Sunday, October 4, 2015

Dondoo za mkutano wa pili na waandishi wa habari kuhusu Uchaguzi

Naibu Katibu Mkuu Bara alifanya mkutano na waandishi wa habari kutokea Ngome ya UKAWA Kawe Jijini Dar jana 03.10.2015, zifuatazo ni dondoo za aliyoyazungumza

Mnyika: Hatujaridhika na majibu ya Jaji Lubuva kuhusu udhaifu wa BVR na uchakachuaji wa kura

Mnyika: UKAWA Tunataka tume ya Uchaguzi itupe nakala tete (soft copy) ya nakala ya Daftari la wapiga kura. Kinachoendelea ni ucheleweshaji!

Mnyika: Tume iseme kwanini hawatoi daftari la wapiga kura?Na ni lini daftari litatolewa?UKAWA haipo tayari kusubiri Siku 8 kabla ya Uchaguzi

Mnyika: Ili kuepusha vurugu kwenye Uchaguzi daftari hili litolewe kuanzia Leo!

Mnyika: Tume ya Uchaguzi waeleze kwanini wameamua kuchelewa kukutana na vyama vya siasa juu ya suala la kupewa soft copy ya Daftari!

Mnyika: Tume imejibu ipo tayari kutoa fursa ya Vyama vya siasa kukagua mfumo wa kujumlisha kura ila hawasemi ni lini? Hizi ni delay tactics

Mnyika: kuna haja ya kuwa na mashaka, mfumo wa kompyuta unaweza kuchezewa, lazima mfumo huu uhakikiwe

Mnyika: Tume imesema wana mfumo miwili ya kujumlisha kura. Lazima mfumo yote ihakikiwe na watalaamu wetu vyama vya siasa!

Mnyika: UKAWA tunasisitiza tena, ukishapiga kura, kaa mita 200 subiria matokeo, ili kuzuia mianya yote ya wizi!

Mnyika: Wananchi waendelee kupuuza kauli ya Mwenyekiti wa Tume, wasiondoke baada ya kupiga kura, wabakie mita 200 nje ya kituo kusubiria!

Mnyika: Matokeo kutangazwa na wanahabari sio hisani, ni suala la kisheria. Kutangaza matokeo itamkwe ni haki ya msingi ya kila mtu.

Mnyika: Kila Mwananchi afanye ujumlishaji wa kura  "parallel voter tabulation" ili wananchi wajue hakuna uchakachuaji na wizi wa kura!

Mnyika: Kazi pekee ya Tume iwe ni Kumtangaza Mshindi, lakini haki ya kutangaza matokeo iwe ni kwa kila mdau wakiwemo waangalizi wa Uchaguzi

Mnyika: Naungana mkono na wanahabari kuwa wasikubali watu wenye press card pekee kutangaza matokeo! Hii itapanua wigo wa Habari kusambaa

Mnyika: wanahabari Nawaomba msambae kwenye vituo mbalimbali ili muweze kutangaza matokeo!

Mnyika: Ukiangalia mazingira hivi sasa, bado hakuna mazingira mazuri ya maandalizi ya huu Uchaguzi!

Mnyika: Sera ambazo UKAWA inaendelea  kuzitangaza kupitia @edwardlowassatz sisi wengine tunaendelea kudai mazingira ya Uchaguzi yaboreshwe!

Mnyika: Rais wa nchi ameiingilia Tume tangu Uchaguzi uanze, alikataa Katiba Mpya ya wananchi, alikataa maazimio ya TCD juu ya tume huru

Mnyika: Rais alienda kinyume na ahadi zake kuhusu marekebisho ya Tume ya Uchaguzi.

Mnyika: Rais anapoenda kwenye Tamasha la Amani kesho, aombewe ili aweke mazingira mazuri ya Uchaguzi

Mnyika: Wananchi wamuombee Jaji Lubuva ili awe na ujasiri wa kutangaza matokeo ya Rais Mpya wa Tanzania

Mnyika: Kesho Rais akiongea naomba aeleze mkakati wake amejiandaaje kukabidhi Madaraka kwa Amani kufuatia Mabadiliko ya tarehe 25.10.2015

Mnyika: Jaji Lubuva alisema atakutana na vyama vya siasa ila hakutaja tarehe! Kuhusu daftari hakujibu hoja yetu ya kupewa "Daftari"


Mnyika: kama Tume ina dhamira, itoe Daftari la wapiga kura na sio orodha ya wapiga kura, waitoe hata leo!

Mnyika: Tume imesema watatoa haki kwa waliopoteza kadi za kupiga kura, wanadanganya! Wanaotakiwa kupiga kura ni walipo kwenye Daftari!

Mnyika: Tume wanachelewesha Daftari ili mawakala wetu vituoni wasiwe na daftari linalofanana na daftari la wasimamizi wa Uchaguzi

Mnyika: Tunayasema haya kwa sababu tuna uhakika wa kushinda, na Tunataka mazingira mabaya ya Uchaguzi yarekebishwe mapema

Mnyika: Daftari la wapiga kura likiwa 'bovu' tayari goli la mkono limeshafungwa! Mfumo wa kujumlisha kura ukiwa 'mbovu' ni goli la mkono!

Mnyika: Kabla ya tarehe 25 Oktoba tunasisitiza wasiondoke, wakae umbali unaoruhusiwa kisheria, walinde kura zao!

Mnyika: Wananchi wa Dar es Salaam, nawahimiza wao waende kwenye kituo cha majumuisho ya kura cha Taifa kwa niaba ya WaTZ wengine!

Mnyika: Wananchi walinde kura zao kwa amani!

Wednesday, September 30, 2015

Dondoo za mkutano na waandishi wa habari kuhusu uchaguzi



Naibu Katibu Mkuu Bara Ndugu Mnyika alifanya mkutano na waandishi wa habari jana kutokea Ngome ya UKAWA Kawe Jijini Dar .Zifuatazo ni dondoo muhimu ya mkutano huo:
 

1.Katika Magazeti Yenu Jana mlimnukuu M/kiti wa TUME akijibu tuhuma za UKAWA juu ya mazingira ya wizi wa Kura  

2.Jaji Lubuva Jana amejibu kwa wepesi tuhuma za wizi wa kura

3. Lubuva anasema ukishapiga kura rudi Nyumbani. Nawaomba vijana na wapiga kura wengine waipuuze kauli ya Jaji Lubuva!

4.Jaji Lubuva amedai yupo tayari kuziba mianya ya wizi wa kura. Nitataja mianya hiyo ili Jaji Lubuva ajibu masuala haya!Mnyika: Matokeo ya Rais kubandikwa kituoni sio jambo jipya. Ni suala la kisheria. Nawaomba watu wasome sheria ya Uchaguzi 

5.Masanduku ya kura kupelekwa kituo cha majumuisho sio jambo Jipya.

6.Lubuva anasema matokeo yatascaniwa jimboni.Hili sio jambo jipya. Mwaka 2010 matokeo yaliyoscaniwa yalikuwa tofauti na karatasi halisi

7.Jaji Lubuva aseme hadharani, ni lini wataalamu wetu wa IT wakakague na kuhakiki mfumo wa kutuma matokeo ili kuepuka goli la mkono

  • 8. mfumo wa kujumlisha kura mwaka 2010 ulikuwa na mapungufu makubwa yaliyopelekea uchakachuaji wa kura!

    9.Jaji Lubuva amesema uhakiki umefungwa, kuna jambo kubwa limejificha.Kama hakuna uhakiki daftari limeshakuwa la kudumu!

    10. Mpaka tunavyozungumza hatujakabidhiwa daftari la kudumu la wapiga kura, Takwimu zinazotolewa idadi ya wapiga kura haziaminiki!

    11. Tume iseme ni kwa nini mpaka sasa hawajatoa nakala za "soft copies" kwa vyama vya siasa ili wazihakiki?Hapa bao la mkono limejificha

    12. UKAWA na vyama vingine Lazima viende kuhakiki Database ya Tume Makao makuu. Kwanini Lubuva hataki sisi tuende kuhakiki?

    13.Jaji Lubuva anasema ipo kamati ya IT, muulizeni hiyo kamati ya IT ya vyama vya siasa inaundwa na nani?
    14.Majeshi kuandikisha namba za askari, IGP alikiri jeshi kufanya hivyo kwa baadhi ya mikoa, kuna kitu kimejificha!

    15.IGP alikiri suala hili limefanyika, msemaji wa TPDF alikanusha, kauli zao zilikinzana.Tume iseme ni kwanini majeshi yaliandika namba?

    16. Suala la kuhamisha watumishi wa Tume, limeamia kwa wakurugenzi baada ya Rais, kuteua mkurugenzi Mpya!

    17. David Radio5: Wapiga kura wa Mara ya kwanza, na wasiojua utaratibu je wanabakia wapi baada ya kupiga kura?

    18.Wapiga kura, wawe makini kuhakikisha wanapiga kura Siku ya tarehe 25 Oktoba!

    19. Daftari la kudumu halitolewi kwa wakati ili kuruhusu goli la mkono!

    20.Wapiga kura wajielekeze kuangalia majina ndani ya daftari la wapiga kura na sio orodha ya wapiga kura inayobandikwa nje ya kituo!

    21. Orodha ya wapiga kura inayobandikwa nje ya kituo inaandaliwa na manispaa, na daftari analopewa wakala limeandaliwa na Tume

    22. Tume itoe Daftari la kudumu la wapiga kura, Jaji Lubuva amesema atalitoa daftari Siku 4 kabla ya Uchaguzi, hapa amejichanganya!

    23.Hatua ya pili ni kutoa 'permanent voter register' hili ilipaswa kutolewa mapema

    24. Kuna madaftari mawili, provisional voter register, hili tulitakiwa kupewa kabla ya uhakiki wa wapiga kura, hili hatujapewa!                                                                                             25. Rai yangu kwa wana UKAWA, wasikate tamaa kufuatia matamko ya mawaziri mbalimbali

    26.Juu ya matumizi ya vyombo vya Serikali kujihusishanaUchaguzi, linaongozwa naraisi,Bunge limevunjwa ila baraza la mawaziri linaendelea

    27. Iundwe kamati ya pamoja ya vyama vya siasa ya IT ikakague Daftari na kuliboresha ili kuzuia goli la mkono!

    Swali la1: Tulianza kusema haya mambo mapema, waliamua kufumba masikio na macho!

  • Maswali:Fred kutoka Mtanzania: Kisheria mnatakiwa mpate soft copy ya Daftari baada ya Muda gani?

  • Maswali: Francis kutoka KTN: suala la uhakiki wa BVR hamuoni Siku zimebaki chache na kwanini msingeliibua suala hili mapema?

  • Mnyika: Tume iliwahi kukiri kuwa haiko huru mbele ya Tume ya Mabadiliko ya Katiba, WaTZ wasikubali faster faster hii.

  • Mnyika: Wanapeleka huu mchakato faster faster, rai yangu tusisubiri tarehe 25 Oktoba, tuanze sasa kudhibiti goli la mkono!

  • Mnyika: Ndani ya nchi tunao watazamaji wasisubiri mpaka Uchaguzi uishe, waende Tume kutazama mfumo huu wa ujumlishaji wa kura

  • Mnyika: Nawaomba 'Waangalizi wa Uchaguzi' watoe ripoti zao mapema juu ya haya masuala!

  • Mnyika: Tume ya Uchaguzi sio Mali ya watu binafsi, ni tume ya Taifa letu.

  • Mnyika: Kijana ukishaona matokeo yamebandikwa, piga picha matokeo hayo na uyatume kwenye WhatsApp!

  • Mnyika: Kama kuna MTU ataniita mchochezi kwa kusema 'first time voters' wakae mita 200 kusubiria matokeo basi atangulie mahakamani,

  • Mnyika: First time voters, kukaa ndani ni kosa kisheria, kukaa nje si kosa kisheria, kisheria wanakaa mita 200!

  • Maswali: David Radio5: UKAWA mtafanya nini endapo tume haitafanya mnayosisitiza wafanye?

  • Mnyika: Nasisitiza BVR ni Bomu la kufungwa bao la mkono, yote tuliyosema yazingatiwe na wahusika!

  • Maswali: Prosper - The Guardian: Mnataka wataalamu wa IT wakakague daftari pekee, vipi kuhusu ukaguzi wa idadi ya kura zilizopigwa?

  • Mnyika: Kama Tume haitasikiliza haya tunayosema wanajitengenezea mazingira ya kupelekwa ICC!

  • Mnyika: Local monitors wa Uchaguzi wapo wachache, wanasubiria matokeo majimboni, kila mpiga kura lazim awe monitor!

  • Mnyika: Nje ya kituo cha kupiga kura sisi wapenda Amani, tutawalinda mawakala wetu, wasirubiniwe kupokea hongo ndani ya vituo vya Uchaguzi!

  • Mnyika: Marando alisema atatangaza matokeo, sasa kwa sababu anaumwa yupo hospitali Mimi Mnyika nitayatangaza.

Monday, September 28, 2015

Baraka za Idd : Ziara mbalimbali siku ya Idd El Hajj


 Nashukuru kwa mwaliko wa kipekee na bahati ya dua njema kwangu toka kwa viongozi na waumini wa Msikiti Saranga.Ushirikiani na ukaribu wetu ambao umedumu kwa miaka sasa toka kabla ya 2005 mpaka sasa.


 Nimefurahi kwa ukaribisho nilioupata toka ktk Madrassa iliyopo Kiluvya kushiriki nao sikukuu ya Idd El Hajj jana.Ni Madrassa ambayo nimekuwa karibu nayo kwa miaka sasa (kabla ya 2005) kushiriki kadiri ya nafasi na uwezo kuiimarisha.
 
Nikizuzungumza na viongozi na waumini, msikiti wa MalambaMawili Mwisho (King'azi B). Moja ya Misikiti ambayo nimekuwa nayo karibu na kushirikiana nayo hata kabla ya kuwa Mbunge (toka kabla ya 2005) mpaka sasa.
  
Allah awajalie kila la kheri.

Wednesday, September 23, 2015

Chagua Madiwani wetu wa Kibamba

            HUMPREY ELIMKIRA SAMBO- KATA YA MBEZI
       ISRAEL AUGUSTINO MUSHI- KATA YA MSIGANI
                DWEZA HORACE KOLIMBA- KATA YA KWEMBE
           ERNEST STANLEY MGAWE- KATA YA KIBAMBA

EPHRAIM ALPHONCE KINYAFU- KATA YA SARANGA

               IBRAHIM KENYA HASSAN-KATA YA GOBA

Tuesday, September 15, 2015

Pumzika kwa amani kamanda Mohamedi Mtoi





Mazishi ya kamanda mwenzetu yalifanyika jana 14 Septemba saa 7:00 mchana kijijini kwao Mkuzi jimboni Lushoto.
Innalilah wainna ilaihi rajiun!

Wednesday, September 9, 2015

Ziara ya Mgombea Urais wa CHADEMA(UKAWA) Ng. Edward Lowassa jimboni Kibamba






Mgombea Urais kwa tiketi ya CHADEMA ndugu Edward Lowassa alifanya mkutano wa hadhara Mbezi jimboni Kibamba Jumatatu Septemba 7. Mkutano huo uliokuwa umejawa na hamasa na umati mkubwa wa aina yake ulimuombea kura Mgombea Ubunge Jimbo la Kibamba Ndugu John John Mnyika na Madiwani wake Sita pamoja na Mgombea Ubunge Jimbo la Ubungo Ndugu Saed Kubenea.

Friday, September 4, 2015

Shiriki nasi katika kampeni za Kibamba 2015



Tunaomba ushiriki wako wa dhati kwa hali na mali kufanikisha ushindi wa Mnyika Kibamba. Waweza pia saidia kusambaza na kuomba kura mitandaoni na kwa ndugu ,jamaa na marafiki kwa kutumia posters hizi katika simu whatsapp, facebook, twitter n.k.

Asante na Ubarikiwe.

Wednesday, July 1, 2015

Muswada wa kuwalinda watoa taarifa na mashuhuda (The Whistleblower and Witness Protection Act, 2015). Soma; shauri/toa maoni yako sasa!

Muswada wa kuwalinda watoa taarifa na mashuhuda 
(The Whistleblower and Witness Protection Act, 2015):
Karibu sasa kuusoma muswada ambao unajadiliwa bungeni, shiriki kwa kutoa maoni yako au ushauri. Unaweza kutuma kwa baruapepe: mnyika@yahoo.com na mbungeubungo@gmail.com

Au kuniandikia maoni yako katika mitandao ya kijamii, kwa Twitter: @jjmnyika na Facebook Page: John Mnyika.

Tushiriki sote ujenzi wa Tanzania tunayoitaka.

John Mnyika (MB)
Julai 1, 2015
Bungeni, Dodoma, Tanzania

Soma sasa Miswada mitatu muhimu: Gesi, Petroli na Uziduaji "Extractive Industries". Tushauri na kuchangia!

Muswada juu ya Petroli, 2015 (The Petroleum Act, 2015):


Muswada juu ya Usimamizi wa Mafuta na Gesi, 2015 
(The Oil and Gas Revenues Management Act, 2015):

Muswada juu ya tasnia ya Uziduaji Tanzania (The Tanzania Extractive Industries Act, 2015):

Karibuni sana wananchi kusoma miswada hii muhimu hasa kwa neema ya rasilimali asili ambazo tumejaliwa Tanzania. Kwa maoni au ushauri niandikie: mnyika@yahoo.com na copy: mbungeubungo@gmail.com

Pia unaweza kuniandikia ktk mitandao ya kijamii ya Twitter: @jjmnyika na Page ya Facebook: John Mnyika

Natanguliza shukrani zangu za dhati. 
Tushirikiane sote kuijenga nchi yetu Tanzania.

John Mnyika, (MB)
Julai 1, 2015
Bungeni, Dodoma, Tanzania

Sunday, April 19, 2015

Jana 19 Aprili: Mkutano wa hadhara Musoma


Picha ni mkutano wa hadhara uliohutubiwa na Kaimu Katibu Mkuu John Mnyika leo jioni Musoma, Uwanja wa Mkendo baada ya asubuhi kuzindua mafunzo ya timu za kampeni, viongozi wa chama na viongozi wa serikali za mitaa kwa kanda ya Serengeti (Mara, Simiyu na Shinyanga), ikiwa ni sehemu ya maandalizi ya kushinda dola na kuongoza serikali, kama yalivyozinduliwa kitaifa na Mwenyekiti wa Taifa hivi karibuni jijini Dar es Salaam.




Friday, April 17, 2015

Habari Picha: Uzinduzi wa Kanda ya Kusini



Wiki iliyopita nilipata wasaa wa kuongoza mkutano wa uzinduzi Kanda ya Kusini uliofanyika siku ya Jumapili April 12, 2015 katika uwanja wa Mashujaa.Mkutano huo wa hadhara wa uzinduzi wa Kanda ya Kusini ulijumuisha mikoa ya Lindi na Mtwara.



Wednesday, April 1, 2015

Pitia Muswada wa Sheria ya Miamala ya Kielectroniki






Wadau,
Tuupitie pia muswada wa sheria ya miamala ya kielectroniki na kuuchambua


Kuusoma ingia kwenye link hapa
(Kiswahili ni kuanzia ukurasa wa 22)


https://drive.google.com/open?id=0BxcivnLsMSPhb3hHa0VjZWJhRDg&authuser=0