Monday, September 8, 2014

Kinondoni Vijana Saccoss (KIVISA) yakabidhiwa Komputa na Kasiki (safe) na Mbunge Mnyika

Mbunge wa Jimbo la Ubungo, John Mnyika akikabidhi kompyuta na Kasiki (Safe) kwa Kinondoni Vijana Saccoss (KIVISA) ikiwa ni sehemu ya milioni 10 za CDCF tulizotenga kwenye kuchochea vijana na wanawake kujiajiri.

Mbunge wa Jimbo la Ubungo, Ndg. John Mnyika akieleza kwamba mali bila daftari hupotea bila habari na kwamba katika karne ya sasa ya Sayansi na Teknolojia daftari la kumbukumbu za mali ni kompyuta hivyo watumie kompyuta hiyo kuboresha uwekaji wa kukukumbu za mahesabu ya kuweka na kukopa SACCOS hiyo iweze kuwa endelevu na kusaidia vijana wengi zaidi. Aidha, Kasiki (safe) iwasaidie kuhifadhi fedha kwa usalama kuliko ilivyo sasa na hivyo kuhakikisha kwamba fedha zinafika kwa walengwa na kwa malengo yanayokusudiwa. 
(Pichani ni Mwenyekiti wa SACCOS (kulia kwa Mbunge Mnyika baada ya Mwenye Kanzu ambaye ni Diwani wa Kata ya Makurumla-CCM Rajab na kushoto kwangu ni Mtendaji wa Kata ya Makurumla.)
Picha ya viongozi wa KIVISA na Mbunge wa Jimbo la Ubungo, Ndg. John Mnyika baada ya makadhiano mbele ya ofisi ya Kata ya Makurumla zilizopo ofisi za SACCOS hiyo.

No comments: