Saturday, December 16, 2017

Uzinduzi wa Mradi wa Kinamama Mji Mpya



Naibu Katibu Mkuu Bara na Mbunge wa Jimbo la Kibamba, Mhe. John Mnyika akikata utepe ikiwa ni ishara ya kufungua mradi wa akina mama wa Mtaa wa Mji mpya Jimbo la Kibamba.

Mradi huu ikiwa ni sehemu ya utekelezaji wa ahadi  aliyoitoa Mhe. John Mnyika na Mwenyekiti wa Serikali ya  Mtaa Mhe. Aron Moye (kushoto kwa John Mnyika) wakati wakiomba ridhaa kwa wananchi.

Mhe John Mnyika na Mhe. Aron waliahidi kusaidia kuanzisha vikundi vya akinamama vya ujasiriamali.

Akizungumza kwenye hafla fupi ya ufunguzi huo Mhe. John Mnyika aliwapongeza wakina mama hao kwa kuweza kutengeneza mfumo wa kusimamia mradi huo kabla haujaanza kwani miradi mingi imekufa kutokana na usimamizi.

Amewataka akina mama hao kuunganisha nguvu ya pamoja ili kufikia malengo waliojiwekea.

Akitoa majibu ya changamoto zilizowasilisha Mhe. Mnyika aliahidi kufatilia ujenzi wa daraja kutoka Mji Mpya kueleka barabara kuu kupitia kwa Mangi na kumuelekeza Mwenyekiti wa Serikali ya Mtaa kumpatia nakala ya maombi ya kupatiwa fedha kwaajili ya ujenzi huo aliyoiwasilisha Manispaa  kupitia kikao cha WDC ili kuweza  kuitengea fedha kwenye mfuko wa Jimbo.

Tuesday, December 5, 2017

Nasimama na Wabunge na Makamanda wetu waliokamatwa Morogoro




Nasimama na wabunge wetu wawili; Ndugu Peter Lijuakali na Susan Kiwanga, Madiwani wetu wawili na wanachama wetu 34 ambao kwa mara ya pili sasa bado wanakataliwa kupewa dhamana.
Ikumbukwe walikamatwa toka Novemba 26 mpaka sasa wananyimwa haki yao ya msingi ya kupata dhamana.
Ninaheshimu mhimili wa Mahakama; lakini kwa yaliyowahi kwisha tokea na mifano lukuki inasukuma hitaji la sauti zetu. Kumeshakuwa na njama ovu nyingi dhidi yetu wapinzani hasa ktk suala zima la utoaji wa haki ya msingi ya dhamana-inahitaji kupazwa sauti zetu na kuunganisha nguvu kukemea hili.
Tuungane ktk hili na madhila mengine mengi ya uvunjifu wa haki, demokrasia na usawa ktk kuendesha siasa nchini.
Tunahitaji siasa safi ili tuweze kupiga hatua kimaendeleo kama alivyotuasa Baba yetu, Mwl. Julius Nyerere

Thursday, August 3, 2017

MHE. JOHN MNYIKA AMTAKA RAIS ATEUE WAZIRI WA NISHATI NA MADINI KUONGOZA MAJADILIANO KUHUSU MADINI

MHE. JOHN MNYIKA AMTAKA RAIS ATEUE WAZIRI WA NISHATI NA MADINI KUONGOZA MAJADILIANO KUHUSU MADINI

Mbunge wa Jimbo la Kibamba, ambae ni Waziri kivuli wa nishati na madini, Mhe. John Mnyika, akiongea katika Mkutano wa hadhara Jana Jumatano 2/8/2017 eneo la Goba mwisho katika Jimbo la Kibamba, Mhe. Mnyika amemtaka Rais Magufuli ateue Waziri wa nishati na madini ili aongoze majadiliano kuhusu madini.

"Ni muda mrefu umepita Rais ajateua Waziri wa nishati na madini, ambae ndiye anayestahili kuongoza majadiliano kuhusu madini, badala yake anamuachia Waziri wa Katiba na Sheria kuongoza majadiliano kuhusu masuala ya madini, Ameamuachia Waziri wa Katiba na Sheria kwa sababu alikuwa kwenye tume ya mabadiliko ya Katiba, nae amekataa kuendeleza mabadiliko ya Katiba mpya" amesema Mnyika.

Amesema Serikali makini isingeanza na makinikia huku madini yanaendelea kuchimbwa na kutoka, wakati kuna makampuni mengine yanaendelea na uchimbaji, na kampuni inayoingoza kwa uzalishaji ni kampuni ya Geita Gold mine (GGM) na inaendelea na uchimbaji hakuna ufuatiliaji wala majadiliano yeyote yanayoendelea, huku Taifa likielekezwa kwenye majadiliano kuhusu makinikia badala yafanyike majadiliano kuhusu madini kwa upana wake.

 KATIBA MPYA

Mwaka 2010, akiwa Rais Kikwete, Mnyika ndiye aliyeibua mjadala kuhusu Katiba mpya ambapo ilipelekea hatua mpaka Rais Kikwete akaanzisha mchakato wa kipatikana Katiba mpya.

Mnyika ameahidi katika Bunge lijalo litakaloanza Septemba 5 mwaka huu kuanzisha tena mjadala mpya utakaopelekea kupatikana kwa Katiba mpya ambayo ndiyo suluhisho ya mambo mengi yanayoendelea.

KUHUSU MIRADI NA KERO JIMBONI
Katika mkutano huo wananchi walipata nafasi ya kuuliza maswali mbalimbali yanayohusu miradi na kero mbalimbali katika Jimbo, ambapo alisimama Mstahiki Meya wa Ubungo, Mhe. Boniface Jacob ambae alijibu maswali mbalimbali ya wananchi, pia kuwataka vijana na wakina mama kujitokeza kwa wingi kwani kuna mikopo ambayo inatolewa kwa ajili ya kufanya ujasiriamali na kujiendeleza katika mambo mbalimbali.

Na Sunday Urio
Katibu Msaidizi wa Mbunge, Jimbo la Kibamba

2 Agosti Mkutano wa Hadhara wa Mbunge: Goba Mwembe Madole








Monday, July 24, 2017

24 July: Ziara ya Ukaguzi wa Miradi katika Kata zote


Mbunge Wa jimbo la Kibamba Mh John John Mnyika leo tarehe 24/07/2017amefanya ziara ya kukagua miradi iliyofadhiliwa na Mfuko Wa Jimbo katika Kata zote sita zinazounda Ji mbo hilo ambazo ni Kata ya Saranga, Goba, Mbezi, Msigani, Kwembe na Kibamba.

Miradi hiyo ambayo ni vyoo vya Shule ya secondari Mpigimagohe , Kivuko cha Kibungobungo Kibamba, Ofisi ya Selikaliya mtaa Kinzudi Goba, Simtank Shule ya msingi msakuzi pamoja na fedha zilizoelekezwa kwenye vikundi vya ujasiliamali wanawake na vijana kwaajili ya kukuza mitaji yao.

Pia Mhe Mbunge aliwaagiza watumishi Wa Manispaa ya Ubungo kukamilisha miradi ambayo haijakamilika kwa wakati  ili kufikia malengo yaliyo kusudiwa  kupitia fedha za mfuko huo.







Tuesday, July 18, 2017

Matengenezo ya haraka ya miundo mbinu-Kata ya Saranga

Jana Julai 17 Nilitembelea Kata ya Saranga na kujionea hali duni ya miundombinu ya barabara ambazo zimeharibika vibaya sana.

Kwa hatua ya awali nimekwishafanya mawasiliano na Mkurugenzi wa Manispaa ya Ubungo na Mkurugenzi wa Dawasco ili nao watembelee na kutuma watendaji kufanya matengenezo kwa haraka.

Nimetoa mwito, maeneo yote mabovu yawekwe kifusi lakini kwa hatua ya kudumu yawekwe slabu za zege kama ilivyofanyika kwenye baadhi ya maeneo kwenye barabara hiyo.

Muhimu: 
Ziara ktk kata zingine tano ndani ya Jimbo letu la Kibamba zinakuja!

John John Mnyika,
Mbunge wa Kibamba,
Julai 18, 2017

Mazishi ya Mzee Mchungaji Mwasiwelwa




Jana, Julai 16 niliungana na wananchi wenzangu wa King'ong'o na kwingineko kumpumzisha Mzee wetu, Mch. Mwasiwelwa-Baba wa Mwenezi wetu, Perfect.

Mwenyezi Mungu amjalie pumziko la milele. Aipe pia faraja na utulivu familia na wote ambao wameguswa na kuondokewa kwa Mzee wetu.

John John Mnyika,
Mbunge wa Kibamba,
Julai 18, 2017

Uzinduzi wa albamu mbili za Baraka Mwaijande katika Kanisa la KKKT Usharika wa Temboni

Mkuu wa Jimbo, Mch.Mwangomola na Mchungaji wa Usharika wa Temboni, Mch.Lusekelo 

Baraka na Mkewe

Kwaya ya vijana
Nikiwa na Paul Clement


Jumapili Julai 16: Nilibahatika kualikwa kushiriki uzinduzi wa albamu mbili za kumsifu Mungu za kijana Baraka Mwaijande katika Kanisa la KKKT Usharika wa Temboni , Jimbo la Magharibi-Dayosisi ya Mashariki na Pwani [ndani ya Jimbo letu la Kibamba].

Nilifurahi na kufarijika sana kushuhudia  vijana wakitumia vipaji vyao kumsifu Mungu.

Baraka pia alinigusa kiupekee sana kwa ndoto yake ya kujenga kituo cha kuhudumia watoto yatima. Anafanya harambee kutekeleza azma hii. Tumuunge mkono. Kwa wenye kutamani kusikia kazi zake mbili za kumsifu Mungu au kumuunga mkono wawasiliane nae moja kwa moja: 0715-189 911

Paul Clement, alinigusa sana na wimbo wake “Amenifanyia Amani”! Hakika ana kipaji cha kipekee.

Nimefurahi pia kuwa na Baba Wachungaji, Mkuu wa Jimbo-Mch. Mwangomola, na Mkuu wa Usharika-Mch. Lusekelo na wachungaji wengine.


Naamini kila mmoja anaweza kuwa chachu ya kuiboresha jamii yetu kwa kutumia vipaji/talanta tulizopewa na MUNGU vyema.

John John Mnyika,
Mbunge wa Kibamba,
Julai 17, 2017

Friday, June 30, 2017

MUHIMU: Nini maoni yako juu ya miswada iliyowasilishwa kwa hati ya dharura


MUHIMU:

Nawaomba wananchi wenye maoni/maboresho juu ya miswada (rasilimali+madini) iliyowasilishwa bungeni wanitumie kwa:

mbungekibamba@gmail.com‬

ISOME kupitia link hii: http://parliament.go.tz

John John Mnyika,
Waziri Kivuli-Nishati na Madini,
Mbunge wa Jimbo la Kibamba


Monday, June 5, 2017

TANZIA: Mzee Philemon Ndesamburo


04 Juni, 2017: Niliweza kuwasili salama Moshi, KDC nyumbani kwa Mzee wetu Philemon Ndesamburo tayari kwa ajili ya shughuli ya kumpumzisha Mzee. Nikisaini kitabu cha maombolezo. 

Mwenyezi Mungu amjalie pumziko jema la milele.

John John MNYIKA,
Mbunge-Jimbo la Kibamba,
Moshi, Juni 05, 2017

Friday, June 2, 2017

HOTUBA YA MSEMAJI MKUU WA KAMBI RASMI YA UPINZANI BUNGENI WIZARA YA NISHATI NA MADINI MHESHIMIWA JOHN JOHN MNYIKA (MB), KUHUSU UTEKELEZAJI WA BAJETI YA WIZARA KWA MWAKA 2016/2017 NA MAKADIRIO YA MAPATO NA MATUMIZI YA WIZARA KWA MWAKA WA FEDHA 2017/ 2018

(Inatolewa chini ya 99(9) ya kanuni za Bunge, Toleo la Mwaka, 2016)
  1. A. UTANGULIZI
Mheshimiwa Spika, Awali ya yote niungane na wenye mapenzi mema katika kuomba ulinzi wa mwenyezi Mungu wakati wa kutimiza wajibu wa kibunge kwa mujibu wa Ibara ya 63 ya katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, kuishauri na kuisimamia Serikali kwa Wizara ya Nishati na Madini juu ya bajeti ya mwaka 2016/2017 na makadirio ya mapato na matumizi kwa mwaka wa fedha 2017/2018. Aidha, nitumie fursa hii kuwatakia waislamu wote mfungo mwema katika mwezi mtukufu wa Ramadhani.

Mheshimiwa Spika, Nitambue mchango Mheshimiwa John Heche, Naibu Waziri Kivuli wa Wizara ya Nishati na Madini alioutoa katika maandalizi ya hotuba hii. Aidha tuendelee kumuombea kwa Mwenyezi Mungu aweze kupona na kurejea katika utekelezaji wa majukumu yake.

Mheshimiwa Spika, naomba nitumie fursa hii kutoa pole kwa familia ya marehemu Mzee Philemon Ndesamburo, wanachama wa CHADEMA kote nchini, wananchi wa Moshi Mjini, wabunge na watanzania wote walioguswa na msiba huu. Marehemu atakumbukwa kwa mchango wake kama mmoja wa waasisi wa chama chetu, Mbunge Mstaafu na Mfanyabiashara Mashuhuri. Mwenyezi Mungu amlaze mahali pema.

  1. B. MCHAKATO WA KATIBA MPYA NA MUSTAKABALI WA MADINI, MAFUTA NA GESI ASILIA

Mheshimiwa Spika, Novemba 4, 2016 Mheshimiwa Rais alipokuwa akizungumza na watanzania kupitia vyombo vya habari, ikulu jijini Dar es salaam alinukuliwa akisema hakuwahi kuzungumzia katiba mpya wakati wa kampeni zake, kwa hiyo siyo kipaumbele chake na kwamba anachotaka kwanza ni kunyoosha nchi.

Thursday, May 25, 2017

Kutoka Bungeni: Michango yangu mbalimbali

Swali kutoka kwa Mh Mnyika

                                                   Mnyika Aunguruma bungeni

                     Mnyika; swali kuhusu Maji Kimbamba

Source Simu.tv

Sunday, May 14, 2017

Mkutano wa hadhara wa Mmbunge wa Kibamba Mbezi Mwisho May 14

 Wananchi na wabunge wao wakiwa kaatika maandamano ya kuangalia nyumba zilizochorwa alama nyekundu kwa ajili ya kubomolewa  katika maeneo ya kuanzia Kimara, Mbezi hadi Kibamba. Maanadamano haayo yaliishia Kibanda cha Mkaa baada ya hali kuwa mbaya kwa msongamano wa magari

 Naibu Katibu Mkuu wa CHADEMA na Mbunge wa Kibamba John Mnyika akiwafafanulia wananchi katika mkutano huo juu ya mipango ya  barabara na sera za nchi juu ya mipaka

                                  Mbunge wa Ubungo, Said Kubenea akitoa neno kwenye tukio hilo

 Mbunge wa Ubungo Said Kubenea na Mbunge wa Kibamba Mnyika wakiwa katika mkutano huo

 Askari wa kikosi barabarani akimuomba Mnyika kupanda gari ili kuzuia wananchi wasiendelee kuleta msongamano barabarani
Wananchi wakimlalamikia trafiki  baada ya kuamuru Mnyika kuondokaeneo hilo la Kibanda cha Mkaa ambapo maandamano hayo ya kawaida yaliishia hapo. (PICHA ZOTE NA ANDREW CHALE,MO BLOG)

Wabunge wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) John Mnyika wa Jimbo la Kibamba na Mbunge wa Jimbo la Ubungo, Saed Kubenea wamejitokeza kwenye mkutano wa wazi uliofanyika jiioni ya leo eneo la Mbezi Mwisho ambapo wamesema wapo tayari kukaa meza moja na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mh. Dkt. Magufuli ili kuangalia utaratibu mwingine wa kuwaondoa wananchi ambao wanataakiwa kuondoka kupisha maeneo ya pembezoni mwa barabara ya Morogoro, ambapo wamepewa mwezi mmoja pekee kwa hatua hiyo amewataka wananchi waliokumbwa na zoezi hilo kujitokeza Mahakama Kuu ya Ardhi.
Kauli hizo zimetolewa leo na wabunge hao akiwemo Mbunge wa Kibamba, Mh. John Mnyika ambaye ameeleza kuwa,  hapingani na Serikali, bali anataka haki itendeke kwa wananchi hao kwani wamepewa notisi ya mwezi mmoja tu na hawajajua fidia zao pia namna zoezi hilo likavyoathiri familia nyingi kwani wengine hadi sasa hawajui wataenda wapi.
“Narudia tena. Sipingani na maendeleo ya upanuzi wa barabara yetu. Ila tunaomba haki itende. Nawaombeni Madiwani andikeni barua ya kuonana na Rais pamoja na mie Mbunge wenu nitakuwepo kwenye hicho kikao. Tunahitaji haki. Kikubwa kwa sasa wananchi wote kesho asubuhi kuanzia saa mbili kwa wale waliowekewa alama ya kubomolewa tujitokeze kwa wingi Mahakama ya Ardhi kusimamisha zoezi hili kisheria” amesema Mnyika.
Hata hivyo baada ya kusema kauli hiyo na kufunga mkutano huo wa wazi, Mnyika alieleza kuwa, anataka kwenda kujionea maeneo hayo yaliyotiwa alama ya nyekundu ya X,  ndipo kundi zima la wananchi waliokuwa kwenye mkutano huo kuungana na Wabunge hao  naa kusababisha maandamano kwani wananchi wengi walijitokeza na kuunga msafara huo huku wakiimba nyimbo mbalimbalii walitembea kutoka sehemu hiyo ya Mkutano mpaka eneo la Kibanda cha Mkaa ambapo maandamano hayo yalisimama licha ya wananchi kuwa na hamu ya kutembea umbali mrefu ili kufikisha ujumbe wao.
Wananchi hao walikiwa wakisikika wakiimba “Tumechoka, Kubomolewa’ tumechoka kubomolewa”  huku wengine wakiimba “Tanzania yetu sote, kwa nini tubomolewe” hata hivyo wakati Mnyika amewatuliza wananchi waishie hapo ili yeye aondoke kuendelea na majukumu yake baada ya Askari Polisi kueleza kwamba wananchi hao wanahatarisha usalama wa mambo mengine,  Mnyika aliingia kwenye gari huku wananchi wakiwa na shahuku ya kulisukuma gari ilo, hata hivyo trafki aliamuru kuondoka mahala hapo na ndipo ukawa mwisho wa wananchi hao na kutawanyika

Mnyika ambaye pis ni Naibu Katibu Mkuu wa CHADEMA na Mbunge wa Kibamba  awali katika mkutano huo alipokea kero mbalimbali huku kero kubwa ikiwa suala hilo la wananchi hao kuwekewa alama hizo nyekundu za kutakiwa kubomolewa  pamoja na suala la Maji kwenye mabomba yao licha ya kuwekewa huduma ya mabomba.
Habari kutoka Mo Dewji Blog