Tuesday, December 31, 2013

Kheri na fanaka kwa mwaka mpya 2014. Nimerudi!

Nimerejea toka kwenye mafungo na tafakari, kumradhi kwa wote mlionikosa simuni na mtandaoni. Nawatakia mwaka mpya wenye upendo na uadilifu

Sunday, December 1, 2013

Ujenzi wa Kituo cha Polisi Kata ya Sinza-Mchango wa Mfuko wa JimboUkaguzi nilioufanya katika Kata ya Sinza; ujenzi wa kituo cha polisi kwa fedha kutoka Mfuko wa Maendeleo ya Jimbo.

Mfuko wa Jimbo umetenga milioni 10; tayari umeshatoa milioni 3.5 zilizofikisha jengo mpaka hatua hiyo. Taratibu za utoaji fedha zilikwamisha mradi toka mwezi Mei mwaka 2013.