Wednesday, September 30, 2015

Dondoo za mkutano na waandishi wa habari kuhusu uchaguzi



Naibu Katibu Mkuu Bara Ndugu Mnyika alifanya mkutano na waandishi wa habari jana kutokea Ngome ya UKAWA Kawe Jijini Dar .Zifuatazo ni dondoo muhimu ya mkutano huo:
 

1.Katika Magazeti Yenu Jana mlimnukuu M/kiti wa TUME akijibu tuhuma za UKAWA juu ya mazingira ya wizi wa Kura  

2.Jaji Lubuva Jana amejibu kwa wepesi tuhuma za wizi wa kura

3. Lubuva anasema ukishapiga kura rudi Nyumbani. Nawaomba vijana na wapiga kura wengine waipuuze kauli ya Jaji Lubuva!

4.Jaji Lubuva amedai yupo tayari kuziba mianya ya wizi wa kura. Nitataja mianya hiyo ili Jaji Lubuva ajibu masuala haya!Mnyika: Matokeo ya Rais kubandikwa kituoni sio jambo jipya. Ni suala la kisheria. Nawaomba watu wasome sheria ya Uchaguzi 

5.Masanduku ya kura kupelekwa kituo cha majumuisho sio jambo Jipya.

6.Lubuva anasema matokeo yatascaniwa jimboni.Hili sio jambo jipya. Mwaka 2010 matokeo yaliyoscaniwa yalikuwa tofauti na karatasi halisi

7.Jaji Lubuva aseme hadharani, ni lini wataalamu wetu wa IT wakakague na kuhakiki mfumo wa kutuma matokeo ili kuepuka goli la mkono

  • 8. mfumo wa kujumlisha kura mwaka 2010 ulikuwa na mapungufu makubwa yaliyopelekea uchakachuaji wa kura!

    9.Jaji Lubuva amesema uhakiki umefungwa, kuna jambo kubwa limejificha.Kama hakuna uhakiki daftari limeshakuwa la kudumu!

    10. Mpaka tunavyozungumza hatujakabidhiwa daftari la kudumu la wapiga kura, Takwimu zinazotolewa idadi ya wapiga kura haziaminiki!

    11. Tume iseme ni kwa nini mpaka sasa hawajatoa nakala za "soft copies" kwa vyama vya siasa ili wazihakiki?Hapa bao la mkono limejificha

    12. UKAWA na vyama vingine Lazima viende kuhakiki Database ya Tume Makao makuu. Kwanini Lubuva hataki sisi tuende kuhakiki?

    13.Jaji Lubuva anasema ipo kamati ya IT, muulizeni hiyo kamati ya IT ya vyama vya siasa inaundwa na nani?
    14.Majeshi kuandikisha namba za askari, IGP alikiri jeshi kufanya hivyo kwa baadhi ya mikoa, kuna kitu kimejificha!

    15.IGP alikiri suala hili limefanyika, msemaji wa TPDF alikanusha, kauli zao zilikinzana.Tume iseme ni kwanini majeshi yaliandika namba?

    16. Suala la kuhamisha watumishi wa Tume, limeamia kwa wakurugenzi baada ya Rais, kuteua mkurugenzi Mpya!

    17. David Radio5: Wapiga kura wa Mara ya kwanza, na wasiojua utaratibu je wanabakia wapi baada ya kupiga kura?

    18.Wapiga kura, wawe makini kuhakikisha wanapiga kura Siku ya tarehe 25 Oktoba!

    19. Daftari la kudumu halitolewi kwa wakati ili kuruhusu goli la mkono!

    20.Wapiga kura wajielekeze kuangalia majina ndani ya daftari la wapiga kura na sio orodha ya wapiga kura inayobandikwa nje ya kituo!

    21. Orodha ya wapiga kura inayobandikwa nje ya kituo inaandaliwa na manispaa, na daftari analopewa wakala limeandaliwa na Tume

    22. Tume itoe Daftari la kudumu la wapiga kura, Jaji Lubuva amesema atalitoa daftari Siku 4 kabla ya Uchaguzi, hapa amejichanganya!

    23.Hatua ya pili ni kutoa 'permanent voter register' hili ilipaswa kutolewa mapema

    24. Kuna madaftari mawili, provisional voter register, hili tulitakiwa kupewa kabla ya uhakiki wa wapiga kura, hili hatujapewa!                                                                                             25. Rai yangu kwa wana UKAWA, wasikate tamaa kufuatia matamko ya mawaziri mbalimbali

    26.Juu ya matumizi ya vyombo vya Serikali kujihusishanaUchaguzi, linaongozwa naraisi,Bunge limevunjwa ila baraza la mawaziri linaendelea

    27. Iundwe kamati ya pamoja ya vyama vya siasa ya IT ikakague Daftari na kuliboresha ili kuzuia goli la mkono!

    Swali la1: Tulianza kusema haya mambo mapema, waliamua kufumba masikio na macho!

  • Maswali:Fred kutoka Mtanzania: Kisheria mnatakiwa mpate soft copy ya Daftari baada ya Muda gani?

  • Maswali: Francis kutoka KTN: suala la uhakiki wa BVR hamuoni Siku zimebaki chache na kwanini msingeliibua suala hili mapema?

  • Mnyika: Tume iliwahi kukiri kuwa haiko huru mbele ya Tume ya Mabadiliko ya Katiba, WaTZ wasikubali faster faster hii.

  • Mnyika: Wanapeleka huu mchakato faster faster, rai yangu tusisubiri tarehe 25 Oktoba, tuanze sasa kudhibiti goli la mkono!

  • Mnyika: Ndani ya nchi tunao watazamaji wasisubiri mpaka Uchaguzi uishe, waende Tume kutazama mfumo huu wa ujumlishaji wa kura

  • Mnyika: Nawaomba 'Waangalizi wa Uchaguzi' watoe ripoti zao mapema juu ya haya masuala!

  • Mnyika: Tume ya Uchaguzi sio Mali ya watu binafsi, ni tume ya Taifa letu.

  • Mnyika: Kijana ukishaona matokeo yamebandikwa, piga picha matokeo hayo na uyatume kwenye WhatsApp!

  • Mnyika: Kama kuna MTU ataniita mchochezi kwa kusema 'first time voters' wakae mita 200 kusubiria matokeo basi atangulie mahakamani,

  • Mnyika: First time voters, kukaa ndani ni kosa kisheria, kukaa nje si kosa kisheria, kisheria wanakaa mita 200!

  • Maswali: David Radio5: UKAWA mtafanya nini endapo tume haitafanya mnayosisitiza wafanye?

  • Mnyika: Nasisitiza BVR ni Bomu la kufungwa bao la mkono, yote tuliyosema yazingatiwe na wahusika!

  • Maswali: Prosper - The Guardian: Mnataka wataalamu wa IT wakakague daftari pekee, vipi kuhusu ukaguzi wa idadi ya kura zilizopigwa?

  • Mnyika: Kama Tume haitasikiliza haya tunayosema wanajitengenezea mazingira ya kupelekwa ICC!

  • Mnyika: Local monitors wa Uchaguzi wapo wachache, wanasubiria matokeo majimboni, kila mpiga kura lazim awe monitor!

  • Mnyika: Nje ya kituo cha kupiga kura sisi wapenda Amani, tutawalinda mawakala wetu, wasirubiniwe kupokea hongo ndani ya vituo vya Uchaguzi!

  • Mnyika: Marando alisema atatangaza matokeo, sasa kwa sababu anaumwa yupo hospitali Mimi Mnyika nitayatangaza.

Monday, September 28, 2015

Baraka za Idd : Ziara mbalimbali siku ya Idd El Hajj


 Nashukuru kwa mwaliko wa kipekee na bahati ya dua njema kwangu toka kwa viongozi na waumini wa Msikiti Saranga.Ushirikiani na ukaribu wetu ambao umedumu kwa miaka sasa toka kabla ya 2005 mpaka sasa.


 Nimefurahi kwa ukaribisho nilioupata toka ktk Madrassa iliyopo Kiluvya kushiriki nao sikukuu ya Idd El Hajj jana.Ni Madrassa ambayo nimekuwa karibu nayo kwa miaka sasa (kabla ya 2005) kushiriki kadiri ya nafasi na uwezo kuiimarisha.
 
Nikizuzungumza na viongozi na waumini, msikiti wa MalambaMawili Mwisho (King'azi B). Moja ya Misikiti ambayo nimekuwa nayo karibu na kushirikiana nayo hata kabla ya kuwa Mbunge (toka kabla ya 2005) mpaka sasa.
  
Allah awajalie kila la kheri.

Wednesday, September 23, 2015

Chagua Madiwani wetu wa Kibamba

            HUMPREY ELIMKIRA SAMBO- KATA YA MBEZI
       ISRAEL AUGUSTINO MUSHI- KATA YA MSIGANI
                DWEZA HORACE KOLIMBA- KATA YA KWEMBE
           ERNEST STANLEY MGAWE- KATA YA KIBAMBA

EPHRAIM ALPHONCE KINYAFU- KATA YA SARANGA

               IBRAHIM KENYA HASSAN-KATA YA GOBA

Tuesday, September 15, 2015

Pumzika kwa amani kamanda Mohamedi Mtoi





Mazishi ya kamanda mwenzetu yalifanyika jana 14 Septemba saa 7:00 mchana kijijini kwao Mkuzi jimboni Lushoto.
Innalilah wainna ilaihi rajiun!

Wednesday, September 9, 2015

Ziara ya Mgombea Urais wa CHADEMA(UKAWA) Ng. Edward Lowassa jimboni Kibamba






Mgombea Urais kwa tiketi ya CHADEMA ndugu Edward Lowassa alifanya mkutano wa hadhara Mbezi jimboni Kibamba Jumatatu Septemba 7. Mkutano huo uliokuwa umejawa na hamasa na umati mkubwa wa aina yake ulimuombea kura Mgombea Ubunge Jimbo la Kibamba Ndugu John John Mnyika na Madiwani wake Sita pamoja na Mgombea Ubunge Jimbo la Ubungo Ndugu Saed Kubenea.

Friday, September 4, 2015

Shiriki nasi katika kampeni za Kibamba 2015



Tunaomba ushiriki wako wa dhati kwa hali na mali kufanikisha ushindi wa Mnyika Kibamba. Waweza pia saidia kusambaza na kuomba kura mitandaoni na kwa ndugu ,jamaa na marafiki kwa kutumia posters hizi katika simu whatsapp, facebook, twitter n.k.

Asante na Ubarikiwe.