Saturday, July 23, 2016

UZINDUZI WA BONANZA LA MICHEZOMhe. JOHN JOHN MNYIKA, MBUNGE WA JIMBO LA KIBAMBA AMEFANYA UZINDUZI WA BONANZA AMBALO LIMEANDALIWA NA CHUO CHA MLIMANI SCHOOL OF PROFESSIONAL STUDIES...BONANZA LILILOKUWA NA KAULI MBIU ISEMAYO,
"SUCCESS BEYOND PROFESSIONALISM"
Lengo la bonanza hilo ni kuleta vijana pamoja ambao ni sehemu ya jamii husika, kwa swala zima la michezo ambayo ni afya kwa mwili.
Lakini pia mhe. Mbunge John Mnyika alikuwa na haya ya kusema kwa vijana wa jimbo lake ambao wameweza kushiriki mashindano hayo na kusema:
Kwanza, amewapongeza uongozi mzima wa chuo cha MLIMANI SCHOOL OF PROFESSIONAL STUDIES kinachoongozwa na Mkuu wa chuo hicho Ndugu. Hassan Nassoro NGOMA na director of studies Ndugu. Consolata Wilfred Kimwaganje kwa kuandaa bonanza hilo na kumualika kama MGENI RASMI kupata fursa ya kushiriki na kuzindua bonanza hilo.
Kisha kuzungumza na vijana na timu zote za mpira walioshiriki katika bonanza hilo. Amewaambia vijana kuwa wao wanamchango Mkubwa kwa jamii yao, jimbo lao na taifa lao..hivyo hawapaswi kukata tamaa. Bali kutazama fursa zilizopo ambazo zinaweza kupatikana zaidi ya taaluma walizonazo ili kujikwamua kiuchumi, kielimu na kijamii ili kuleta maendeleo yenye tija kwa taifa.
Kisha kuwatakia mashindano mema yenye heri na baraka ktk bonanza hilo.
IMETOLEWA NA OFISI YA MBUNGE, JIMBO LA KIBAMBA

No comments: