Makala hii niliiandika Septemba 2005 wakati huo nikiwa Mkurugenzi wa Vijana. Miaka minne imepita toka niandike makala hiyo. Nimeikumbuka makala hii leo ikiwa ni siku ambayo kombe la dunia linafika kwa mara nyingine tena Tanzania. Tufakari pamoja kuhusu kukua kwa soka la bongo katika kipindi hicho. Najua mabadiliko kadhaa yamefanyika toka wakati huo yakijikita zaidi kwenye kubadilika kwa uongozi wa TFF na makocha wa timu ya taifa kutoka wazawa kwenda wa wageni kama Maximo, pia michezo imerudishwa tena mashuleni, moja ya ahadi zilizokuwepo kwenye ilani ya CHADEMA ya mwaka 2005. Suala hili liliondolewa na serikali ya CCM na halikuwepo kwenye ilani yake wala ahadi za Kikwete za mwaka 2005, lakini nashukukuru kwamba walau serikali yake ilisikiliza sauti ya wadau kuhusu hili. Hata hivyo, oganizesheni ya soka na michezo mingine bado iko hohehahe; mathalani viwanja vya wazi vya michezo katika mitaa yetu vilivyouzwa hajirudishwa na vingine vimeendelea kuuzwa kwa ari, nguvu na kasi mpya. Uwekezaji wa soka na michezo kwa ujumla kwa vijana wadogo bado kizungumkuti na uendeshaji wa vyama vya michezo nao unaacha maswali mengine. Yote kwa yote, hebu nikukumbushe nilisema nini wakati kupitia makala inayopatikana kwa kubonyeza hapa: http://www.chadema.or.tz/makala/makala.php?id=34
No comments:
Post a Comment