Wednesday, July 27, 2016

ZIARA YA UKAGUZI WA SHULE ZILIZOKO NDANI YA KATA YA KWEMBE





OFISI YA MBUNGE JIMBO LA KIBAMBA PAMOJA NA DIWANI KATA YA KWEMBE IMEFANYA ZIARA YA UKAGUZI WA SHULE ZILIZOKO NDANI YA KATA YA KWEMBE ILI KUONA CHANGAMOTO MBALIMBALI ZINAZOKUMBA SHULE HIZO PAMOJA NA UKAGUZI WA MADAWATI YALIYOFIKISHWA KUNAKO SHULE HIZO.
Ofisi ya Mbunge jimbo LA kibamba imefanikiwa kufika ktk shule zilizoko Kata ya Kwembe huku ikiwakilishwa na mwakilishi toka ofisi ya Mbunge Ms. SUNDAY URIO pamoja na Diwani wa Kata hiyo Mhe. DWEZA KOLIMBA ili kujionea hali halisi na changamoto zinazozikabili shule hizo.
Katika ziara hiyo tumebaini changamoto zifuatazo:
*Uhaba wa madarasa ya kusomea watoto hao. Huku mhe. Diwani KOLIMBA akalijibia swala hili kwa kusema, ni kweli ameona changamoto hiyo ndani ya shule zilizoko ktk Kata na kwamba atashirikiana bega kwa bega na wananchi wa Kata yake pamoja na wadau mbalimbali wa elimu pasipo kumsahau mhe. Mbunge JOHN JOHN MNYIKA ktk kufanikisha swala zima la kuwezesha elimu bora ndani ya Kata ya Kwembe pamoja na jimbo zima LA kibamba.
*Uhaba wa madawati ya kukalia wanafunzi hao. Napo hapa mhe Diwani KOLIMBA alisema kwamba, japo kuna madawati yamewasilishwa ktk shule zilizoko ndani ya Kata yangu bado natambua uhaba huo ya kwamba hayatoshelezi...na kwasababu hiyo basi manispaa ya kinondoni chini ya Mstahiki Meya BONIFACE JACOB imefanikiwa kutengeneza madawati bora na imara zaidi ambayo yanazidi kuwasili ktk manispaa hiyo toka kwa wazabuni waliopewa tenda hiyo na muda si mrefu sana yataanza kuwasili ktk shule zetu zote zilizoko ndani ya manispaa ya kinondoni..
Na hakika tatizo LA madawati ktk shule zetu ndani ya manispaa ya kinondoni litakuwa limekwisha na kuwa historia. Hivyo msiwe na hofu wala mashaka linashughulikiwa ipasavyo.
Lakini pia tulipofika ktk shule ya MSAKUZI tulijionea mambo yafuatayo:
Ubovu wa choo cha shule ambacho kinanyufa nyingi ambacho kinahatarisha usalama wa wanafunzi wa shule hiyo kwa kujengwa chini ya kiwango hivyo kuweza kudondoka muda wowote. Pamoja na ubovu wa baadhi ya madarasa nayo kujengwa chini ya kiwango na kusababisha nyufa kubwa na madarasa hayo kuanza kumomonyoka. Huku Mwalimu mkuu na walimu wa shule hiyo kukosa ofisi na kufanyia kazi zao chini ya miti.
Nae Diwani Kolimba akamueleza Mwalimu mkuu wa shule hiyo kuwa kwanza atamfuatilia mkandarasi aliyejenga choo hicho pamoja na madarasa hayo ili kujua ni kwanini alijenga chini ya kiwango pia amelichukua na kulipeleka sehemu husika kwaajili ya utekelezaji.
Kuhusu walimu pamoja na mkuu wa shule hiyo kutokuwa na ofisi na kufanyia kazi zao chini ya miti, Diwani amesema swala hilo amelichukua na atalifanyia kazi kwa kushirikiana na wananchi wake, wadau wa elimu pamoja na mhe. Mbunge ili kuhakikisha Kata ya Kwembe inapata elimu bora kwa faida ya watoto wetu na kizazi kijacho ili kujenga taifa bora na imara.
Mwisho, mhe Diwani Kolimba aliwashukuru na kuwapongeza walimu hao kwa uvumilivu mkuu na upendo dhidi ya wanafunzi hao pamoja na changamoto zote zilizoko bado wameonesha kusonga mbele na kutimiza wajibu wao wa kuandaa kizazi kilichoelimika ambao wengi wao wameonesha kutaka kuwa viongozi wa kesho wa taifa..kama alivyo yeye Diwani wa Kata yao.

IMETOLEWA TAREHE 27/07/2016. NA OFISI YA MBUNGE JIMBO LA KIBAMBA.

Saturday, July 23, 2016

UZINDUZI WA BONANZA LA MICHEZO







Mhe. JOHN JOHN MNYIKA, MBUNGE WA JIMBO LA KIBAMBA AMEFANYA UZINDUZI WA BONANZA AMBALO LIMEANDALIWA NA CHUO CHA MLIMANI SCHOOL OF PROFESSIONAL STUDIES...BONANZA LILILOKUWA NA KAULI MBIU ISEMAYO,
"SUCCESS BEYOND PROFESSIONALISM"
Lengo la bonanza hilo ni kuleta vijana pamoja ambao ni sehemu ya jamii husika, kwa swala zima la michezo ambayo ni afya kwa mwili.
Lakini pia mhe. Mbunge John Mnyika alikuwa na haya ya kusema kwa vijana wa jimbo lake ambao wameweza kushiriki mashindano hayo na kusema:
Kwanza, amewapongeza uongozi mzima wa chuo cha MLIMANI SCHOOL OF PROFESSIONAL STUDIES kinachoongozwa na Mkuu wa chuo hicho Ndugu. Hassan Nassoro NGOMA na director of studies Ndugu. Consolata Wilfred Kimwaganje kwa kuandaa bonanza hilo na kumualika kama MGENI RASMI kupata fursa ya kushiriki na kuzindua bonanza hilo.
Kisha kuzungumza na vijana na timu zote za mpira walioshiriki katika bonanza hilo. Amewaambia vijana kuwa wao wanamchango Mkubwa kwa jamii yao, jimbo lao na taifa lao..hivyo hawapaswi kukata tamaa. Bali kutazama fursa zilizopo ambazo zinaweza kupatikana zaidi ya taaluma walizonazo ili kujikwamua kiuchumi, kielimu na kijamii ili kuleta maendeleo yenye tija kwa taifa.
Kisha kuwatakia mashindano mema yenye heri na baraka ktk bonanza hilo.
IMETOLEWA NA OFISI YA MBUNGE, JIMBO LA KIBAMBA

Friday, July 22, 2016

TUNAUKATAA UDIKTETA......



"Tunaukataa udikteta ndani ya Bunge, na tunaukataa nje ya Bunge, ndiyo maana tupo hapa mahakamani."
~Hon. John Mnyika (Mb)
"Tumefungua kesi dhidi Serikali ya Magufuli na Katibu Mkuu wa Africa Mashariki kwenye mahakama ya Haki EAC."
~Hon. John Mallya.
Naibu Katibu Mkuu wa Chadema (Bara), John Mnyika (kushoto) na Wakili wa chama hicho, John Mallya wakiwa kwenye ofisi Msajili wa Mahakama ya Afrika Mashariki jijini Arusha kufungua kesi dhidi ya Serikali kwa kupiga marufuku mikutano ya kisiasa. Picha na Filbert Rweyemamu