgumu kuchukua au kutoa maamuzi magumu kuliko kupiga eti ni mdhaifu, maana waosha vinywa sasa wamepata cha kuongea, be reasonable naamini you were provoked, call the president and apologize tuanze tena upya.Utajijengea heshima mbele ya Chama chako as you dont have to lower yourself to mwigulu's and komba level. Lugha hii kali na direct tupeleke kwenye mimbari ya operation sangara na M4C. Salute Kijana

Anonymous said...

Ni kosa kubwa kumwogopa adui au mpinzani wako bila kikomo.Nyerere na mashujaa wetu wangekuwa na uwoga enzi hizo usio na kikomo mpaka leo wakoloni wengekuwepo mpaka leo.Mnyika umeonesha njia.

Anonymous said...

KAMA KUNA KOSA KUBWA UTAFANYA MNYIKA NI KUPOKEA USHAURI WA WANAOKUOMBA UOMBE RADHI. MACCM HAYANA RAFIKI. WASIKUDANGANYE HAWA, HATUJAKESHA WOTE KULINDA KURA ZAKO UBUNGO. KOMAA TU MBONA LISSU NA MSINGWA WANACHUKIWA SANA NA MACCM HAYA LAKINI HAWAJAPUNGUKIWA TU.

Anonymous said...

M***kers Don't know what freedom of Speech means?

F**k CCM and their crap we are all f***cked up cause of their f**in Crap Shit !

Those who thinks U should apologies are Crazy..

BABA J said...

MHESHIMIWA MNYIKA HIO NI TISHIA NYAU KWA MTU MZIMA. HAO KINA NDUGAI NA MAGAMBA WENZIE WATAKUJA WAO KUKUOMBA MSAMAHA ILA WEWE KOMAA. RAISI WETU KWELI KABISA NI DHAIFU SANA NA HATA MTU ASIYENA ELIMU KUBWA ANALIONA HILO. SERIKALI NZIMA DHAIFU SANA

Anonymous said...

adhaifu sio tusi, wanaambiwa soccer players, teachers na watu wengine hata kuna wabunge ni dhaifu kusimamia ukweli sio sababu ni raisi asiambiwe hii sio sahihi anapoambiwa anapokosea ndo kutatua kero zenyewe ni mara kikwete hatoi kauli kama rais huo ni udhaifu mnyika yupo sahihi
lissu aliandika barua kwenye kamati ya bunge ya uongozi kuhoji upendeleo wa spika kwa hoja za upinzani huo pia ni udhaifu wa spika kutosimamia ukweli na kuibeba ccm.
mtu yeyote aweza kuwa spika

suke suke waq mbele said...

MABADILIKO YA KWELI HUANZA NA WACHACHE KISHA WENGI....TUNAPASWA KUTAMBUA KWAMBA HIZI SI ZAMA ZA ENZI ZA MWALIMU, PIA RAIS SIO MUNGU.....[ONE DAY YES!!!!!!!]

Anonymous said...

safi sana bora kuwawashia moto wamezidi uzembe hao wizi tu ndio wameweka mbele kujali maslahi yao bila kutazama shida za wananchi mwendo ni jino kwajino hakuna kuwapa upenyo tuko pamoja kaka mnyika

Anonymous said...

Kwani ni nini maana ya neno dhaifu?sio tusi na ni kweli rais wetu ni dhaifu. Mfano chenge na vijisenti huko jersey island,mkapa na makaa ya mawe,hela za EPA..na mambo mengine kibao. Kama rais wetu asingekuwa dhaifu tungekuwa na majibu ya japo hayo machache

Anonymous said...

Hongera Mh. Mbunge, kamwe usichoke wananchi tunautambua mchango wako, kwani ni nyinyi ndio watetezi wetu sisi wanyonge.
Mungu akubariki, ukirejea bungeni wembe ni ule ule.

Mungu Ibariki Tanzania

Anonymous said...

Hongera Mh. Mbunge, kamwe usichoke wananchi tunautambua mchango wako, kwani ni nyinyi ndio watetezi wetu sisi wanyonge.
Mungu akubariki, ukirejea bungeni wembe ni ule ule.

Mungu Ibariki Tanzania

Anonymous said...

KWANZA MHESHIMIWA NDIO NINI, UJINGA HUU NDIO MAANA UNAWWEKA DHANA YA KUTOKUMHOJI NA HATA KAMA TUMEMPA KAZI NA AMEKOSEA. WALE KUNA BAADHI YA WATANZANIA NI WAPUMBAVU SASA NI KIPI HATUMUELEWI MBUNGE HAPA?. MBUNGE KASEMA RAISI ALIPITISHA MPANGO KAZI AKASEMA KWA MIAKA MITANO NITAUFANYIA KAZI, SASA LEO ANALETEWA BAJETI AMBAYO HAIONYESHI KUTEKELEZA HUO MPANGO KAZI ALIOUSAINI NA YEYE ANAUKUBALI HUO SIO TU NI UDHAIFU NADHANI MBUNGE UNGESEMA NI UPUMBAVU WA RAISI. TUCHUKUE MFANO WA SERIKALI ZETU TUNAZOZIONGOZA MAJUMBANI LEO UNAWAPA NAFASI NYUMBANI WAKUELEZE TUFANYE NINI KWA MIAKA MIWILI IJAYO, WATOTO WANADAI WANATAKA KUSOMA, MAMA ANASEMA ANATAKA KUFUNGUA BIASHARA YA KUKU, KUNA BAJETI YA CHAKULA KWENDA SINEMA, SASA UNAKUBALIANA b

Anonymous said...

Warioba


NA MIPANGO AMBAYO FAMILIA IMEKULETEA, UNAWAAMBIA WAKAKULETEE BAJETI YA HAYO MATUMIZI KWA KUWA WEWE NDIYE UNAYEGAPA naendelea ilikatika.. NAO KWA KUWA WEWE NDIYE UNAYETOA MAFUNGU YAANI PESA, UNAWAAMBIA WAKALETE BAJETI BAADAE WANARUDI NA BAJETI UNAKUTA MAMA ANATAKA KWENDA HOLIDAY, ANATAKA MAFUTA YA GARI,WANATAKA KIYOYOZI KILA CHUMBA ETC, UKIWA KAMA BABA UNATAKIWA UHOJI KULIKONI ULE MKAKATI UMEFIA WAPI.? BADALA YAKE UNAKUBALIANA NA PUMBA AMBAZO FAMILIA YAKO IMEKULETEA! LAHAULA NADHANI WEWE UNAKUWA NI MGONJWA WA AKILI


Warioba

Anonymous said...

Daaah ebwana mkuu saaaaaafi sana... kwa kweli hapa nchini tulipofika tunahitaji viongozi wenye msimamo.. na uwezo wa kuiteteta nchi na kufichua maovu yote yanayoendelea... we kaza buti song mbele na wala usipate shida tupo pamoja kwa lolote lile hata kama ni muhanga...

Anonymous said...

Hello Mheshimiwa Mnyika, sikufurahi kwa yaliyotokea. Nafikiri utumiaji wa neno dhaifu hata kama unafikiri una maelezo yake mazuri vipi ungelifuta maana ujumbe ulishafika na watanzania walishasikia ulimaanisha Udhaifu. ambacho ungefanya ni kulifuta. Umeshajua CCM wanabebana Bungeni, sasa huna haja ya kupunguza nguvu na nafikiri ulikuwa na hoja nzuri sana. ungetumia maneno ya kidiplomasia kumaanisha neno hilo hilo dhaifu....kwamba ni mpole kushindwa kufuatilia ...yuko busy sana .... ana mambo mengi na wanamwonea watu aliowaamini na maneno kama haya....ujumbe ungefika kama neno "dhaifu". Huna haja ya kulitolea maelezo ulosema badala yake apologize na tumia lugha ya kidiplomasia kurudisha hali ya upepo....Mungu bariki BUNGE na Wape hekima wabunge na uongozi wake!!

Anonymous said...

UNAHAKI, UNANGUVU, UNANAFASI, UNAULINZI NA HATA UKISEMA KWA UZURI WA NAMNA GANI NENO (DHAIFU) LITABAKIA NA MAANA ILEILE. WALISHATUMIA NJIA NYINGI SANA KUSEMA NENO HILO, NA KAMA HAWAKUWEZA KUSIKIA NI BORA LISEMWE WAZI KABISA ILI WASIKIE LIKITOKA NENO KAMILI KULIKO KUZUNGUKA MBUYU.
"RAHISI KUZUNGUKA MMBUYU ILA KUUKUMBATIA SI RAHISI" WATANZANIA NI WANAFIKI KUPINDUKIA NDIO MAANA HATUENDELEI, FANYA KAZI KWA KADRI YA UTASHI WAKO NA SIO MARA YA KWANZA KULISEMA NENO HILO. LABDA TU UMELISEMA AMBAPO WANAWEZA KUKUCHUKULIA HATUA ILA UKWELI NI KWAMBAAAA "UDHAIFU HUO NDIO UMETULETEA BALAA ZOTE HIZI" MWENYE AKILI ANGEKUWA KASHALIONA NA ASINGESHANGAA USEMI WAKO. SIKULISIKIA HILI WAKATI WA UTAWALA WA MH. MKAPA, KWANINI SASA, KWANINI UTAFUTE NJIA YA KUSEMA HILO NA LINAWEZEKANA. CANT QUESTION WHAT YOU HAVE JUST SAID BECAUSE I CANT FIND THE PROPER WORD TO CALL THIS GOVERNMENT.

Dr. Kunda John Stephen said...

Dhana yako ni nzuri pia argument, lakini lugha yaweza haribu kila kitu. Hata maisha ya kawaida mtu waweza Kuwa na hoja nzuri lakini kauli zako zikadilute kila kitu. Tuna waomba wabunge wetu wawe weledi wa hoja na lugha hapo ni bungeni

ESTA said...

HAJAKOSEA KABISAAA MIMI NASEMA HAJAKOSEA KWA SABB RAIS NDIE MTENDAJ MKUU NA MWENYE MAAMUZI KIPI SAWA KIPI SI SAWA KIBADILISHWE KWANI HII NCHI HAINA GREAT THINKERS WA KUMSAIDIA rAIS HATA KAMA YUKO BUSY BWN?MBONA KELELE ZA WAPINZANI NDIO ZIMEFANYA BARAZA LA MAWAZIRI KUBADILISHWA TENA FASTA HAMKULIONA HILO NYIE MNAOBISHA?
2NDLY NAOMBA KUMWAMBIA MNYIKA ANISAIDIE KUNIJIBU KWENYE BAJETI HII SECTA YA MADINI IMEONGEZEWA AU KUPUNGUZIWA %NGAPI YA KODI?

Ng'hily Dickson said...

Mkuu Mnyika, kabla ya yote naomba ku-declare interest hasa kwa wale wasionifahamu. Mimi ni mwanachama na kada mwaminifu wa CHADEMA.

Baada ya hayo, naomba sasa niseme kuwa, bunge letu linakoelekea siko na actually hii inatokana na uongozi dhaifu wa bunge.

inasikitisha sana kuona viongozi wa muhimili huu wanasababisha unapoteza nguvu yake ya kuisimamia serikali na badala yake unaonekana upo kwa ajili ya kuitetea serikali.

Nimekuwa nikichukizwa na viongozi wa bunge kwa maana ya spika, naibu wake na wenyeviti kushindwa kusimamia vyema kazi zao na badala yake wanaonekana kuwa bias.

Nachukizwa pia na baadhi ya wabunge ambao badala ya kujadili hoja, wao wanaleta ushabiki wa vyama na hasa kuendeleza kampeni ndani ya bunge.

Nikirudi katika hoja yako, ndugu yangu mnyika, ni ukweli usiopingika kuwa Kikwete na serikali yake ni dhaifu. Na kwa mujibu wa kamusi ya kiswahi;

Neno dhaifu ni kivumishi

kwa kimombo ni;

1 weak, feeble, frail, sickly, deficient, shaky, powerless

2 spineless, decrepit

Tunaposema fulani yu dhaifu kwa kimombo tunawezasema fulani is weak

Kwa tafsiri hizo kutoka katka kamusi ya kiswahili, hakuna TUSI.

Udhaifu ni nomino
mfano mzizi dhaifu

Udaifu kwa kimombo wawezatamkwa kama frailty. Sasa hapo tusi au lugha ya kejeli iko wapi ambayo kwayo ulitolewa nje iko wapi!

Viongozi hawa wenye ufinyu wa kufikiri na kudhani ndo wajuzi sana, watatupeleka bapaya. Tena wasitake kutufikirisha kama wanavyofikiri.

Kamanda Mnyika, mwaka 2010 niliposema kuwa Kikwete hana adabu, watu wasiojua maana ya hilo neno, walinilaumu sana. Hata hivyo sijawahi na sitarajii kujuta kwa kuitoa hiyo kauli.

Heko kwa kusimama imara bila kuyumbishwa, na heko kwa kutokubali kufuta kauli. Tuko pamoja na tunakuombea Mungu akusaidie na akufanikishe katika kudai haki kwa niaba ya mtanzania....

MARRY said...

MNYIKA USIOGOPE TUPO PAMOJA ACHANA NA HAO WAZEE WANAOSUBIRI KUBEBWA TUU WANAFULIA WANARUDISHWA TENA BUNGENI UNADHANI WATAKUSUPPORT?WALISHAONA BUNGE NDIO MAISHA YAO KWA AJILI YA ALLOWANCE WENGI WAKIKOSA UBUNGE WITHN A YR WATAKUWA MAREHEMU,KWA HIYO NIA YAO SIO KUTETEA WANANCHI WALOWATUMA,WANAFANYA MAZOEA NDIO MAANA WANASEMA UTOTO UNAWASUMBUA CHADEMA HAKUNA KITU KAMA HICHO,TUMECHOKA KILA BAADA YA BAJETI EVERY YR VITU VINAPANDA BEI,SAIVI SODA ITAKUWA 750 AU 700 KM SIKOSEI,WANYONGE NDIO WANAOUMIA,AU WAMEONA HATA SOFT DRINKS NI LUXURIUS WAO WANAKUNYWA SODA HAO WAHESHIMIWA?KILA SIKU KODI INAPANDISHWA KWENYE SIGARA ,POMBE,SIMU,SIO WABUNIFU HAKUNA CHOCHOTE KIPYA?SIO WABUNIFUU NASEMA CCM WANABORE.

Anonymous said...

Suala la kuogopa au kutoogopa halituhusu... Mnyika upo makini kwenye mambo yako lakini kwa hili la Jana umechemsha. najua wewe ni mbishi sana lakini umeniudhi sana sana. Tafuta lugha ya kufikisha ujumbe... Nilishangaa kumuona Halima anakupigia makofi ulivyogoma kutengua kauli. Jamani hatutaki tabia hizo tunaomba michango yenu iliyoenda shule

Ebenezer Vetenary Choir said...

Wanaoona Rais hana udhaifu hao ni Dhaifu zaidi ya Rais tena machiziiiiii.Big up Mnyika

Anonymous said...

muheshimiwa nakupongeza kwa ujasiri wako na nia yako ya dhati unayoionesha ya kutetea maslahi ya wanyonge.sisi wananchi wako wa ubungo tunasema tuko pamoja na wewe in every step towards revolution.mungu akutie nguvu katika hili.

Anonymous said...

SAFI SANA MH. MNYIKA KWANI YEYE RAISI NI NANI MPAKA AKIKOSEA ASIAMBIWE MAMBO YA KIKOLONI HAYATAKI KWA MUDA HUU KWANI UNAPOSEMA KILA MTU ANA HAKI YA KUONGEA NI WAKATI WA KUWEKA MAMBO YOTE WAZI SASA KAMA RAISI ANAKOSEA LAZIMA AAMBIWE KWANI URAIS NI CHEO LAKINI UTU UITABAKI KUWA UTU DAIMA NA MAPUNGUFU YAKE GOOOOOOOOOOD....!!!!!!!!

Anonymous said...

Huu ni wakati wa ukweli na uwazi tafadhali Watanzania tuache mambo ya uogauoga na hii isiwe kwa raisi tu bali hata kwa viongozi wengine wakienda kinyume na maadili wawekwe wazi kwani tumuchoka akiiba waziri eti anajiudhulu lakini masikini akiiba heeeee atakiona cha moto na wakati wote ni binadamu sawa tubadilike ndugu zangu acheni uoga tuwe kama Wakina Mnyika tuweke mambo waziiii

Kev West said...

Kwani Mnyika ange apologise what would happen? Nothing, so hata wewe mnyika ni dhaifu because they say "Forgiveness is for the strong people, Weak people can't forgive" so wewe unge apologise, utoe hoja then ungekuja ku explain kwamba umeonewa au la. Simple like that.

Anonymous said...

Mnyika safi sana ulichokifanya, Unajua haya yote yanatokana na kile KITI hakitendi haki na kabisa hasahasa mh, Ndugai yaani simpendi huyu baba hajui kabisa kuongoza bora hata ya mh makinda anaafadhali kidogo, Ndugai anaonekana wazi kabisa alivyolalia upande mmoja, inamaana ccm hawaongei lugha za kuudhi?? mbona hatujawahi kuona wakitolewa nje?

Mh, angempa nafasi Mnyika aweze kuelezea udhaifu wa rais yeye anaanza kutoa maamuzi tu kisa ndio anongoza bunge mtu akitaka kuelezea anadai kiti kimeshaamu, na ndugai nakuhakikishia 2015 ndio mwisho wakuingia bungeni.....

Anonymous said...

Sa fi sana Mnyika kiongozi bora ni yule mwenye msimamo na sio wakupelekeshwa, kwani rais ni nani? hasiwe mdhaifu? na ni mdhaifu kweli huwezi kumcopare na maraisi wote waliopita.

Anonymous said...

Mtu mwingine ni huyo Lukuvi anajifanya huko makini sana na kitabu cheke cha kanuni wakati wapinzani wakiongea ila wa ccm humwoni akijifanya mwongozoooo kunakanuni, naye ni mdhaifu na mnafiki tu hana lolote kama huyo rais,

Na mimi naomba kiti kiwe kinatenda haki kama leo namwona mh makinda kaenda vizuri ngoja kesho akija hiyo iddi amini dada Ndugai na mimacho yake, hajui hata anachokifanya mtu akitoa ufafanuzi akilinganisha na juzi kilichotokea hutamsikia mimi sikuwepo, ndio hukuwepo lakini hilo bunge yapasw ahumsikilize kwa makini,

Mimi ni ccm ila ccm mnaboa sana wanachama wenzangu hamko fair kumbukeni mtakuja kufana mungu atawauliza mambo mliyokuwa manayafanya bungeni sio kkabisa

Anonymous said...

Mi mwenyewe ni ccm lakini nampango wa kuama kwenda chadema na nikwa ajili ya ndugai huyu sijui ni mchristu au mwisilamu ila nahisi atakuwa mchristu, na huwa anaenda church anasali nini? mbona hayuko sawa kabisa, anboa sana anapoendesha bunge yeye kwa sababu kama mtu wa ccm kaongea na kakosea halafu mtu wa chedema kaomba mwongozo anajifanya hasikiii kabisa au utasikia ntakupa nafasi buri kidogo.
ila kama ni ccm kaomba mwongozo ni hapohapo anampa nafasi
wewe ndugai naomba hubadilike kabisa, Mnyika nakupa pongezi zote na huyo ndugai najua nafsi yake inamsuta kwa kile alichokifanya

Kwa tahari nawaambia huyo mwesnhimiwa ndugai angejua anavyowapaisha wabunge kuwatoa nje, sasa mnyika katolewa nje kampaisha sana na tumejua ni kwanini kamtoa nje, ni kwaajili ya udhaifu wa ccm ukiongozwa na mkuu wao kikwete. Tumechoka kabisaaaaaaaaaaaaaa

Anonymous said...

Mnyika nakufagilia sana nakupenda kwa ungozi wako na nakupenda wew memwenye ulivyo, unamaamuzi ya kweli, unafaa kabisa kuwa baba wa watoto wangu,I wish............. da ila najua utakuwa na mtu ila kama huna da nitafute natamani kutoa namba ila wengi watanizinguwa nitakufata tu ukouko

Kazi nzuri sana uliyoifanya jana ila ningeomba utuambie ulichokuwa unataka kuchangia kozi walikuharibia mudi kabisa hawa wadhaifu, tuandikie hata kwnye vyombo vya habari najua huwa unakuwaga na mchango mzuri sana na point za huwakika

Anonymous said...

Mhe Mnyika , ulikuwa na ujumbe mzuri tu. na kila mtu anaelewa kuwa hakuna aliyekamilika/aliye timilifu.

Tatiozo ninaloliona na lugha,kwa mtu kama Rais ulitakiwa kutumia lugha ya staha. nadhani chukua hili kama somo kwako

Anonymous said...

Mimi natoka kwenye jimbo la Ndugai, jamani nakuomba kiongozi wetu sisi wananchi wako tunasikitika kwa kitendo unachokifanya bungeni hauongezi bunge kisawa kabisa unalalia upande mmoja waziwazi kabisa , hii inaonyesha ni jinsi gani mlivyokuwa hamana maamuzi mazuri jamani naomba uige mfano wa Mh. Sitta alivyokuwa, au unaogopa ktengwa kama sitta walivyomfanya? sisi ndio wananchi wako tunaokupigia kura please kuwa fair jamani ndugai watu wanakusema vibaya sana mi sipendi kwa sababu nakupenda ila unaniangusha,

Anonymous said...

KUNYA ANYE KUKU AKINYA BATA AMEAHRISHA. HAWA SISIEMU VIPI MBONA WAO HUWA WANASIMAMA NA KUTOA MATUSI NA KEJELI DHIDI YA WAPINZANI LAKINI HATUONI KUWAJIBISHWA, LAKINI MPINZANI AKITOA MANENO HAYO ANAWAJIBISHWA. MFANO MZURI NI JOHN KOMBA JUZI J3 BUNGENI ALIONGEA MANENO MAKALI KUHUSU WAPINZANI KWAMBA NI WAPUUZI NA AKAPIGIWA MAKOFI. INAKUAJE LEO DHAIFU IKAWA NI TUSI? KAZA BUTI MNYIKA

Anonymous said...

hivi jitu zima kama komba kutembea na kitoto kidogo kama(******)na kuongea upuuzi kama ule bungen nan anapaswa kupelekwa mirembe?????Mwigulu ni kijana asiyejua hatima yake ndan ya "fools CCM" let em wait 2015 tuone kama atakua na jeuri aliyonayo sasa, mnyika stick to your statement na kwakukutoa nje wameprove hw jakaya yuko weak tena inabidi tumchunguze vizur WAT A PREZDENT HUH?

Anonymous said...

Kwa mtazamo wangu hukupaswa kutumia lugha ya namna hiyo mheshimiwa naomba nikukumbushe...upo bungeni kwa ajili ya maslai ya wengi ila kwa kitendo chako kimepelekea hata hoja zako kutotiliwa mkazo na mwisho ukatolewa nje ya bunge...effect inabaki kwa wananchinani atawasaidia kufikisha matatizo yao?? nani atasimama kutilia mkazo maombi yao?? nani atasimama kupinga uonevu wao?? bajeti ina mapungufu ila urais hata kama ungepewa mwisho wangetoka wachache kuipinga bajeti yako ila cha msingi ni kuwa BUNGE liheshimike kwa tuliowatuma tunawaamini na kuwategemea ninyi kama mkifanya hivyo mtakuwa hamjengi bali mnabomoa

Anonymous said...

KIMSINGI NATAMBUWA WAZI KUWA SIRIKALI YA NYINYIEM NDO CHANZO CHA MATATIZO YOTE YANAYOMKABILI MTANZANIA WA SASA BILA KUPOTOSHA, NA MBAYA ZAIDI SERIKALI HIHI HAITAKI KUKUBALI MAKOSA PALE INAPOELEZWA UKWELI WA MAMBO NA BADALA YAKE HUJENGA CHUKI KWA KAMBI YA UPINZANI ZAIDI SANA INAZIDI KUKUMBATIA MADUDU AMBAYO KIMSINGI KWETU SISI KAMA CHADEMA NI FURAHA YA MKIZI. SISI TUWAACHENI WAFANYE WANAVYOONA WAO KUWA INAFAA LAKINI IFIKAPO 2015 NDIPO WATAKAPOJUA KUWA KACHUMBALI SI KITOWEO PEKEE KUMBE WAKATI MWINGINE HUTUMIKA KAMA NI MBOGA!

Ndelanzali said...

Kuna Mafala wengi sana wamepost utumbo kana kwamba hii ni enzi ya awamu ya kwanza wakati Rais alipokuwa Mungu mtakatifu. Mijitu kibao imeingiwa na MFADHAIKO wa akili eti kwa sababu Rais ameitwa Dhaifu.
If u didnt know now u know, our President, JM Kikwete is Weak and he is being used by people who know his weakness.The guy's upstairs is not well connected,he is out of touch and he is not aware of what is going on in his country.
All loosers are backing him simply because he resides at the most famous piece of real estate in Magogoni.
Well done Mnyika and you loosers Wake UP!

Anonymous said...

WATANZANIA NI WATU WANAFIKI SANA, SANA,SANA, NA KI-UKWELI UNAFIKI HUU NDIO UNAOTUFANYA TUSIENDELEE, NI UNAFIKI TU HAKUNA KINGINE. WATU WANALILIA MAENDELEO NA KIUKWELI WANAHITAJI HAYO MAENDELEO LAKINI ANAPOTOKEA MTU NA KUTUMIA NJIA ZITAKAZOTUFANYA TUELEKEE KATIKA MAENDELEO HALISI WANANG'ANG'ANIA KATIKA UNAFIKI WAO. KA WALE WASIOJUA KULINDA STATUS QUO NI LAANA AMBAYO MPAKA TUTAKAPOONDOKANA NAYO NDIPO MAENDELEO YA KWELI YATAKAPOPATIKANA.SASA WATANZANIA AMABO WENGI WAO NI WANAFIKI HAWALIONI HILO WANALINDA KITU AMBACHO MPAKA TUTAKAPOONDOKANA NACHO KAMWE HATUATAFIKIA MAENDELEO YAKWELI....!!! SASA NIWAULIZE HAO WANAOTETEA UJINGA TOKA LINI NENO UDHAIFU LIKAWA TUSI... TOKA LINI!? KWA HAO WANAOONA NI DHAIFU NAOMBA KABLA HAWAJONGEA HOJA ZAO ZISIZO NA MASHIKO WAJIULIZE KWANZA TOKA LINI NENODHAIFU LIKAWA TUSI!!!? KINYUME NA HAPO ,PLEASE PLEASE, PLEASE I BEG YOU TO SHUT THE F**CK UP!!!