Monday, January 26, 2015

Tumezindua ujenzi wa barabara za; Mbezi mwisho-Goba-Tangi Bovu, Barabara ya External –Kilungule, Barabara ya Msewe-Baruti!

Uwekaji wa jiwe la msingi kuzindua rasmi ujenzi wa barabara ya Mbezi mwisho-Goba-Tangi Bovu


Uwekaji wa jiwe la msingi kuzindua rasmi ujenzi wa barabara ya External –Kilungule

Uwekaji wa jiwe la msingi kuzindua ujenzi wa barabara ya Msewe-Baruti

 Tukisalimiana na wananchi

Mbunge wa Jimbo la Ubungo, John Mnyika, Waziri wa Ujenzi, Dkt John Magufuli na Mbunge wa Jimbo la Kawe, Halima Mdee mara baada ya kuzindua mitambo itakayofanya kazi katika ujenzi wa barabara ya Mbezi mwisho-Goba-Tangi bovu
 Mbunge wa Jimbo la Ubungo, John Mnyika akizungumza na Waziri wa Ujenzi, Dkt. Pombe Magufuli
Muonekano wa sasa katika hatua za awali za ujenzi wa barabara ya Mbezi mwisho-Goba-Tangibovu eneo la Goba

Babaraba zilizowekewa mawe ya msingi ni pamoja na ile ya Kinyerezi-Kifuru hadi Mbezi Mwisho yenye urefu wa kilometa 14.0, Kigogo-Tabata Dampo yenye urefu wa kilometa 1.6 na Kimara Baruti-Msewe hadi Chuo Kikuu cha Dar es Salaam yenye urefu wa kilomita 2.6

Barabara nyingine ni ile ya External-Kilungure hadi Kimara Korogwe kilometa 8.0, Wazo Hill-Goba hadi Mbezi Mwisho kilometa 20 na Goba-Tangi bovu kilometa 9.0

Waziri Magufuli  alisema, barabara ya Wazo Hill-Goba yenye urefu wa kilometa 20 ikikamilika kwa kiwango cha lami itaziunganisha barabara za  Bagamoyo na Morogoro ambazo zimekuwa zikikabiliwa na msongamano kwa muda mrefu.

Pia, barabara ya Kinyerezi-Kifuru hadi Mbezi Mwisho yenye urefu wa kilometa 14 itapunguza msongamano kwa kiasi kikubwa kwa kuwa itakuwa inaunganisha barabara ya Morogoro na Nyerere.

Kwa umuhimu sana, Waziri Magufuli alisisitiza; "kumbukeni mkiiba vifaa vya ujenzi hamuibi vifaa vya kampuni zinazojenga bali mnajiibia wenyewe kwa sababu hizi ni fedha za kodi ya wananchi bali kwa kufanya kazi kwa bidii na uadilifu kutawezesha ujenzi wa barabara kukamilika kwa wakati na ninyi (mafundi) kujihakikishia uhakika wa ajira"

Naye Mtendaji Mkuu wa Wakala wa Barabara nchini (TANROADS), Eng.Patrick Mfugale ameiomba serikali kuongeza bajeti ya barabara ili kuwezesha miradi ya barabara kukamilika kwa wakati na kuwataka wananchi kutoa ushirikiano kwa wakandarasi ili barabara zijengwe kwa kiwango kilichokubalika katika mikataba.

Shukrani sana kwa: http://michuzi-matukio.blogspot.com/2015/01/waziri-magufuli-azindua-miradi-sita-ya.html

2 comments:

Welcome to my Blog,Nkoha said...

nawapongeza wote kwa umoja wenu na mmefanikisha hili na zaidi utayari wa serikali na msisitizo wa chadema katika kufanikisha hili, kwakweli itatupunguzia sana kero sisi watumiaji wa hizi barabara na itapunguza kero,, nahisi kuna tatizo kwenye matoleo ya hizi barabara hasa upande wa mbezi mwisho na tangi bovu sielewi ni court injuction on something else, Mbunge clarify this.. pia naiomba serikali irelease pesa kwa wakati muafaka therwise hizi barabara zitajengwa miaka mingi hadi kukamilika, however nampongeza sana mkandarasi wa njia ya goba mbezi mwisho to Tangi bovu ana kasi na welede wa hali ya juu, Pongezi Magufuli, Mnyika na Halima Mdee kwa umoja wenu towards haya mabadiliko....

Unknown said...

Dash niliyoyataka ktk wng moyo yanatendeka kaza buti